< Torati 13 >

1 Kama miongoni mwenu ainuka nabii au muota ndoto, 2 na kama anawapa ishara au maajabu, na kama ishara au maajabu yanatokea, kama alivyozungumza kwenu na kusema, “Ebu tuifuate miungu mingine, ambayo hatuijui, na tuiabudu. 3 Usisikilize maneno ya nabii huyo, au kwa huyo muota ndoto, kwa kuwa Yahwe Mungu wako anakujaribu kujua kama unampenda Yahwe Mungu wako kwa moyo wako wote na roho yako yote. 4 Mtatembea baada ya Yahwe Mungu wenu, mheshimu, mzishike amri zake, na mtii sauti yake, na mtamwabudu na kushikamana naye. 5 Nabii huyo au muota ndoto atauwawa, kwa sababu amezungumza uasi dhidi ya Yahwe Mungu wenu, ambaye aliwaleta toka nchi ya Misri, na aliyewakomboa kutoka nyumba ya utumwa. Hivyo nabii anataka kuwaondoa katika njia ambayo Yahwe Mungu wenu aliwaamuru kutembea. Kwa hiyo weka mbali maouvu kutoka kwenu. 6 Tuseme kwamba ndugu yako, mwana wa mama yako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa karibu nawe, au rafiki yako ambaye ni kama roho yako, kukushawishi kwa siri na kusema, “Acha tuende na tukaabudu miungu mingine ambayo hatujazijua, wala wewe wala mababu zako- 7 Miungu yeyote ya watu ambayo imewazunguka, karibu nanyi au mbali kutoka, kutoka mwisho wa dunia kwenda mwisho mwingine wa dunia. 8 Usimkubali au kumsikiliza. Wala macho yako yasione huruma, wala hautamuacha akiba au kumficha. 9 Badala yake, utamuacha hakika; mkono wako utakuwa wa kwanza kumuua, na badae mkono wa watu wote. 10 Mtamponda mpaka kufa kwa mawe, kwa sababu amejaribu kuwaondoa kutoka kwa Yahwe Mungu wenu, ambaye aliwatoa kutoka nchi ya Misri, nje ya nyumba ya utumwa. 11 Israel yote itasikia na kuogopa, na haitaendelea kufanya aina ya uovu miongoni mwenu. 12 Kama utasikia yeyote anasema kuhusu moja ya miji yenu, kwamba Yahwe Mungu wenu anawapa kuishi ndani yake. 13 Baadhi ya wenzuni waovu wamewaacha miongoni mwenu na kuacha kwa mbali wakazi wa miji yao na kusema, “Acha tuende na kuabudu miungu mingine ambayo hamjaijua. 14 Basi utaichunguza uthibitisho, kufanya utafiti na kuipeleleza kwa kina. Wakati unagundua kwamba ni kweli na hakuna shaka kwamba chukizo hilo lililofanyika miongoni mwenu, kisha utachukua hatua. 15 Utawashambulia hakika wenyeji wa mji huo kwa makali ya upanga. Utaangamiza kabisa na watu wote walio ndani yake, pamoja na mifugo yake, pamoja na makali ya upanga. 16 Utakusanya nyara zote kutoka katikati mwa mitaa yake na utuunguza mji, pamoja na nyara zake zote - kwa kuwa Yahwe Mungu wako. Mji utakuwa mchungu wa uharibifu milele; haupaswi kujengwa tena. 17 Hakuna hata kimoja kati ya vitu hivyo vimewekwa wakfu kwa ajili ya kuangamizwa vinapaswa kugadamana kwenye mkono wako. Hii inapaswa kuwa kesi, ili kwamba Yahwe atageuka kutoka kwenye ukali wa hasira yake, kumuonyesha rehema, kuwa na huruma kwako, na kukufanya wewe kuogezeka katika idadi, kama alivyoapa kwa baba zako. 18 Atafanya hivi kwa sababu unasikiliza sauti ya Yahwe Mungu wako, kuzishika amri zake ambazo ninakuamuru leo, kufanya kile kilicho sahihi mbele ya macho ya Yahwe Mungu wako.

< Torati 13 >