< 2 Nyakati 28 >

1 Ahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, na akatawala miaka kumi na sita katika Yerusalemu. Hakufanya yaliyoadili katika macho ya Yahwe, kama Daudi babu yake alivyokuwa amefanya. 2 Badala yake, alitembea katika njia za wafalme wa Israeli; pia alitengeneza sanamu za kusubu kwa ajila ya Mabaali. 3 Zaidi ya hayo, akafukiza uvumba katika bonde la Beni Hinomu na akawaweka watoto wake ndani ya moto, kwa mjibu wa desturi za uzinzi za watu ambao Yahwe aliwafukuza nje ya nchi zao mbele za watu wa Israeli. 4 Akatoa sadaka na kufukiza uvumba katika sehemu za juu na juu ya vilima na chini ya kila mti wenye majani mabichi. 5 Kwa hiyo Yahwe Mungu wa Ahazi, akamweka katika mikono ya mfalme wa Shamu. Waaramu wakamshinda na kuchukua kutoka kwake kundi kubwa la mateka, wakawapeleka Damesiki. Ahazi pia aliwekwa katika mikono ya mfalme wa Israeli ambaye alimshinda kwa mauji makuu. 6 Kwa maana Peka mwana wa Remalia, aliwaua katika Yuda wanajeshi 120, 00 kwa siku moja, wote walikuwa wanaume hodari, kwa maana walikuwa wamemsahau Yahwe, Mungu wa babu zao. 7 Zikri, mtu mwenye nguvu kutoka Efraimu, akawaua Maaseya mwana wa mfalme, Azrikamu, mwangalizi mkuu wa ikulu, na Elkana, ambaye alikuwa karibu na mfalme. 8 Jeshsi la Israeli likachukua mateka kutoka kwa ndugu zao 200, 000 wake, wana, na mabinti. Pia wakachukua nyara nyingi, ambazo walipeleka Samaria. 9 Lakini nabii wa Yahwe alikuwapo huko, jina lake aliitwa Odedi. Alikwenda nje kukutana na jeshi likiingia Samaria. Akawaambia, “Kwa sababu Yahwe, Mungu wa babu zenu, alikuwa na hasiri na Yuda, akawatia katika mikono yenu. Lakini mmewaua katika hasira inayofika juu mbinguni. 10 Sasa ninyi badala ya kuwahifadhi wanaume na wanawake wa Yuda na Yerusalemu kama watumwa wenu. Lakini je hamko na hatia ya dhambi zenu zidi ya Yahwe Mungu wenu? 11 Sasa basi, nisikilizeni: warudisheni wafubgwa, ambao mmewachukua wa ndugu zenu, kwa maana ghadhabu ya Yahwe iko juu yenu.” 12 Kisha baadhi ya viongozi wa watu wa Efraimu—Azaria mwana wa Yohanani, Berekia mwana wa Meshiremothi, na Yehizikia mwana wa Shalumu, na Amasa mwana wa Hadlai, wakasimama kinyume na wale waliorudi kutoka vitani. 13 Wakasema kwao, “Lazimaa msiwaleta wafungwa hapa, kwa kuwa mlikusudia jambo ambalo litaleta juu yetu dhambi dhidi ya Yahwe, kuongeza dhambi juu yetu na makosa yetu, kwa maana makosa yetu ni makuu, na kuna hasira kali dhidi ya Israeli.” 14 Hivyo watu wenye silaha wakawaacha wafungwa na mateka mbele ya viongozi wa Israeli na kusanyiko lote 15 Watu ambao walipangwa kwa majina wakanyanyuka na kuwachukua wafungwa, na kuwavika wote waliokuwa uchi miongoni mwa mateka. Wakawavika na kuwapa viatu. Wakawapa chakula wale na kunywa. Wakawahudumia majeraha yao na kuwaweka waliodhaifu juu ya punda. Wakawarudisha kwenye familia zao katika Yeriko, (Ulioitwa mji wa mitende). Kisha wakarudi Samaria. 16 Wakati huo Mfalme Ahazi akatuma wajumbe kwa wafalme wa Ashuru kuwaomba wamsaidie. 17 Kwa maana Waedomu walikuwa wamekuja tena na kuvamia Yuda, wakachukua wafungwa. 18 Wafilisti pia wakavamia miji ya nchi ya chini na ya Negebu ya Yuda. Waliichukua Beth-shemeshi, Ayaloni, Giderothi, SoKo pamoja na vijiji vyake, Timna pamoja na vijiji vyake. Wakaenda kuishi katika sehemu hizo. 19 Kwa kuwa Yahwe aliishusha chini Yuda kwa sababu ya Ahazi, mfalme wa Israeli; kwa maana alikuwa ametenda maovu katika Yuda na alikuwa ametenda dhambi nzito sana dhidi ya Yahwe. 20 Tiglath-pileseri, mfalme wa Ashuru, akaja kwake na akampa tabu badala ya kumpa nguvu. 21 Kwa kuwa Ahazi aliteka nyara nyumba ya Yahwe na nyumba ya mfalme na viongozi, kwa ajili ya kuvitoa vitu vya thamani kwa mfalme wa Ashuru. Lakini kufanya hivyo hakukumfaidisha yeye. 22 Mfalme Ahazi huyu huyu akatenda dhambi hata zaidi dhidi ya Yahwe katika muda wa mateso yake. 23 Kwa maana aliwatolea dhabihu mingu wa Dameski, miungu ambao walimshinda. Akasema, “Kwa sababu miungu wa mfalme wa Aramu waliwasaidia, nitawatolea sadaka ili wanisaidie.” Lakini walikuwa watesi wake na Israeli yote. 24 Ahazi akazikusanya pamoja samani za nyumba ya Mungu na kuzikata vipande vipande. Akaifunga milango ya nyumba ya Yahwe na kuzitengeneza madhabahu kwa ajili yake mwenyewe katika kila kona ya Yerusalemu. 25 Katika kila mji wa Yuda akafanya sehemu za juu kwa ajili ya kutolea sadaka za kuteketezwa kwa miungu wengine. Akamfanya Yahwe, Mungu wa babu zake, akasirike. 26 Sasa matendo yake yaliyobaki, na njia zake zote, mwanzo na mwisho, ona, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli. 27 Ahazi akalala pamoja na babu zake, na wakamzika katika mji, katika Yerusalemu, lakini hawakumleta kwenye makaburi ya wafalme wa Israeli. Hezekia, mwanaye, akawa mfamle katika nafasi yake.

< 2 Nyakati 28 >