< Torati 17 >

1 Haupaswi kumtolea dhabihu Yahwe Mungu wako ng'ombe au kondoo aliye na kasoro au kitu chochote kibaya, kwa kuwa hiyo itakuwa chukizo kwa Yahwe Mungu wako. 2 Kama kunapatikana miongoni mwenu, ndani ya malango ya mji wowote ambao Yahwe Mungu wenu anawapatia, mwanaume yoyote au mwanamke ambaye anafanya uovu mbele ya Yahwe Mungu wenu kuiharibu agano lake - 3 yoyote ambaye ameenda na kuabudu miungu mingine na kuisujudia, wala jua, mwezi, au kati ya jeshi la mbinguni- hakuna chochote nimekuamuru, 4 na kama ungeambiwa kuhusu hiki, au kama una mifugo- basi unapaswa kufanya uchunguzi wa makini. Kama ni kweli na hakika kwamba chukizo kama hilo limefanyika Israeli- 5 -basi utamleta huyo mwanaume au mwanamke, aliyefanya uovu huu, katika malango ya mji, kwamba mwanaume kabisa au mwanamke, na umponde huyo mtu mpaka kufa. 6 Kwa kinywa cha mashahidi wawili, au mashahidi watatu, itakuwa yeye anayepaswa kuuwawa; lakini kwa kinywa cha shahidi mmoja peke hatauwawa. 7 Mkono wa mashahidi unapaswa kuwa wa kwanza kumuuwa, na badae mkono wa watu wote; na mtamuondoa muovu miongoni mwenu. 8 Kama jambo linatokea ambalo ni gumu kwenu kufanya maamuzi- pengine swali la mauaji au kifo cha ajali, haki ya mtu mmoja na haki ya mtu mwingine, au swali moja la aina ya kuzulu kufanyika, au aina nyingine ya jambo-mambo ya utata ndani ya malango yenu, basi utapaswa kwenda kwenye eneo ambalo Yahwe Mungu wako atachagua kama patakatifu pake. 9 Utapaswa kwenda kwa makuhani, wazao wa Lawi, na kwa mwamuzi atakayetumika kwa wakati huo; mtatafuta ushauri wao, na watawapa ninyi maamuzi. 10 Mnapaswa kufuata sheria mliyopewa, katika eneo Yahwe atachagua kama patakatifu pake. Mtakuwa makini kufanya kila kitu ambacho wanawaelekeza kufanya. 11 Fuata sheria wanayowafundisha, na kufanya kulingana na maamuzi wanawapa. Msigeuke kutoka kwa kile wanawambia, kwa kulia au kushoto. 12 Yeyote anayefanya kwa kiburi, kwa kutomsikiliza kuhani anayesimama kutumika mbele ya Yahwe Mungu wako, au kwa kutomsikiliza mwamuzi- huyu mtu atakufa; mtaweka mbali uovu kutoka Israeli. 13 Watu wote wanapaswa kusikia na kuogopa, na kutofanya kwa kiburi tena. 14 Wakati mlipokuja kwenye nchi ambayo Yahwe Mungu anawapa, na wakati mnamiliki na kuanza kuishi ndani yake, na halafu unasema, 'Nitajiwekea mfalme juu yangu, kama mataifa yote yanayonizunguka mimi,' 15 basi unapaswa kwa hakika kujiwekea mfalme juu yako mtu yeyote ambaye Yahwe atachagua. Unapaswa kujiweka kama mfalme juu yako mtu yeyote kutoka miongoni mwa ndugu zenu. Haupaswi kuweka mgeni, ambaye si ndugu yenu, juu yenu. 16 Lakini hapaswi kuzidisha farasi kwa ajili yake, wala kusababisha watu kurudi Misri ili kwamba aweze kuzidisha farasi, kwa kuwa Yahwe alikwisha sema kwako, 'Unapaswa kuanzia sasa usirudi njia hiyo tena.' 17 Na hapaswi kuzidisha wake kwa ajili yake, ili kwamba moyo wake usigeuke kotoka kwa Yahwe; wala hapaswi sana kuzidisha kwa ajili yake fedha au dhahabu. 18 Wakati aketipo kwenye kiti cha enzi cha ufalme wake, anapaswa kuandika kwenye kitabu kwa ajili yake nakala ya sheria hii, kutoka kwenye sheria ambayo iko mbele ya makuhani, ambao ni Walawi. 19 Kitabu kinapaswa kuwa na yeye, na anapaswa kusoma ndani yake kwa siku zake zote, ili kwamba aweze kujifunza kumheshimu Yahwe Mungu wako, ili kwamba ashike maneno yote ya sheria hii na amri hizi, kuzishika. 20 Anapaswa kufanya hivi ili kwamba moyo wake usiinuliwe zaidi ya ndugu zake, na ili kwamba asigeuke mbali na amri, kwa kulia au kwa kushoto' kwa kusudi kwamba aweze kuzidisha siku zake katika ufalme wake, yeye na watoto wake, miongoni mwa Israel.

< Torati 17 >