< 2 Wafalme 1 >

1 Moabu aliasi dhidi ya Israeli baada ya kifo cha Ahabu. 2 Baada hapo Ahazi akaanguka chini ya dirisha lenye waya zinazikinzana kwenye chumba chake juu katika Samaria, na alikuwa amejeruhiwa. Kwa hiyo alituma wajumbe na kuwaambia, “Nendeni, muulizeni Baal Zebubu, mungu wa Ekroni, kama nitapona hili jeraha.” 3 Lakini malaika wa Yahwe wakamwambia Eliya Mtishbi, “Inuka, nenda ukaonane na wajumbe wa mfalme wa Samaria, na uwaulize, 'Je ni kwasababu hakuna Mungu katika israeli ambaye mnayekwenda kuuliza pamoja na Zebebu, mungu wa Ekroni? 4 Kwa hiyo Yahwe anasema, “Hutaweza kushuka chini kutoka kwenye kitanda ambacho ulichokipanda; badala yake, utakufa hakika."”” Baada ya hapo Eliya akaondoka. 5 wakati wale wajumbe waliporudi kwa Ahazia, akawaambia, “Kwa nini mmerudi?” 6 Wakamwambia, “mtu amekuja kuonana na sisi ambaye ametuambia, 'Turudi kwa mfalme ambaye aliyewatuma, na mkamwambie, Yahwe amesema hivi: 'Je ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli mpaka mmewatuma watu kwenda kumuuliza kwa Baal Zabubu, mungu wa Ekron? Kwa hiyo hutashuka kutoka kitanda ulichokipanda; badala yake, utakufa hakika."”” 7 Ahazi akawaambia wajumbe wake, “'Alikuwa mtu wa aina gani, yule ambaye alikuja kuonana na ninyi na akasema haya maneno kwenu?” 8 Wakamjibu, “Alikuwa amevaa kanzu yenye manyaya na alikuwa na mkanda wa ngozi kiunanoni kwake.'” Hivyo mfalme akajibu, '“Yule alikuwa Eliya Mtishbi.” 9 Ndipo mfalme akatuma nahodha wa askari hamsini kwa Elya. Nahodha akaenda mpaka kwa Eliya ambapo alipokuwa amekaa juu ya mlima. Nahodha akamwambia Eliya, “Wewe, mtu wa Mungu, mfalme amesema, 'shuka chini.'” 10 Eliya akajibu na kusema kwa nahodha, “Kama mimi ni mtu wa Mungu, moto na ushuke chini kutoka mbinguni na kukula wewe na watu wako hamsini.” Kisha moto ukashuka chini kutoka mbinguni na kumla yeye na watu wake hamsini. 11 Tena Mfalme Ahazi akamtuma nahodha mwingine pamoja na maaskari wengine hamsini. Huyu nahodha pia akasema kwa Eliya, “Wewe, mtu wa Mungu, mfalme anasema, teremka chini haraka.”' 12 Eliya akajibu na kuwaambia, “Kama mimi ni mtu wa Mungu, ngoja moto ushuke kutoka mbinguni na ukule wewe na watu wako hamsini.” Moto wa Mungu ukashuka chini tena kutoka mbinguni na kumla yeye na watu wake hamsini. 13 Bado tena mfalme alituma kundi la tatu la wapiganaji hamsini. Huyu nahodha akaenda, akaanguka mbele ya miguu ya Eliya, na kumsihi na kumwambia, “Wewe, mtu wa Mungu, Nakuomba, acha uzima wangu na uzima wa hawa watumishi wako hamsini uwe na thamani machoni kwako. 14 Ndipo, moto ukashuka chini kutoka mbinguni na kuwala wale manahodha wawili wa kwanza pamoja na watu wao, bali sasa acha uzima wangu uwe na thamani machoni kwako.” 15 Malaika wa Yahwe akamwambia Eliya, “'Nenda chini pamoja naye. Usimwogope.”' Hivyo Eliya akainuka na kwenda chini pamoja naye kwenda kwa mfalme. 16 Baadye Eliya akamwambia Ahazia, '“Hivi ndivyo Yahwe asemavyo, Umewatuma wajumbe kuzungumza pamoja na Baal-Zebubu, mungu wa Ekron. Je ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli ambaye unayeweza kumuuliza habari? Kwa hiyo sasa, hutaweza kushuka chini kutoka kwenye kitanda ulichokipanda; utakufa hakika.'” 17 Hivyo Mfalme Ahazia alikufa kulingana na neno la Yahwe ambalo Eliya alilisema. Yoramu alianza kutawala katika eneo lake, katika mwaka wa pili Yoramu mwana wa Yohoshafati mfalme wa Yuda, kwa sababu Ahazia hakuwa na mtoto. 18 Kama mambo mengine yanayomuhusu Ahazia, je hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?

< 2 Wafalme 1 >