< 2 Wafalme 20 >

1 Katika siku hizo Hezekia aliugua akawa kwenye hatari ya kufa. Hivyo Isaya mwana wa Amozi, akaja, na kumwambia, “Yahwe asema, 'Weka nyumba yako kwenye mpangilio; kwa kuwa utakufa, na hutapona.'” 2 Kisha Ahazi akageuza uso wake kwenye ukuta na kumuomba Yahwe, akisema, 3 “Tafadhali, Yahwe, ukumbuke jinsi nilivyo mwaminifu kutembea mbele yako kwa moyo wangu wote, na jinsi nilivyofanya yaliyo mazuri usoni kwako.” Kisha Hezekia akalia kwa sauti. 4 Kabla ya Isaya hajatoka nje kwenye mji wa kati, neno la Yahwe likamjia, kusema, 5 '“Rudi, na umwambie Hezekia, kiongozi wa watu wangu, 'Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Daudi babu yako, asemavyo: “Nimesikia maombi yako, na nimeyaona machozi yako. Nitakuponya katika siku ya tatu, na utapanda juu kwenye nyumba ya Yahwe. 6 Nitakuongeza miaka kumi na tano ya maisha yako, na nitakulinda na huu mji kwa ajili yangu na kwa ajili ya mtumishi wangu."”' 7 Hivyo Isaya akasema, “Chukueni mkate wa tini.” Walifanya hivyo na kuweka kwenye jipu lake, na akapona. 8 Hezekia akamwambia Isaya, “Je kutakuwa na alama gani ambayo Yahwe ataniponya, na kwamba nitapanda juu hadi kwenye hekalu la Yahwe katika siku ya tatu?” 9 Isaya akajibu, “Hii ndiyo itakuwa ishara kwako kutoka kwa Yahwe, kwamba Yahwe atafanya kitu amacho alichokisema. Je kivuli kitaenda mbele hatua saba, au kurudi nyuma hatua saba?” 10 Hezekia akajibu, “Ni kitu chepesi kwa kivuli kwenda mbele hatua kumi. Hapana, hicho kivuli kirudi nyuma hatua kumi.” 11 Hivyo Isaya nabii akamlilia Yahwe, na akaleta kivuli hatua kumi nyuma, kutoka pale ambapo zilikuwa zimevuka kwenye ngazi za Ahazi. 12 Katika kipindi hicho Merodak Baladani mfalme wa Babeli alituma barua na zawadi kwa Hezekia, kwa kuwa alisikia kwamba Hezekia alikuwa anaumwa. 13 Hezekia akasikiliza hizo barua, na kisha kuwaonyesha wajumbe sehemu zote na sehemu zake za thamani, fedha, dhahabu, manukato na marhamu na nyumba yenye ghala la silaha zake, na yote yaliyokutwa kwenye ghala za nyumba zake. Hapakuwa na kitu kwenye nyumba, wala kwenye ufalme wake wote, ambao Hezekia hakuwaonyesha. 14 Kisha Isaya akaja kwa Hezekia na kumuuliza, “Hawa watu walikuwa wanakwambiaje? Wanatokea wapi?” Hezekia aksema, “Wamekuja kutoka nchi ya mbali ya Babeli. 15 Isaya akauliza, “Wameona nini kwenye nyumba yako?” Hezekia akajibu, “Wameona kila kitu kwenye nyumba yangu. Hakuna kitu miongoni mwa vitu vyangu vya thamani ambavyo sijawaonyesha.” 16 Basi Isaya akamwambia Hezekia, “Sikiliza neno la Yahwe: 17 'Tazama siku zinakuja wakati kila kitu kwenye kwenye nyumba yako ya kifalme, vitu ambavyo babu zako walivitunza huko hadi leo, vitabebwa kwenda Babeli. Hakuna kitakachobakia, Yahwe asema. 18 Watoto waliozaliwa na wewe, ambao umewazaa wewe mwenyewe-watawachukua mbali, na watakuwa matowashi kwenye nyumba ya kifalme ya mfalme wa Babeli.'” 19 Hezekia akamwambia Isaya, “neno la Yahwe uliloliongea ni jema.” Kwa kuwa alifikiri, Je sivyo ikiwapo amani na kweli katika siku zangu?” 20 Kama kwa mambo mengine yanamuhusu Hezekia, na ushujaa wake wote, na jinsi alivyotengeza bwawa la maji na mfereji, na kuleta maji kwenye mji-hayakuandikwa kwenye kitabu cha ya matukio ya wafalme wa Yuda? 21 Hezekia akalala na babu zake, na Manase mwanae akawa mfalme katika sehemu yake.

< 2 Wafalme 20 >