< 2 Nyakati 5 >

1 Wakati ilipomalizika kazi aliyofanya Selemani kwa ajili ya Yahwe, Selemani akapeleka vitu ndani, ambavyo Daudi, baba yake, aliviweka wakifu kwa kusudi hilo, pamoja na zile fedha, dhahabu, na vyombo vyote akavileta ndani ya hazina ya nyumba ya Mungu.
Hivyo Solomoni alipomaliza kazi ya Hekalu la Bwana, akaviingiza ndani vile vitu ambavyo Daudi baba yake alikuwa ameviweka wakfu: yaani, fedha, dhahabu na samani; kisha akaviweka katika hazina za Hekalu la Mungu.
2 Kisha Selemanai akawakusanya wazee wa Israeli, wakuu wa makabila yote, na viongozi wa familia za watu wa Israeli, katika Yerusalemu, ili walilete sanduku la agano la Yahwe kutoka mji wa Daudi, ambao ni Sayuni.
Kisha Solomoni akawaita huko Yerusalemu wazee wa Israeli, viongozi wote wa makabila na wakuu wa jamaa za Waisraeli, ili walilete Sanduku la Agano la Bwana kutoka Sayuni, Mji wa Daudi.
3 Wanaume wote wa Israeli wakakusanyika mbele za mfalme katika sikukuu, ambayo ilikuwa katika mwezi wa saba.
Nao wanaume wote wa Israeli wakakusanyika kwa mfalme wakati wa sikukuu mwezi wa saba.
4 Wazee wote wa Israeli wakaja, na Walawi wakalichukua sanduku.
Wazee wote wa Israeli walipofika, Walawi wakajitwika Sanduku la Agano,
5 Wakalileta sanduku, hema ya kukutania, na vyombo vitakatifu vyote ambavyo vilikuwa ndani ya hema. Makuhani waliokuwa wa kabila la Lawi wakavileta vtu hivyo.
nao wakalipandisha Sanduku na Hema la Kukutania pamoja na vyombo vyote vitakatifu vilivyokuwa ndani yake. Makuhani, waliokuwa Walawi, walivibeba vitu hivyo,
6 Mfalme Selemanai na kusanyiko lote la Israeli wakaja pamoja, mbele ya sanduku, wakitoa sadaka za kondoo na maksai ambao hawakuweza kuhesabika.
naye Mfalme Solomoni na kusanyiko lote la Israeli waliokusanyika kumzunguka walikuwa mbele ya hilo Sanduku, nao wakatoa dhabihu nyingi za kondoo na ngʼombe ambao idadi yao haikuwezekana kuandikwa au kuhesabiwa.
7 Makuhani wakalileta sanduku la anago la Yahwe ndani mahali pake, katika chumba cha ndani cha nyumba, kwenye patakatifu pa patakatifu, chini ya mabawa ya makerubi.
Makuhani wakalileta Sanduku la Agano la Bwana hadi mahali pake ndani ya sehemu takatifu ndani ya Hekalu, yaani Patakatifu pa Patakatifu, na kuliweka chini ya mabawa ya makerubi.
8 Kwa kuwa makerubi walitandaza mabawa yao juu ya mahali pa sanduku, na walilifunika sanduku na na miti yake ya kulibebea.
Makerubi yalitandaza mabawa yao juu ya mahali pa Sanduku la Agano na kufunika Sanduku na mipiko yake ya kubebea.
9 Miti ilikuwa mirefu sana kwamba ncha zake zlionekana kutoka ile sehemu takatifu mbele ya chumba cha andani, lakini hazikuweza kuonekana kutoka nje. Zipo hapo hadi leo.
Mipiko hiyo ilikuwa mirefu sana kiasi kwamba ncha zake zilizojitokeza kutoka kwenye Sanduku, nazo zilionekana ukiwa mbele ya Patakatifu pa Patakatifu, lakini sio nje ya Mahali Patakatifu. Hiyo mipiko ipo hata leo.
10 Hapakuwa na kitu katika sanaduku isipokuwa zile meza mbili ambazo Musa aliziweka humo huko Horebu, wakati Mungu alipofanya agano na watu wa Israeli, walipotoka nje ya Misri.
Ndani ya Sanduku hapakuwepo kitu kingine chochote isipokuwa zile mbao mbili ambazo Mose alikuwa ameziweka ndani yake huko Horebu, mahali ambapo Bwana alifanya Agano na Waisraeli baada ya kutoka Misri.
11 Ilikuwa makuhani walipotoka nje ya sehemu takatifu. Makuhanai wote wliokuwepo wakajiweka wakifu wenyewe kwa Yahwe, bila kujiamuru wenyewe kulingana na sehemu zao.
Basi makuhani wakaondoka hapo Mahali Patakatifu. Makuhani wote waliokuwa huko walikuwa wamejiweka wakfu, bila kujali migawanyo yao.
12 Pia makuhani waliokuwa waimbaji, wote kwa ujumla wao, pamoja na Asafu, Hemani, Yeduthuni, na wana wao na ndugu zao, wakiwa wamevalia kitani safi na wakipiga matoazi, vinanda, na vinubi, wakaasimama upande wa mashariki wa mwisho wa madhabahu. Pamoja nao palikuwa na makuhuni 120 wakipuliza tarumbeta.
Walawi wote waliokuwa waimbaji, yaani, Asafu, Hemani, Yeduthuni, wana wa ndugu zao, walisimama upande wa mashariki wa madhabahu, wakiwa wamevaa kitani safi huku wakipiga matoazi, vinubi na zeze. Walikuwa pamoja na makuhani 120 wakipiga tarumbeta.
13 Ikawa kwamba wapuruza tarumbeta na waimbaji wakafanya mziki pamoja, wakifanya sauti moja isikike kwa ajili ya kumsifu na kumshukuru Yahwe. Walipaza sauti zao kwa tarumbeta, toazi na vyombo vingine, na wakamsifu Yahwe. Wakaimba, “Kwa maana Yeye ni mwema, kwa kuwa uaminifu wa agano lake wadumu milele.” Kisha nyumba, ile nyumba ya Yahwe, ikajawa na wingu.
Wapiga tarumbeta na waimbaji wakaungana katika sauti linganifu, ikawa kama vile ni sauti moja, wakimsifu na kumshukuru Bwana, nao alipoinua sauti zao pamoja na tarumbeta na matoazi na vyombo vingine vya uimbaji, wakamsifu Bwana wakisema: “Yeye ni mwema; upendo wake unadumu milele.” Ndipo Hekalu la Bwana likajazwa na wingu,
14 Makuhani hawakuweza kusimama ili wahudumu kwa sababu ya lile wingu, kwa maana utukufu wa Yahwe uliijaza nyumba yake.
nao makuhani hawakuweza kufanya huduma yao kwa sababu ya lile wingu, kwa kuwa utukufu wa Bwana ulijaza Hekalu la Mungu.

< 2 Nyakati 5 >