< 1 Samweli 31 >

1 Basi Wafilisti wakapigana dhidi ya Waisraeli. Waisraeli wakakimbia mbele ya Wafilisti na wakaanguka chini wakafa katika mlima wa Gilboa.
さてペリシテびとはイスラエルと戦った。イスラエルの人々はペリシテびとの前から逃げ、多くの者は傷ついてギルボア山にたおれた。
2 Wafilisti wakamwandama Sauli na wanawe kwa karibu. Wakawaua wanawe Yonathani, Abinadabu, and Malkishua.
ペリシテびとはサウルとその子らに攻め寄り、そしてペリシテびとはサウルの子ヨナタン、アビナダブ、およびマルキシュアを殺した。
3 Vita vikamwelemea Sauli, na wapiga upinde wakampata. Akapata maumivu makali kwa sababu yao.
戦いは激しくサウルに迫り、弓を射る者どもがサウルを見つけて、彼を射たので、サウルは射る者たちにひどい傷を負わされた。
4 Kisha Sauli akamwambia mbeba silaha wake, “Chomoa upanga wako unichome nao. Vinginevyo, hawa wasiotahiriwa watakuja na kuninyanyasa.” Lakini mbeba silaha wake hakukubali, kwa kuwa aliogopa sana. Hivyo Sauli alichukua upanga wake mwenyewe na kuuangukia.
そこでサウルはその武器を執る者に言った、「つるぎを抜き、それをもってわたしを刺せ。さもないと、これらの無割礼の者どもがきて、わたしを刺し、わたしをなぶり殺しにするであろう」。しかしその武器を執る者は、ひじょうに恐れて、それに応じなかったので、サウルは、つるぎを執って、その上に伏した。
5 Yule mbeba silaha akaona kwamba Sauli amekufa, yeye naye vivyo hivyo akauangukia upanga wake akafa pamoja naye.
武器を執る者はサウルが死んだのを見て、自分もまたつるぎの上に伏して、彼と共に死んだ。
6 Kwa hiyo Sauli alikufa, wanawe watatu, na mbeba silaha wake - watu hawa wote walikufa pamoja siku iyo hiyo.
こうしてサウルとその三人の子たち、およびサウルの武器を執る者、ならびにその従者たちは皆、この日共に死んだ。
7 Watu wa Israeli waliokuwa upande mwingine wa bonde, na hao waliokuwa ng'ambo ya Yordani, walipoona kwamba Waisraeli wamekimbia, na kwamba Sauli na wanawe wamekufa, waliiacha miji yao na kukimbia, nao Wafilisti wakaja na kukaa humo.
イスラエルの人々で、谷の向こう側、およびヨルダンの向こう側にいる者が、イスラエルの人々の逃げるのを見、またサウルとその子たちの死んだのを見て町々を捨てて逃げたので、ペリシテびとはきてその中に住んだ。
8 IKawa katika siku iliyofuata, Wafilisti wakafika kuchukua nyara za waliokufa, ndipo wakamuona Sauli na wanawe watatu wameanguka juu ya mlima wa Gilboa.
あくる日、ペリシテびとは殺された者から、はぎ取るためにきたが、サウルとその三人の子たちがギルボア山にたおれているのを見つけた。
9 Nao wakakata kichwa chake na kuondoa silaha zake, na wakawatuma wajumbe kwenda pande zote katika nchi ya Wafilisti kutangaza habari hizo katika mahekalu yao ya sanamu na kwa watu.
彼らはサウルの首を切り、そのよろいをはぎ取り、ペリシテびとの全地に人をつかわして、この良い知らせを、その偶像と民とに伝えさせた。
10 Wakaziweka silaha zake katika hekalu la Ashtorethi, nao wakakitundika kiwiliwili chake kwenye ukuta wa mji wa Bethi Shani.
また彼らは、そのよろいをアシタロテの神殿に置き、彼のからだをベテシャンの城壁にくぎづけにした。
11 Na wenyeji wa Yabeshi Gileadi waliposikia kile Wafilisti walichomfanyia Sauli,
ヤベシ・ギレアデの住民たちは、ペリシテびとがサウルにした事を聞いて、
12 wapiganaji wote wakainuka na kwenda usiku wote na wakauondoa mwili wa Sauli na miili ya wanawe kutoka ukuta wa Bethi Shani. Nao wakaenda Yabeshi na wakaichoma moto hiyo miili huko.
勇士たちはみな立ち、夜もすがら行って、サウルのからだと、その子たちのからだをベテシャンの城壁から取りおろし、ヤベシにきて、これをそこで焼き、
13 Kisha wakachukua mifupa yao na kuizika chini ya mti wa mkwaju huko Yabeshi, na wakafunga siku saba.
その骨を取って、ヤベシのぎょりゅうの木の下に葬り、七日の間、断食した。

< 1 Samweli 31 >