< 2 Wafalme 15 >

1 Katika mwaka wa ishirini na saba wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Azaria mwana wa Amazia mfalme wa Yuda akaanza kutawala. 2 Azaria alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala, na alitawala kwa mda wa miaka hamsini na mbili katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Yekolia, na alikuwa anatokea Yerusalemu. 3 Alifanya yaliyo mema machoni pa Yahwe, kama baba yake Amazia alivyofanya. 4 Lakini, mahali pa juu hapakuwa pameondolewa. Watu wakaendelea kutoa sadaka na kufukiza ubani katika mahala pa juu. 5 Yhawe akampiga mfalme hivyo basi akawa na ukoma mpaka siku ya kifo chake na alikaa kwenye nyumba ya pekee. Yothamu, mtoto wa mfalme, alikuwa juu ya watu na kuwaongoza watu wa nchi. 6 Kama kwa mambo mengine yanayomhusu Azaria, yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda? 7 Hivyo Azaria alilala pamoja na babu zake katika mji wa Daudi. Yothamu, mtoto wake, akawa mfalme katika mahala pake. 8 Katika mwaka wa thelathini na nane mwaka wa Azaria mfalme wa Yuda, Zekaria mwana wa Yeroboamu akatawala juu ya Israeli katika Samaria kwa miezi sita. 9 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe, kama baba zake waliyoyafanya. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambaye alisababisha Israeli kuasi 10 Shalumu mwana wa Yabeshi akafanya njama dhidi ya Zekaria, akamshambulia katika Ibleamu, na kumuua. Kisha akawa mfalme katika mahala pake. 11 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Zekaria, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli. 12 Hili ndilo lililokuwa neno la Yahwe ambalo aliongea na Yehu, kusema, “Kizazi chako kitakaa katika kiti cha Israeli mpaka kizazi cha nne.” Hiyo ikatokea. 13 Shalumu mwana wa Yabeshi akaanza kutawala katika mwaka wa thelathini na tisa wa Azaria mfalme wa Yuda, na kutawala kwa mwezi mmoja tu katika Samaria. 14 Menahemu mwana wa Gadi akapanda kutoka Tirza kwenda Samaria. Akamshambulia Shalumu mwana wa Yabeshi hapo, katika Samria. Akamuua na kuwa mfalme katika mahali pake. 15 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Shalumu na njama aliyoifanya, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio cha wafle wa Israeli. 16 Ndipo Menahemu akamshambulia Tifsa na wote waliokuwa pale, na mipaka yote kuzunguka Tizra, kwasababu hawakufungua kwenye mji. Hivyo akaushambulia, na akawapasua wanawake wajawazito wote katika hicho kijiji. 17 Katika mwaka wa thelathini na tisa wa Ahazia mfalme wa Yuda, Menahemu mwana wa Gadi akaanza kutawala; alitawala kwa miaka kumi katika Samaria. 18 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe. Katika maisha yake yote, hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambaye alifanya Israeli kufanya dhambi. 19 Kisha Pulu mfalme wa Ashuru akaja kinyume cha nchi, na Menahemu akampatia Pulu talanta elfu moja za fedha, hivyo msaada wa Pulu ungeweza kuwa na yeye kuimarisha utawala wa Israeli katika nchi yake. 20 Menahemu akatoza hii pesa kutoka Israeli kwa kumtaka kila mtu tajiri alipe shekeli hamsini za fedha kwake kumpatia mfalme wa Ashura. Hivyo mfalme wa Ashuru akarudi na hakukaa pale katika ile nchi. 21 Kama kwa mabo mengine yanayomuhusu Menahemu, na yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya waflme wa Israeli? 22 Hivyo Menahemu akalala pamoja na babu zake, na Pekahia mtoto wake akawa mfalme katika mahala pake. 23 Katika mwaka wa hamsini wa Azaria mfalme wa Yuda, Pekahia mwana wa Menahemu akaanza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; alitawala kwa muda wa miaka miwili. 24 Alifanya yaliyo maovu usoni pa Yahwe. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambazo kwa hizo alisababisha Israeli kufanya dhambi. 25 Pekahia alikuwa na afisa aliyekuwa anaitwa Peka mwana wa Remalia, ambaye alifanya njama dhidi yake. Pamoja na watu hamsini wa Gileadi, Peka akamuua Pekahia pamoja na Argobu na Arie katika Samaria, katika ngome ya nyumba ya mfalme. Peka akamuua alipomua Pekahia akawa mfalme katika mahala pake. 26 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Pekahia, yote aliyoyafanya, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli. 27 Katika mwaka wa hamsini na mbili wa Azia mfalme wa Yuda, Peka mwana wa Remalia akaanza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; alitawala miaka Ishirini. 28 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabati, ambaye alisababisha Israeli kufanya dhambi. 29 Katika siku za Peka mfalme wa Israeli, Tiglath Pileseri mfalme wa Ashuru akaja na kuichukua Iyoni, Abel Beth Maaka, Yanoa, Kadeshi, Hazori, Gileadi, na nchi yote ya Naftali. Akawachukua hao watu hadi Ashuru. 30 Hivyo Hoshea mwana wa Ela akafanya njama dhidi ya Peka mwana wa Remalia. Akaishambulia na kisha kumuua. Kisha akawa mfalme katika mahali pake, katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia. 31 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Peka, yote aliyoyafanya, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli. 32 Katika mwaka wa pili wa Peka mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli, Yothamu mwana wa Azaria, mfalme wa Yuda akaanza kutawala. 33 Alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala; alitawala kwa muda wa miaka kumi na sita katika Yerusalimu. Mama yake alikuwa anaitwa Yerusha; alikuwa binti ya Sadoki. 34 Yotahmu alifanya yaliyo sahihi usoni pa Yahwe. Alifuata mfano wa yote baba yake Azaria aliyofanya. 35 Ila, mahali pa juu hapakuchukuliwa. Watu walikuwa wakitio sadaka na kufukiza ubani katika mahali pa juu. Yothamu akajenga lango la juu la nyumba ya Yahwe. 36 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Yothamu, na yote aliyoyafanya, je yameandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda? 37 Katika zamani hizo Yahwe akaanza kumtuma dhidi ya Yuda Rezini mfalme wa Sahmu, na Peka mwana wa Remalia. 38 Yothamu akalala pamoja na babu zake na akazikwa pamoja na babu zake katika mji wa Daudi, babu yake. Kisha Ahazi, mtoto wake, akwa mfalme katika mhali pake.

< 2 Wafalme 15 >