< 2 Nyakati 21 >

1 Yehoshafati akalala pamoja na babu zake na akizikwa pamoaja nao katika mji wa Daudi; 2 Yehoramu, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake. Yehoramu alikuwa na ndugu, wana wa Yehoshafati: Azaria, Yerieli, Zekaria, Azaria, Mikaeli, na Shefatia. Wote hawa walikuwa wana wa Yehoshafati, mfalme wa Israeli. 3 Baba yao alikuwa amewapa zawadi kubwa ya fedha, dhahabu, na vitu vingine vya thamani, na miji yenye ngome katika Yuda, lakini kiti cha enzi alimpa Yehoramu, kwa sababu alikuwa mzaliwa wake wa kwanza. 4 Sasa Yehoramu alipokuwa ameinuka katika ufalme wa baba yake na kujiimarisha mwenyewe kama mfalme, akawaua ndugu zake wote kwa upanga, na pia viongizi wengine mbali mbali wa Israeli. 5 Yehoramu alikuwa na umri wa mika thelathini na mbili alipoanza kutawala, na akatawala kwa miaka minane katika Yerusalemu. 6 Akatembea katika njia za wafalme wa Israeli, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa ikifanya, kwa maana alikuwa na binti Ahabu kama mke wake, na akafanya yaliyo maovu katika macho ya Yahwe. 7 Vile vile, Yahwe hakutaka kuiangamiza nyumba ya Daudi, kwa sababu ya agano ambalo alikuwa amefanya na Daudi; alikuwa ameahidi kwamba siku zote angetoa uzima kwa ajili yake na kwa ajili ya vizazi vyake. 8 Katika siku za Yehoramu, Edomu wakaasi wasiwe chini ya Yuda, na wakajisimamishia mfalme juu yao. 9 Kisha Yeroboamu akavuka ng'ambo pamoja na maakida na magari yake yote. Ilikuwa usiku aliposimama na kupigana dhidi ya Waedomu ambao walikuwa wamemzunguka na maakida wa magari yake. 10 Kwa hiyo Edomu iliasi kutoka kuwa chini ya Yuda mpaka leo. Libna pia aliasi wakati ule ule wasiwe chini yake. Kwa sababu Yehoramu alikuwa amemsahau Yahwe, Mungu wa babu zake. 11 Zaidi ya hayo, Yehoramu pia alikuwa amezijenga sehemu zake za juu katika milma ya Yuda na akawafanya wakaaji wa Yuda kuishi kama makahaba, na akawaongoza Yuda katika upotevu. 12 Barua kutoka kwa nabii Eliya ikaja kwa Yerohamu. Ilisema, “Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Daudi, babu yako, anasema: Kwa sababu hujatembea katika njia za Yehoshafafati, baba yako, wala katika njia za Asa, mfalme wa Yuda, 13 bali umetembea katika njia za wafalme wa Israeli, na umewafanya Yuda na wakaaji wa Yerusalemu kuenenda kama kahaba, kama nyumba ya Ahabu walivyofanya—na kwa sababu pia umewaua ndugu zako katika familia ya baba yako kwa upanga, watu waliokuwa bora kuliko wewe mwenyewe— 14 ona, Yahwe atawapiga watu wako na pigo kubwa, watoto wako, wake zako, na mali zako zote. 15 Wewe mwenyewe utakuwa na ugonjwa mwingi kwa sababu ya ugonjwa kataika katika utumbo wako, mpaka utumbo wako uanguke nje kwa sababu ya ugonjwa, siku baada ya siku. 16 Yahwe akaichochea roho ya Wafilisiti dhidi ya Yuda na ya Waarabu waliokuwa karibu na Waethipia. 17 Wakaivamia Yuda, wakavamia katika nyumba ya mfalme. Pia wakawachukua wanaye na wake zake. Hakuna mwana aliyebakizwa kwa ajili yake ispokuwa, Yehoshafati, mwanaye mdogo. 18 Baada ya haya yote, Yahwe akampiga katika utumbo wake kwa ugonjwa usiopona. 19 Ikawa wakati ulipofika, katika mwisho wa miaka miwili, kwamba utumbo wake ukaaanguka nje kwa sababu ya ugonjwa wake, na kwamba akafa kwa ugonjwa mkali. Watu wake hawakutengeneza moto kwa ajili ya heshima yake kama walivyokuwa wamefanyia babu zake. 20 Alikuwa ameanza kutawala alipokuwa na umrai wa miaka thelatahini na mbaili; akatawala katika Israeli kwa miaka minane, na alikufa bila kuaombolezwa. Wakamzika katika mji wa Daudi, lakini siyo katika makaburi ya kifalme.

< 2 Nyakati 21 >