< 1 Wafalme 9 >

1 Sulemani alipomaliza kulijenga hekalu la BWANA, na ikulu ya mfalme, na baada ya kukamilisha vyote alivyokusudia kufanya, 2 BWANA alionekana kwa Sulemani kwa mara ya pili, kama alivyoonekana kwake kule Gibeoni. 3 Na BWANA akamwambia, “Nimeyasikia maombi yako na dua zako ambazo umeniomba. Nimeitakasa nyumba hii ambayo umeijenga, kwa ajili yangu, ili niweke jina langu humo milele. Macho yangu na moyo wangu yatakuwa humo kwa nyakati zote. 4 Lakini pia na wewe, kama utatembea mbele zangu kama Daudi baba yako alivyotembea kwa haki na unyofu katika moyo wako, ukitii yote niliyokuamuru na kuyashika maagizo na sheria zangu, 5 ndipo nitakapoimarisha kiti cha enzi kwa Israeli milele, kama nilivyomwahidi baba yako Daudi, nikiseama, 'uzao wako hautaondoka katika kiti cha enzi cha Israeli. 6 Lakini kama utageuka, wewe au watoto wako, na kutozishika amri zangu na maagizo yangu ambayo nimeyaweka mbele zako, na kama utaenda kuabudu miungu mingine na kuisujidia, 7 basi nitaikatilia mbali Israeli kutoka katika ardhi niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli itakuwa mfano wa kukejeliwa na kitu cha kutusiwa katika mataifa yote. 8 Ijapokuwa hekalu hili limetukuka sasa, kila mtu atakayepita pembeni yake atasituka na kuzoomea. Watajiuliza, 'Kwa nini BWANA amefanya hili katika chi hii na kwa nyumba hii?' 9 Na wengine watajibu, 'Ni kwa sababu walimwacha BWANA, Mungu wao, ambaye aliwaleta mababu zao toka Misri, na sasa wamegeukia miungu mingine ambayo wameiinamia na kuisujudu. Hiyo ndiyo sababu BWANA amewaletea majanga haya yote.” 10 Ilitokea mwishoni mwa miaka ishirini, Sulemani alikuwa amemaliza kuyajenga majengo yote mawili, hekalu la BWANA na ikulu ya mfalme. 11 Basi Hiramu, mfalme wa Tiro, alikuwa amemletea Sulemani mbao za mierezi na miboreshi, pamoa na dhahabu; vitu vyote ambavyo Sulemani alitamani. Kwa hiyo mfalme Sulemani akampatia Hiramu miji ishirini huko Galilaya. 12 Hiramu akaja kutoka Tiro kuiona ile miji ambayo Sulemani alikuwa amempatia, lakini hakupendezwa nayo. 13 Kwa hiyo Hiramu akasema, “Ndugu yangu, ni miji gani hii uliynipatia? Hiramu akaiita nchi ya Kabuli mpaka leo. 14 Hiramu alikuwa amemtumia mfalme tani nne za dhahabu. 15 Vifuatavyo ndivyo vigezo ambavyo mfalme Sulemani aliweka: ili kulijenga hekalu la BWANA na ikulu yake, kuijenga Milo na ukuta wa Yerusalemu, na Hazori, Megido, na Gezari. 16 Farao mfalme wa Misri alikuwa ameenda kuitwaa Gezeri, akaichoma moto, na kuwaua Wakanaani katika mji. Kisha Farao akampatia binti yake ule mji, mke wa Sulemani kuwa zawadi ya arusi. 17 Kwa hiyo Sulemani akaijenga Gezeri na Bethi Horoni ya Loweri, 18 Baalathi na Tamari jangwani katika nchi ya Yuda, 19 na miji yote ya hazina yote iliyokuwa yake, na miji ya magari yake, na miji ya wapanda farasi wake, na hata kama alipenda kuijenga kwa ajili ya fahari yake kule Yerusalemu, Lebanoni, na katika nchi yote kwenye utawala wake. 20 Na kwa watu wote waliokuwa wamesalia wa Waamori, Wahiti, Waperezi, Wahivi, na Yebu, ambao hawakuwa Waisraeli, 21 na uzao wao waliokuwa wamesalia baada yao katika nchi, ambao Waisraeli hawakuweza kuwaangamiza kabisa - Sulemani akawafanya kuwa vibarua, ambao wako hata leo. 22 Hata hivyo, Sulemani hakuwafanya kuwa shokoa watu wa Israeli. Badala yake, walifanyika kuwa wanajeshi wake na watumishi wake, maakida wake, na wakuu wake, na majemedari wake na wapanda farasi wake. 23 Hawa ndio waliokuwa maakida wakuu waliokuwa wakiwasimamia kazi za Sulemani, watu 550, walikuwa wasimamizi wa watu waliokuwa wakifanya kazi. 24 Binti wa Farao alihama kutoka mji wa Daudi kwenda kwenye ile nyumba ambayo Sulemani alimjengea. Baadaye, Sulemani akaijenga Milo. 25 Mara tatu kwa kila mwaka Sulemani alitoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani katika madhabahu ambayo alimjengea BWANA, akifukiza uvumba pamoja nazo juu ya madhabahu ilyokuwa mbele ya BWANA. Kwa hiyo akalimalizia hekalu na sasa alikuwa akilitumia. 26 Tena Sulemani alitengeneza merikebu kule Ezioni Geberi, ambayo iko karibu na Elathi katika ufukwe wa bahari ya shamu, katika nchi ya Edomu. 27 Hiramu alituma watumishi kwenye merikebu ya Sulemani, wanamaji wanaoijua bahari, pamoja na watumishi wake Sulemani. 28 Walikwenda kwa Ofri pamoja na watumishi wa Sulemani. Kutoka huko walileta takribani tani 14. 5 za dhahabu kwa Sulemani.

< 1 Wafalme 9 >