< 2 Wafalme 18 >

1 Ikawa katika mwaka wa tatu wa Hoshea mwana wa Ela, mfalme wa Israeli, Hezekia mwana wa Ahazi, mfalme wa Yuda akaanza kutawala. 2 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala; alitawala miaka ishirini na tisa katika Yerusalemu. Jina la mama yake alikuwa anaitwa Abija; alikuwa binti wa Zekaria. 3 Alifanya yaliyo mema usoni pa Yahwe, kufuata mfano wa yote ambayo Daudi, babu yake, aliyoyafanya. 4 Alipaondoa mahali pa juu, akaiharibu nguzo ya jiwe, akaikata hiyo nguzo ya Ashera. Akavunja vipande vipande ile nyoka ambayo Musa aliyokuwa ameifanya, kwa sababu siku zile wana wa Israeli walikuwa wakichoma ubani katika hiyo; ilikuwa inaitwa “Nehushtani.” 5 Hezekia alimwamini Yahwe, Mungu wa Israeli, hivyo basi baada ya yeye hapakuwa kama yeye miongoni mwa wafalme wote wa Yuda, wala miongoni mwa wafalme ambao walikuwa kabla yake. 6 Aliambatana na Yahwe. Hakuacha kumfuata lakini alizifuata amri zake, ambazo Yahwe alimwamuru Musa. 7 Hivyo Yahwe alikuwa na Hezekia, kila alipokwenda alifanikiwa. Akaasi dhidi ya mfalme wa Ashuru na hakumtumikia. 8 Akawashambulia Wafilisti hadi Gaza na mipaka inayoizunguka, kutoka mnara wa walinzi hadi hadi mji wenye ngome. 9 Katika mwaka wa nne wa Mfalme Hezekia, ambao ulikuwa mwaka wa saba wa Hoshea mwana wa Ela mfalme wa Israeli, Shalmanesa mfalme wa Ashuru akapanda hadi Samaria na kuizunguka. 10 Mwishoni mwa miaka mitatu wakaichukua, katika mwaka wa sita wa Hezekia, ambao ulikuwa mwaka wa tisa wa Hoshea mfalme wa Israeli; hivi ndivyo Samaria ilivyotekwa. 11 Basi mfalme wa Ashuru akawachukua Israeli kwenda Ashuru na kuwaweka kwenye Hala, na katika mto Habori katika Gozani, na katika mji wa Wamedi. 12 Alifanya hivi kwasababu hakutii sauti ya Yahwe Mungu wao, lakini walikiuka makubaliano ya agano lake, yote yale ambayo Musa yule mtumishi wa Yahwe aliwaamuru. Walikataa kuyasikiliza au kuyafanya. 13 Kisha katika mwaka wa kumi na nne wa mfalme Hezekia, Senakerebu mfalme wa Ashuru akaishambulia miji yote yenye boma na kuwateka mateka. 14 Basi Hezekia mfalme wa Yuda akatuma neno kwenda kwa mfalalme wa Yuda akatuma neno kwa mfalme wa Ashuru, ambaye alikuwa Lachishi, akisema, “Nimekuudhi. Nichukue. Popote utakaponiweka nitavumulia”. Mfalme wa Ashuru akamtaka Hezekia mfalme wa Yuda kulipa talanta mia tatu za fedha na talanta thelathini za dhahabu. 15 Hivyo Hezekia akampatia fedha zote ambazo zilikuwa zimepatikana kwenye nyumba ya Yahwe na kawenye hazina nyumba ya mfalme. 16 Kisha Hezekia akaikata ile dhahabu kutoka kwenye milango ya hekalu la Yahwe na kutoka juu ya nguzo; akampatia dhahabu mfalme wa Ashuru. 17 Lakini mfalme wa Ashuru akalihamasisha jeshi lake kubwa, akawatuma Tartani na Rabsarisi na amiri jeshi mkuu kutoka Lakishi kwenda kwa Hezekia huko Yerusalemu. Wakasafiri hadi kwenye mabarabara na kufika nje ya Yerusalemu. Wakakaribia karibu na mfereji wa birika la juu, kwenye barabara kuu ya shamba la dobi, na kusimama hapo. 18 Wakati walipokuwa wamemwita Mfalme Hezekia, Eliakimu mwana wa Hilkia, ambaye alikuwa kiongozi wa nyumba ya mfalme na Shebna mwandishi, na Joa mwana wa Asafu, anayeandika kumbukumbu, wakatoka nje kwenda kuwalaki 19 Basi yule amiri jeshi mkuu akawaambia wamwambie Hezekia kile alichosema mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru, amesema: “Nini chanzo cha ujasiri wako? 20 Unaongea maneno yasiyo na maana, kusema lipo neno na nguvu ya vita. Sasa unamtumainia nani? Nani anakupa ujasiri wa kuasi dhidi yangu? 21 Tazama, unatumainia kutembelea fimbo ya mwanzi huu uliopondeka wa Misri, lakini kama mtu akiutegemea, utamchapa kwenye mkono wake na kuutoboa. Hicho ndicho Farao mfalme wa Misri kwa ymtu yeyote ambaye anayemtumainia. 22 Lakini kama ukiniambia, 'Tunamwamini Yahwe Mungu watu; je si yeye ambaye mahali pa juu na madhabahu Hezekia amezichukua, na kumwambia Yuda na kwa Yerusalemu, 'Lazima uabudu mbele ya hii madhabahu katika Yerusalemu'? 23 Basi kwa hiyo, nataka kukufanyia ahadi nzuri kutoka kwa bwana wangu mfalme wa Ashuru. Nitakupatia farasi elfu mbili, kama unaweza kuwatafuta kuwaendesha kwa ajili yao. 24 Wanawezaje kumpinga hata nahodha mmoja wa watumishi walio wadogo? Mmeweka tumaini lenu katika Misri kwa magari ya farasi na waendesha farasi! 25 Je nimesafiri kwenda huko juu bila Yahwe kupapigania hapa mahali na kupaharibu? Yahwe ameniambia, 'Ishambulie hii nchi na uiharibu.”' 26 Kisha Elikana mwana wa Hilkia, na Shebna, na Joa wakamwambia amiri jeshi mkuu, “Tafadhali ongea na watumishi wako katika lugha ya Kiaramu, kwa kuwa tunaielewa. Usiongee nasi katika lugha ya Yuda katika masikio ya watu ambao wako ukutani.” 27 Lakini yule amiri jeshi mkuu akawaambia, “Je bwana wangu amenituma kwa bwana wako na kuwachukua kuongea haya maneno? Je hajanituma kwa hawa watu ambao wameketi kwenye ukuta, ambao watakula kinyesi chao na kunywa mkojo wao wenyewe?” 28 Kisha yule amiri jeshi mkuu akasimama na akapiga kelele kubwa kwa lugha ya Kiyahudi, akisema, “Sikilizeni neno la mfalme mkuu, mfale wa Ashuru. 29 Mfalme asema, 'Msimwache Hezekia akawadanganya, kwa kuwa hataweza kuwaokoa kwenye nguvu yangu. 30 Msimwache Hezekia akawatumainisha katika Yahwe, akisema, “Yahwe atatuokoa hakika, na huu mji hautawekwa kwenye mkono wa mfalme wa Ashuru.'” 31 Msikilize Hezekia, kwa kuwa hivi ndivyo mfalme wa Ashuru asemavyo: 'Fanyeni amani pamoja nami na njooni kwangu. Kisha kila mmoja wenu atakula kutoka kwenye mzabibu wake mwenyewe na kutoka kwenye mtini wake mwenyewe, na kunywa kutoka kwenye maji kwenye maji ya birika lake mwenyewe. 32 Mtafanya hivyo hadi nitakapokuja na kuwachukua kwenda kwenye nchi kama nchi yenu, nchi ya nafaka na divai, nchi ya mkate na mashamba ya mizabibu, nchi ya miti ya mizaituni na asali, ili muweze kuishi na sio kufa.' Msimsikilize Hezekia wakati atakapojaribu kuwashawishi, akisema, 'Yahwe atatuokoa.' 33 Je miungu yeyote ya watu inayewaokoa kutoka kwenye nchi ya mfalme wa Ashuru? 34 Iko wapi miungu ya Hamathi na Arpadi? iko wapi miungu ya Sefarvaimu, Hena, na Iva? Je imeiokoa Samaria kutoka mkono wangu? 35 Miongoni mwa miungu yote ya nchi, je kuna mungu ambaye ameiokoa nchi yake kutoka kwenye nguvu yangu? Inawezekanaje Yahwe akaiokoa Yerusalemu kutoka kwenye uwezo wangu?” 36 Lakini watu wakabaki kimya na hawakujibu, kwa kuwa mfalme alikuwa ameamuru, “Msimjibu.” 37 Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia, ambaye alikuwa juu ya nyumba ya mfalme; Shebna yule mwandishi; na Joa mwana wa Asafu, mtunza kumbukumbu, akaja kwa Hezekia pamoja na nguo zao zilizoraruliwa, na kumpatia taarifa ya maneno ya yule amiri mkuu.

< 2 Wafalme 18 >