< 2 Nyakati 18 >

1 Sasa Yehoshafati alikauwa na utajiri mwingi na heshima kubwa; alifanya undugu na Ahabu mmoja wa watu wa familia yake akamuo binti yake. 2 Baada ya miaka kadhaa, akashsuka chini kwa Ahabu huko Samaria. Ahabu akachinja kondoo na ngo'mbe wengi kwa ajili ya yake na watu waliokuwa pamoja naye. Ahabu pia akamshawishi kuivamia Ramothi-gileadi pamoja naye. 3 Ahabu, mfalme wa Israeli, akamwambia Yehoshafati, mfalme wa Yuda, “Utakwenda Ramothi-gileadi pamoja nami?” Yehoshafati akamjibu, “Mimi ni kama wewe, na watu wangu ni kama watu wako; tutakuwa pamoja nawe katika vita.” 4 Yehoshafati akamwambia mfalme wa Israeli, Tafadhali litafute neno la Yahwe kwanza kwa ajili ya jibu lako” 5 Kisha mfale wa Israeli akawakusanya manabii pamoja, wanauame mia nne, na akasema akwao, Tutaenda vitani Ramothi-gileadi, au nisiende?” Wakasema, “Vamia, kwa maana Mungu ataitia mkononi mwa mfalme.” 6 Lakini Yehoshafati akasema, “Hakuna nabii mwingine hapa wa Yahwe ambaye kwake tunapaswa kutafuta ushauri?” 7 Mfale wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Bado kuna mtu mmoja amabaye kwake lazima tuutafute ushauri wa Yahwe, Mikaya mwana wa Imla, lakini namchukia kwa sababu yeye huwa hatabiri mema kamwe kuhusu mimi, bali kila mara maovu,” Lakini Yehoshafati akasema, “Mfalme hapaswi kusema hivyo.” 8 Kisha mfalme wa Israeli akamwita akida na kusema, Haraka mlete Mikaya mwana wa Imla.” 9 Sasa Ahabu mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda walikuwa wamekaa kila mmoja katika kiti cha enzi, wamevalia kanzu zao, katika sehemu ya uwazi katika maingilia ya lango la Samaria, na manabii wote walikuwa wakitabairi mbele zao. 10 Zedekia mwana wa Kenaani akajitengenezea pembe za chuma na kusema, Yahwe anasema hivi: Kwa kutumia hizi pembe mtawasukuma Waaramu hadi waangamie.” 11 Manabii wote wakatabiri kitu kile kile, wakisema, “Vamia Raamothi-gleadi na shinda. kwa maana Yahwe ameutia kwenye mkono wa mfalme.” 12 Mjumbe aliyeenda kumuita Mikaya akasema kwake, akisema, “Sasa angalia, maneno ya manabii yanatangaza mambo mema kwa ajili ya mfalme kwa kinywa kimoja. Tafadhali maneno yako yawe kama maneno ya mmoja wao na sema mambo mema.” 13 Mikaya akajibu, “Kama Yahwe aishivyo, mimi nitasema kile mbacho Mungu anasema.” 14 Alipokuja kwa mfalme, mfamle akamwambaia, “Mikaya, tutaenda Ramothi -gileadi kwa ajili ya vita, au la?” Mikaya akamjibu, “Vamia na utashinda! kwa maana utakuwa ushinda mkuu.” 15 Kisha mfalme akasema kwake, “Ni mara ngapi ninapaswa kukutaka kuapa kutoniambia kitu chochote sispokuwa kweli katika jina la Yahwe? 16 Kwa hiyo Mikaya akasema, “Niliwaoana Israeli wametawanyika ktika mlima, kama kondoo wasio na mchungaji, na Yahwe akasema, hawa hawana mchungaji. Ebu kila mtu arudi nyumbani kwake kwa amani.” 17 Kwa hiyo mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Sikukuambia kwamba asingeweza kutabiri mema juu yangu, bali majanga tu? 18 Kisha Mikaya akasema, “Kwa hiyo ninyi nyote mnapashwa kulisikia neno la Yahwe: Nilimuon Yahwe amekaa juu ya kiti chake cha enzi, na majeshi yote ya mbinguni yalikauwa yamekaa mkono wake wa kulia na mkono wake wa kushoto. 19 Yahwe akasema, Ni nani atakayemrubuni Ahabu, mfalme wa Israeli, ili kwamba aende na kuanguka huko Ramothi-gileadi?' Mmoja alisema hivi na mwingine hivi. 20 Kisha roho ikaja moja kwa maja na kusimama mbele ya Yahwe na kusema, 'Nitamrubuni.' Yahwe akamwambia, 'Kivipi?' 21 Roho ikajibu, “nitatoka nje na nitakuwa roho ya uongo katika vinywa vya manabii wake wote.' Yahwe akajibu, 'utamrubuni, na pia utafanikiwa. nenda sasa na fanya hivyo.' 22 Sasa ona, Yahwe ameweka roho ya uongo katika midomo ya manabii wako hawa, na Yahwe ametangaza majanga kwa ajili yako.” 23 Kisha Zedekia mwana wa Kenaana, akaja, akampiga kofi mika juu ya shavu, na kusema, “Kwa njia gani Roho wa Yahwe alitoka kwangu ili aseme nawe?” 24 Mika akasema, Angalia, utalijua hilo katika siku hiyo, mtakapokimbia katika baadhi ya vyumba vya ndani kwa ajili ya kujificha.” 25 Mfalme wa Israeli akasema kwa baadhi ya watumishi, “Enyi watu mkamateni Mikaya na mmpeleke hadi Amoni, mkuu wa mji na, na kwa Yoashi, mwanangu. 26 Nanyi mtamwambia, 'Mfalme anasema: Mweke gerezanai huyu mtu na umlishe kwa mkate kiogo tu na maji kidogo tu, mpaka nitakaporudi salama.” 27 Kisha Mikaya akasema, “Kama utarudi salama, Yahwe hajasema nami.”Kisha akaongeza, “Sikiliza haya, enyi watu wote.” 28 Kwa hiyo Ahabu, mfalme wa Israeli, na Yehoshafati, mfalme wa Yuda, wakaenda juu ya Ramothi-giledi. 29 Mfalme wa Israeli akamwamabia Yehoshafati, “Nitajibadilisha mwenyewe na kwenda vitani, lakini wewe vaa mavazi yako ya kifalme.” Kwa hiyo mfalame wa Israeli akajibalisha, na wakaenda vitani. 30 Sasa mfalme wa Aramu alikuwa amewaamuru maakida wa magari yake, akisema, Msiwavamie wanajeshsi wasio wa muhimu wala wanajeshsi muhimu. Badala yake, mvamieni mfalme wa Israeli pekee,” 31 Ikawa kwamba maakida wa magari walipomuona Yehoshafati wakasema, “Yule ni mfalme wa Israeli.” Wakageka kumzunguka wamvamie, lakini Yehoshafati akalia, na Yahwe akamsaidia. Mungu akawageza nyuma kutoka kwake. 32 Ikawa kwamba maakida wa magari walipoona ya kuwa hakuwa mfalme wa Israeli, wakarudi nyuma wasimfukuze. 33 Lakini mtu mmoja akauvuta upinde wake kwa kubahatisha na kumpiga mfalme wa Israeli kati kati ya maungio ya mavazi yake. Kisha Ahabu akamwambia dereva wa gari lake, “Geuza nyuma na nitoe nje ya mapigano, kwa maana nimejeruhiwa vibaya sana.” 34 Mapigano yakazidi kuwa makali siku hiyo, na mfalme wa israeli akashikiliwa katika gari lake kuwaelekea Waaramu hadi jioni. Muda jua lilipokaria kwenda chini, akafa.

< 2 Nyakati 18 >