< 2 Nyakati 32 >

1 Baada ya mambo haya na matendo haya ya uaminifu, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, akaja na kuingia Yuda. Alipiga kambi kwa ajili ya kuivamia miji yenye ngome, ambayo alikusudia kuiteka kwa ajili yake. 2 Sedekia alipoona kwamba Senakeribu amekuja na kwamba amedhamiria kupigana zidi ya Yerusalemu, 3 aliwashirikisha viongozi wake na watu wake wenye nguvu kuyazuia maji ya chemichemi yaliyokuwa nje ya mji; waalimsaidia kufanya hivyo. 4 Kwa hiyo watu wengi wakakusanyika na kuyazuia maji ya chemichemi zote na mikondo yote amabayo ilikuwa inatiririka katikati ya nchi. wakasema, “Kwa nini mfalme wa Ashuru aje na kupata maji mengi?” 5 Hezekia akijipa ujasiri na kuujeenga ukuta wote uliokuwa umeangushwa chini. Akaijenga minara mirefu, na pia ukuta mwingine nje. Pia akaiimarisha Milo katika mji wa Dudi, na akafanya kiasi kikubwa cha silaha na ngao. (Maanshi ya kale yanasema hivi: “Badala ya, “akajenga minara amirefu”, baadhi ya matoleo ya zamani na kisasa yanasema, “akajenga minara mirefu juu yake”, Hii ni juu ya ukuta). 6 Akaweka maamri jeshi juu wa watu. Akawakusanya pamoja kwake katika sehemu pana kwenye lango la mji na akasema kwao kwa ujasiri. Akasema, 7 “Muwe imara na wenye ujasiri mzuri. Msiogope wala kukata tamaa kwa sababu ya mfalme wa Ashuru na jeshi lote ambalo liko naye, kwa maana kuna mtu yuko pamoja nasi ambaye ni mkuu kuliko 8 walio naye mfalme wa Ashuru. walionaye ni jeshi la mwili tu, lakini aliye nasi ni Yahwe, Mungu wetu, kwa ajili ya kutusaidia, na kupiagana vita vyetu.” Kisha watu wakajifariji wenyewe kwa maneno ya Hezekia, mfalme wa Yuda. 9 Baada ya hayo, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, aliwatuma watumishi wake kwenda Yetusalemu (sasa alikuwa mbe ya Lakishi, na jeshi lake lote lilikuwa pamoja naye), kwa Hezekia, mfaalme wa Yuda, na watu wote wa Yuda walikuwa Yerusalemu. Akasema, 10 “Hivi ndivyo Senakeribu, mfalme wa Ashuru, anasema: Ni kitu gani mnategemea kwa ajili ya kuhimili uvamizi katika Yerusalemu? 11 Je, Hezekia hawapotoshi ninyi, ili kwamba awatoe kufa kwa njaa na kiu, anapowaambia, “Yahwe Mungu wetu atatuokoa na mkono wa mfalme wa Ashuru? 12 Je, siyo Hezekia yule yule ambaye amezipeleka juu sehemu zake na madhabahu zake na kuwaamuru Yuda na Yerusalemu, juu ya madhabahu moja lazima muabudu, na juu yake lazima mchome sadaka zenu? 13 Je, hamjui mimi na babu zangu tulifanya nini kwa makundi ya wote wa inchi zingine? Je, miungu ya watu wa hizo nchi iliweza kwa njia yoyote kuziokoa nchi zao zidi ya nguvu zangu? 14 Miongoni mwa miungu yote ya mataifa hayo amabayo babu zangu waliwatekeza, je, kulikuwa na muungu yeyote aliyeweza kuwaokoa watu wake kutoka kwenye mkono wangu? Itakuwaje Mungu wenu aweze kuwakoa ninyi zidi ya nguvu zangu? 15 Sasa msimuruhusu Hezekia awadanganye au kuwashawishi katika njia hii. Msimwamini, kwa maana hakuna muungu wa taifa lolote au ufalme amewahi kuwaokoa watu wake nje ya mkono wangu, au nje ya mkono wa babu zangu. Sembuse na Mungu wenu kwa namna gani atawaokoa na mkono wangu? 16 Watumishi wa Senakeribu hata walinena mabaya zaidi juu ya Yahwe Mungu na juu ya mtumishi wake Hezekia. 17 Senakeribu pia akandika barua ili kumdhihaki Yahwe, Mungu wa Israeli, na kunena kinyume naye. Alisema, “Kama ambavyo miungu ya mataifa haikuwaokoa watu wake kutoka kwenye mkono wangu, hivyo hivyo na Mungu wa Hezekia hatawaokoa watu wake kutoka kwenye mkono wangu.” 18 Wakawalilia kwa lugha ya Wayahudi watu wa Yerusalemu waliokuwa juu ya ukuta, ili kuwaogopesha na kuwasumbua, ili kwamba waweze kuuteka mji. 19 Wakamnenea Mungu wa Yerusalemu kama walivyowanenea miungu wa Dunia, ambao ni kazi ya mikono ya wanadamu tu. 20 Hezekia, mfalme, na Isaya mwana wa Amozi, nabii, wakaomba kwa sababu ya jambo hili na wakalia hadi mbinguni. 21 Yahwe akatuma malaika, ambaye aliwaua wanaume wa kupigana vita, majemedari, na maakida wa mfalme katika kambi. Kwa hiyo Senakeribu akarudi katika nchi yake akiwa na uso wa aibu. Alipokuwa ameenda katika nyumba ya muungu wake, baadhi ya watoto wake wakamuua huko kwa upanga. 22 Katika namna hii, Yahwe akamwokoa Hezekia na wakazi wa Yerusalemu kutoka kwenye mkono wa Senakeribu, mfalme wa Ashuru, na kutoka kwenye mikono ya wengine, na akawapa pumzika juu ya kila upande. (Maandishi ya kale yanasema hivi: badala ya “akawapa pumziko juu ya kila pande”, baadhi ya matoleo ya zamani na ya kisasa yanasema, “akawaongoza juu ya kila pande”). 23 Wengi walikuwa wakileta sadaka kwa Yahwe katika Yarusalemu, na zawadi za thamani kwa Hezekia mfalme wa Yuda, kwa hiyo aliinuliwa mbele za macho ya mataifa yote toka wakati huo na kuendelea. 24 Katika siku hizo Hezekia akaugua hadi hatua ya kufa. Akaomba kwa Yahwe, ambaye alisema kwake na kumpa ishara kwamba angeponywa. 25 Lakini Hezekia hakumlipa Yahwe kwa ajili ya msaada uliotolewa kwake, kwa maana moyo wake uliinuliwa juu. 26 Kwa hiyo hasira ikaja juu yake, na juu ya Yuda na Yerusalemu. Hata hivyo, baadaye Hezekia alijinyenyekesha mwenyewe kwa jali ya kiburi cha moyo wake, wote Yeye na wakaaji wa Yerusalemu, hivyo hasira ya Yahwe haikuja juu yao wakati wa siku za Hezekia. 27 Hezekia alikuwa na utajiri mwingi sana na heshima kubwa. Alijipatia mwenyewe vyumba vya kuhifadhia kwa ajili ya fedha, dhahabu, vito vya thamani, na kwa ajili ya manukato, na kwa ajili ya ngao na na vyombo vyote vya thamani pia. 28 Pia alikuwa na nyumba za maghala kwa ajili ya mavuno ya nafaka, divai mpya, na mafuta, na malisho kwa ajili ya aina zote za wanyama. 29 Pia alikuwa na makundi katika mazizi. Zaidi ya hayo, alijipatia mwenyewe miji na makundi ya na ng'ombe kwa wingi, kwa maana Mungu alaikuwa amempa afya tele. (Maandishi ya kale yanasema hivi: Badala ya “miji” baadji ya matoleo ya kisasa yanasema “punda”, na baadhi mengine ya kisasa yanaacaha neno nzima) 30 Alikuwa ni Hezekia huyu huyu ambaye alisimamisha chemi chemi ya juu ya maji ya Gihoni, na aliye ileta moja kwa moja chini upande wa magharibi mwa mji wa Daudi. Hezekia alifanikiwa katika miradi yake yote. 31 Hata hivyo, katika jambo la mabolozi wa wakuu wa Babeli, waliotumwa kwake kuwauliza waliofahamu, kuhusu ishara za miujiza iliyokuwa imefanywa katika nchi, Mungu alimwachia mwenyewe, ili kumjaribu, na kujua yote yaliyokuwa katika moyo wake. 32 Kwa mambo mengine kuhusu Hezekia, pamoja na matendo yake ya uaminifu wa agano, unaweza kuona kwamba yameandikwa katika Maono ya Nabii Isaya Mwana wa Amozi, na katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli. 33 Hezekia akalala pamaoja na babu zake, na wakamzika katika mlima wa makaburi ya vizazi vya Daudi. Yuda wote na wakaaji wa Yerusalemu wakamheshimu katika kifo chake. Manase mwanaye akawa mfalme katika nafasi yake.

< 2 Nyakati 32 >