< 2 Wafalme 9 >

1 Nabii Elisha akamwita mmoja wa watoto wa manabii na kumwambia, “Vaa kwa kwa safari, halafu chukua hii chupa ndogo ya mafuta kwenye mikono yako na uende Romoth Geliadi. 2 Wakati utakapofika, mtafute Yehu mwana wa Yehoshafati mwana wa Nimshi, na uende ukaingie na kumfanya ainuke kutoka miongoni mwa rafiki zake, na ukampeleke katika chumba cha ndani. 3 Kisha chukua ile chupa ya mafuta na imiminie kwenye kichwa chake na kusema, 'Yahwe anasema hivi: “Nimekumiminia mafuta uwe mfalme juu ya Israeli. “Halafu fungua mlango, na kukimbia; usichelewe.” 4 Basi yule kijana, yule nabii kijana, akaenda Romoth Geliadi. 5 Wakati alipofika, kumbe, wale manahodha wa lile jeshi walikuwa wamekaa. Hivyo yule nabii kijana akasema, “Nimekuja mara moja naneno kwako, nahodha.” Yehu akajibu, “kwa yupi katika sisi?” Yule nabii kijana akajibu, “Kwako nahodha.” 6 Basi Yehu akainuka na kwenda kwenye nyumba, na yule nabii akammiminia mafuta kwenye kichwa chake na kumwambia Yehu, “Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema hivi: 'Nimekumiminia mafuta uwe mfalme juu ya watu wa Yahwe, juu ya Isaraeli. 7 Wewe lazima uiue familia ya Ahabu bwana wako, ili niweze kulipiza kisasi cha damu ya watumishi wangu manabii, na damu ya watumishi wote wa Yahwe, ambao waliokuwa wameuawa kwa mkono wa Yezebeli. 8 Kwa kuwa nyumba yote ya Ahabu itaangamia, na nitamkatilia mbali kila mtoto wa kiume wa Ahabu, yeyote awe mtumwa au mtu huru. 9 Nitaifanya nyumba ya Ahabu kama nyumba ya Yerobohamu mwana wa Nebati na kama nyumba ya Baasha mwana wa Ahiya. 10 Mbwa watamla Yezebeli katika Yezreeli, na hakutakuwa na mtu wa kumzika.” Kisha nabii akafungua mlango na kukimbia. 11 Kisha Yehu akatoka kwenda kwa watumishi wa bwana wake, na mmoja akamwambia, “Je kila kitu kiko sawa? Kwa nini huyu mwenda wazimu amekuja kwako?” Yehu akawajibu, “Mnamjua huyo mtu na mambo asemayo.” 12 Wakasema, “Huo ni uongo. Tuambie.” Yehu akajibu, “Alisema hivi na vile juu yangu, na pia akasema, 'hivi ndivyo Yahwe asemavyo: Nimekumiminia mafuta kama mfalme juu ya Israeli.”” 13 Kisha kila mmoja wao akachukua vazi haraka na kuweka chini ya Yehu juu ya madaraja. Wakapiga baragumu na kusema, “Yehu ni mfalme.” 14 Katika njia hii Yehu mwana wa Yehoshafati mwana wa Nimshi akafanya njama juu ya Yoramu. Basi Yoramu alikuwa akiilinda Ramothi Gileadi, yeye na Israeli yote, kwa sababu ya Hazaeli mfalme wa Shamu, 15 lakini mfalme Yoramu alikuwa amesharudi kwa Yezreeli ili kuponywa yale majeraha aliyokuwa ameyapewa na Washami, wakati akiwa anapigana dhidi ya Hazaeli mfalme wa Shamu. Yehu akawaambia watumishi wa Yoramu, “kama hili ndilo wazo lako, kisha usimwache mtu aondoke na kwenda nje ya mji, ili aende kupeleka habari hii Yezreeli.” 16 Basi Yehu akaendesha gari la farasi mpaka Yezreeli; kwa kuwa Yoramu alikuwa amelala huko. Basi Ahazi mfalme wa Yuda alikuwa ameshuka chini kuonana na Yoramu. 17 Mlinzi alikuwa amesimama juu ya mnara katika Yezreeli, akaliona lile kundi la Yehu alipokuwa akija kwa mbali kidogo; akasema, “Naona kundi la watu wanakuja.” Yoramu akasema, “Chukua mwendesha farasi, na umtume akakutane nao; mwambie aseme, “Je mnakuja kwa amani?”” 18 Hivyo mwendesha farasi akatoka kumlaki; akasema, “Mfalme asema hivi: Je mnakuja kwa amani?”' Basi Yehu akasema, “Wewe una nini na amani? Geuka na unifuate nyuma.” Kisha yule mlinzi akamwambia mfalme, Yule mjumbe ameshaonana nao, lakini anarudi.” 19 Kisha akapeleka mpanda farasi wa pili, ambaye alikuja kwao na kusema, “Mfalme asema hivi: 'Je mnakuja na amani?”' Yehu akajibu, “Wewe una nini na amani? Geuka na kunifuata nyuma. 20 Tena yule mlinzi akatoa taarifa, “Amekwisha kuonana nao, lakini hatorudi. Kwa kuwa hilo gari la farasi limekuwa likiendeshwa ndivyo ambavyo Yehu mwana wa Nimshi aendeshavyo; anaendesha kwa kasi.” 21 Hivyo Yoramu akasema, “Andaa gari langu la farasi liwe tayari.” Wakaandaa gari lake la farasi, na Yoramu mfalme wa Israeli na Ahazi mfalme wa Yuda akaendesha, kila mmoja kwenye gari lake la farasi, kumlaki Yehu. Wakamkuta kwenye mali ya Nabothi Myezreeli. 22 Wakati Yoramu alipomuona Yehu, alisema, “Je unakuja katika hali ya amani, Yehu?” Akajibu, “Amani gani hapo, wakati uzinzi wa ukahaba hufanywa na uchawi wa mama yako Yezebeli umejaa tele?” 23 Basi Yoramu akarudisha magari yake ya farasi na kukimbia na kumwambia Ahazia, “Kuna udanganyifu, Ahazia. 24 Ndipo Yehu akauvuta upinde wake kwa nguvu zake zote na kumpiga Yoramu kati ya mabega yake; mshale ukaenda kwenye moyo wake, akaanguka chini kwenye gari lake la farasi. 25 Ndipo Yehu akamwambia Bidkari nahodha wake, “Mchukue na mtupie kwenye shamba la Nabothi Myezreeni. Fikiria kuhusu vile ambavyo wewe na mimi tulivyoendesha pamoja baada ya Ahabu baba yake, Yahwe aliuweka juu unabii dhidi yake: 26 Jana niliona damu ya Nabothi na damu ya watoto wake - asema Yahwe - na nitahakikisha unalipia hili shamba - asema Yahwe. Sasa basi, mchukue na mtupe kwenye hili shamba, sawa sawa na neno la Yahwe.” 27 Wakati Ahazi yule mfalme wa Yuda alipoliona hili, akakimbia kwa njia ya Bethi Hagani. Lakini Yehu akamfuata, na kusema, “Muulie humo kwenye gari la farasi,” na wakampiga mahali pa kupandia Guri, karibu na Ebleamu. Ahazi akakimbilia Megido na kufia pale. 28 Watumishi wake wakaubeba mwili wake kwa magari ya farasi kwenda Yerusalemu na kumzika kwenye kaburi lake pamoja na baba zake katika mji wa Daudi. 29 Basi ilikuwa mwaka wa kumi na moja wa Yoramu mwana wa Ahabu huyo Ahazia akaanza kutawala juu ya Yuda. 30 Wakati Yahu alipokuja kwa Yezebeli, Yezebeli akasikia juu ya hilo, akapaka wanja kwenye macho yake, akatengeneza nywele zake vizuri, na kuchungulia kwenye dirisha. 31 Kadiri Yehu alipokuwa akiingia kwenye lango, akamwambia, “Je unakuja kwa amani, wewe Zimri, muuaji wa bwana wako?” 32 Yehu akatazama juu ya dirisha na kusema, “Ni nani yuko upande wangu? Nani?” Matowashi wawili au watatu wakachungulia nje. 33 Basi Yehu aksema, “Mtupeni chini.” Hivyo wakamtupa Yezebeli chini, na damu yake nyingine ikamwagika kwenye ukuta na farasi, na Yehu akamkanyaga kanyaga chini ya miguu. 34 Basi Yehu akaingia hiyo sehemu, akala na kunywa. Kisha akasema, “Mtazamani sasa huyu mwanamke aliyelaaniwa na kumzika, kwa kuwa ni binti wa mfalme.” 35 Wakaenda kumzika, lakini hawakumkuta ila fuvu, miguu, na viganga vya mikono yake. 36 Basi wakarudi na kumwambia Yehu. Akasema, “Hili ndilo neno la Yahwe ambalo ameliongea kupitia Eliya Mtishbi, likisema, 'Katika nchi Yezreeli mbwa ataula mwili wa Yezebeli, 37 na mwili wa Yezebeli utakuwa kama kinyesi juu ya uso wa mashamba katika nchi ya Yezreeli, kwa hiyo basi hakuna atakayeweza kusema, “Huyu ni Yezebeli.””

< 2 Wafalme 9 >