< 2 Nyakati 3 >

1 Kisha Selemani akaanza kuijenga nyumba ya Yahwe katika Yerusalemu juu ya Mlima Moria, ambako Yahwe alimtokea Daudi baba yake. Aliandaa sehemu ambayo Daudi aliikusudia, katika sakafu ya kupuria ya Arauna Myebusi. 2 Alianza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili, katika mwaka wa nne wa utawala wake. 3 Sasa hivi ndinyo vipimo vya ule msingi ambao Selemani alijenga kwa ajili ya nyumba ya Mungu. Akitumia mtindo wa vipimo vya zamani, urefu ulikuwa mikono sitini, na upana ulikuwa mikono ishirini. 4 Urefu wa ukumbi mbele ya nyumba ulikuwa mikono ishirini, ukilingana na upana wa nyumba, urefu wake kwenda juu pia ulikuwa mikono ishirini, na Selemani akaifunika sehemu ya ndani kwa dhahabu halisi. 5 Akailitengeneza paa la ukumbi mkuu kwa miti ya miberoshi, ambayo aliifunika kwa dhahabu halisi, na ambayo aliifunika kwa miti ya mitende na minyororo. 6 Akaipamba nyumba kwa vito vya thamani; dhahabu ilikuwa dhahabu kutoka Parvaimu. 7 Pia akazifunika boriti zake, vizingiti, kuta, na milango kwa dhahabu; akachonga makerubi juu ya kuta zake. 8 Akaijenga sehemu ya patakatifu pa patakatifu. Urefu wake ulilingana na upana wa nyumba, mikono ishirini, na upana wake pia ulikuwa mikono ishirini. Aliifunika kwa dhahabu halisi, thamani yake ilikuwa talanta mia sita. 9 Uzito wa misumari ulikuwa shekeli hamsini za dhahabu. Alizifunika sehemu za juu kwa dhahabu. 10 Akachonga makerubi wawili kwa ajili ya sehemu za patakatifu pa patakatifu, wahunzi wakayafunika kwa dhahabu. (Maandishi ya kale yanasema: makerubi wawili waliochongwa kwenye mbao). 11 Mabawa ya makerubi yalikuwa na urefu wa mikono ishirini yote kwa pamoja; bawa la kerubi mmoja lilikuwa na urefu wa mikono mitano, lilifikia kwenye ukuta wa chumba; bawa jingine lilikuwa na urefu wa mikono mitano pia. 12 Bawa la kerubi mwingine lilikuwa mikono mitano, likifikia kwenye ukuta wa chumba; bawa lake jingine lilikuwa mikono mitano pia, likigusana na bawa la kerubi wa kwanza. 13 Mabawa ya makerubi hawa yalienea jumla ya mikono mitano. Makerubi yalisimama kwa miguu yake, na nyuso zake zikiuelekea ukumbi mkuu. 14 Akatengeneza pazia la samawati, dhambarau, na sufu nyekundu, na kitani safi, na akachora makerubi juu yake. 15 Selemani pia akatengeneza nguzo mbili, kila moja ikiwa na urefu wa mikono thelathini na tano kwenda juu, kwa maana mbele ya nyumba; taji ambazo zilikuwa juu ya nguzo zilikuwa na urefu wa mikono mitano kwenda juu. 16 Akatengeneza minyororo kwa ajili ya nguzo na akaiweka juu yake, pia akatengeneza maakomamanga mia moja na akayaunganisha kwenye minyororo. 17 Akazisimamisha nguzo mbele ya hekalu, mkono wa kulia, na nyingine mkono wa kushoto; akaiita nguzo ya kulia Yakini, na nguzo ya kushoto akaiita Boazi.

< 2 Nyakati 3 >