< 2 Nyakati 25 >

1 Amaza alikuwa na umri wa amiaka ishirini na na tano alipoanza kutawala; alitawala miaka ishini na tisa katika Yerusalemu. Jina la mama yake lilikuwa Yehoadani, wa Yerusalemu.
Amasias was five and twenty years old when he began to reign, and he reigned nine and twenty years in Jerusalem, the name of his mother was Joadan of Jerusalem.
2 Alifanya yaliyokuwa sahihi katika macho ya Yahwe, lakini siyo kwa moyo uliojitoa kikamilifu.
And he did what was good in the sight of the Lord: but yet not with a perfect heart.
3 Ikawa kwamba mapema utawala wake ulipokuwa umeimarika, aliwaua watumishi ambao walikuwa wamemuua baba yake, mfalme.
And when he saw himself strengthened in his kingdom, he put to death the servants that had slain the king his father.
4 Lakini hakuwaua watoto wa wale wauaji, bali alitenda kama kama ilivyoaandikwa katika sheria, katika kitabu cha Musa, kama Yahwe alivyokuwa ameamru. “Baba hatajuta kwa ajili ya watoto, wala watoto hawatakufa kwa ajili ya baba zao. Badala yake, kila mtu lazima afe kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe”.
But he slew not their children, as it is written in the book of the law of Moses, where the Lord commanded, saying: The fathers shall not be slain for the children, nor the children for their fathers, but every man shall die for his own sin.
5 Aidha, Amazia aliwakusanya Yuda pamoja, na akawaandikisha kwa kufuata nyumba za babu zao, chini ya maakida wa maelfu na maakida wa mamia —wote wa Yuda na wa Benyamini. Akawahesabu kuanzia wa mika ishirini na kuendelea, na akawaona wako 300, 000 wanaume waliochaguliwa, wawezaoa kwenda vitani, walioweza kushika mkuki na ngao.
Amasias therefore gathered Juda together, and appointed them by families, and captains of thousands and of hundreds in all Juda, and Benjamin: and he numbered them from twenty years old and upwards, and found three hundred thousand young men that could go out to battle, and could hold the spear and shield.
6 Pia alikodi wanaume wa kupigana 100, 000 kutoka Israeli kwa fedha mia moja.
He hired also of Israel a hundred thousand valiant men, for a hundred talents of silver.
7 Lakini mtu wa Mungu alikuja kwake na kusema, “Mfalme, usiliache jeshi la Istaeli kwenda nawe, kwa maana Yahwe hayupo pamoja na Israeli -wala na mtu Yeyote wa Efraimu.
But a man of God came to him, and said: O king, let not the army of Israel go out with thee, for the Lord is not with Israel, and all the children of Ephraim:
8 Lakini hata kama mtaenda na mkiwa wenye ushupavu na imara katika vita, Mungu atawatupa chini mbele ya adui, kwa maana Mungu ana nguvu za kusaidia, na nguvu za kurusha chini”.
And if thou think that battles consist in the strength of the army, God will make thee to be overcome by the enemies: for it belongeth to God both to help, and to put to flight.
9 Amazia akasema kwa mtu wa Mungu, “Lakini tutafanyaje kuhusu talanta mia moja nilizowapa jeshi la Israeli? Mtu wa Mungu akajibu, Yahwe anauwezo wa kukupa vingi zaidi kuliko hivyo.”
And Amasias said to the man of God: What will then become of the hundred talents which I have given to the soldiers of Israeli and the man of God answered him: The Lord is rich enough to be able to give thee much more than this.
10 Kwa hiyo Amazia akalitenganisha jeshi lilokuja kwake kutoka Efraimu; akawarudisha nyumbani tena. Hivyo hasira yao iliwaka sana zidi ya Yuda, na walirudi nyumbani kwa hasara kali.
Then Amasias separated the army, that came to him out of Ephraim, to go home again: but they being much enraged against Juda, returned to their own country.
11 Amazia akajipa ujasiri na kuwaongoza watu wake kwenda nje kwenye bonde la chumvi, huko akawashinda wanaueme elfu kumi wa Seiri.
And Amasias taking courage led forth his people, and went to the vale of saltpits, and slew of the children of Seir ten thousand.
12 Jeshi la Yuda likawachukua elfu kumi wengine wakiwa hai. Wakawapeleka juu ya mwamba na kuwarushwa chini kutoka huko, hivyo wote wakavunjika vunjika katika vipande.
And other ten thousand men the sons of Juda took, and brought to the steep of a certain rock, and cast them down headlong from the top, and they all were broken to pieces.
13 Lakini watu wa jeshi ambalo Amazia alilirudisha, ili kwamba wasiende naye vitani, wakauvamia mji Yuda kuanzia Somaria hadi Beth- horoni. Wakawapiga watu elfu tatu na kuwateka wengi sana.
But that army which Amasias had sent back, that they should not go with him to battle, spread themselves among the cities of Juda, from Samaria to Beth-horon, and having killed three thousand took away much spoil.
14 Sasa ikawa kwamba baada ya Amazia kurudi kutoka kuwachinja Waedomu, akaileta miungu ya watu wa Seiri, na kuisimamisha iwe miungu yake. Akainama chini mbele ya hiyo miungu na kuitolea sadaka za uvumba.
But Amasias after he had slain the Edomites, set up the gods of the children of Seir, which he had brought thence, to be his gods, and adored them, and burnt incense to them.
15 Hivyo hasira ya Yahwe ikawaka zidi ya Amazia. Akamtuma nabii kwake, ambaye alisema, “Kwa nini umeitafuta miungu ya watu ambayo haikuwaokoa hata watu wake yenyewe zidi ya mkono wako?”
Wherefore the Lord being angry against Amasias, sent a prophet to him, to say to him: Why hast thou adored gods that have not delivered their own people out of thy hand?
16 Akiwa kwamaba yule nabii alipokuwa anaongea naye, mfalme akamwambia, “Je, wewe tumekufanya kuwa mshauri wa mfalme? Acha! Kwa nini ujitakie kuuawa?” Kisha nabii akaacha na kusema, ninajua kwamba Mungu ameamua kukuangaamiza kwa sababu umefanya tendo hili na hujasikilisa ushauri wangu.”
And when he spoke these things, he answered him: Art thou the king’s counsellor? be quiet, lest I kill thee. And the prophet departing, said: I know that God is minded to kill thee, because thou hast done this evil, and moreover hast not hearkened to my counsel.
17 Kisha Amazia akashauriana na washauri na kutuma wajumbe kwa Yehoashi mwana wa Yehoahazi mwana wa Yehu, mfalme wa Israel. akisema, “Njoni, tukutane uso kwa uso katika vita”.
Then Amasias king of Juda taking very bad counsel, sent to Joas the son of Joachaz the son of Jehu, king of Israel, saying: Come, let us see one another.
18 Lakini Yehoashi mfalme wa Israeli akatuma wajumbe kwa Amaziahi mfalme wa Yuda, akisema, Mbaruti uliokuwa Lebanoni ulituma ujumbe kwa mwerezi ulioko Lebanoni, ukisema, Mtoe binti yako kwa mwanangu awe mke wake; lakini akapita hayawani katika Lebanoni akatembea na kuukanyaga chini mbaruti.
But he sent back the messengers, saying: The thistle that is in Libanus, sent to the cedar in Libanus, saying: Give thy daughter to my son to wife: and behold the beasts that were in the wood of Libanus passed by, and trod down the thistle.
19 Umesema, 'Ona, nimeipiga Edomu,' na moyo wako umekuinua juu. Jipe fahari katika ushindi wako, lakini ukae nyumbani, kwa maana ni kwa nini ujisababishie matatizo mwenyewe na kuanguka, wote wewe na Yuda pamoja nawe?'
Thou hast said: I have overthrown Edom, and therefore thy heart is lifted up with pride: stay at home, why dost thou provoke evil against thee, that both thou shouldst fall and Juda with thee.
20 Lakini Amazia hakusikiliza, kwa sababu tukio hili lilikuwa limetoka kwa Mungu, ili awatie Waisraeli katika mkono wa adui zao, kwa sababu walikuwa wametafuta ushauri kutoka kwa miungu ya Edomu.
Amasias would not hearken to him, because it was the Lord’s will that he should be delivered into the hands of enemies, because of the gods of Edom.
21 Kwa hiyo, Yehoashsi, mfalme wa Israeli, akavamia; yeye na Amazia, mfalme wa Yuda, wakakutana uso kwa uso huko Beth -shemishi, ulioko Yuda.
So Joas king of Israel went up, and they presented themselves to be seen by one another: and Amasias king of Juda was in Bethsames of Juda:
22 Yuda akashindwa mbele za Israeli, na kila mtu akarudi nyumbani.
And Juda fell before Israel and they fled to their dwellings.
23 Yehoashi, mfalme wa Israeli, akamkamata Amazia mwana wa Yehoashi mana wa Ahazia, mfalme wa Yuda, huko Beth - shemeshi. Akamleta Yerusalemu na kuuangusha chini ukuta wa Yerusalemu kuanzia Lango la Efraimu hadi kona ya Lango, umbali wa mikono mia nne.
And Joas king of Israel took Amasias king of Juda, the son of Joas, the son Joachaz, in Bethsames, and brought him to Jerusalem: and broke down the walls thereof from the gate of Ephraim, to the gate of the corner, four hundred cubits.
24 Akachukua dhahabu na fedha zote, vitu vyote vilivyoonekana akatika nyumba aya Mungu kwa Obedi Edomu, na vitu vya thamanai katika nyumba ya mfalme, na mateka pia, na akarudi Samaria.
And he took all the gold, and silver, and all the vessels, that he found in the house of God, and with Obededom, and in the treasures of the king’s house, moreover also the sons of the hostages, he brought back to Samaria.
25 Amazia mwana wa Yoashi, mfalme wa Yuda, aliishi miaka kumi na tano baada ya kifo cha Yehoashi, mwana wa Yehoahazi, mfalme wa Israeli.
And Amasias the son of Joas king of Juda lived, after the death of Joas the son of Joachaz king of Israel, fifteen years.
26 Kwa mambo mengingine kuhusu Amzia, mwanzo na mwisho, tazama, je, hayajaandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli?
Now the rest of the acts of Amasias, the first and last, are written in the book of the kings of Juda and Israel.
27 Sasa kutoka wakati amabaoa Amazia aligeukia mbali asimfuate Yahwe, walianza kupanga njama zidi yake katika Yerusalemu. Akakimbilia Lachishi, lakini wakatuma watu nyuma yake wamfuate Lachishsi na walimuua huko.
And after he revolted from the Lord, they made a conspiracy against him in Jerusalem. And he fled into Lachis, and they sent, and killed him there.
28 Wakamleta juu ya farasis na wakamzika pamoja na babu zake kataika Mji wa Yuda.
And they brought him back upon horses, and buried him with his fathers in the city of David.

< 2 Nyakati 25 >