< 1 Wafalme 3 >

1 Sulemani akawa na ushirikiano wa kindoa na Farao mfalme wa Misri. Alimwoa binti wa Farao na kumleta katika mji wa Daudi mpaka alipomaliza kujenga nyumba yake, nyumba ya BWANA, na ukuta wa Yerusalemu. 2 Watu walikuw wakitoa sadaka kwenye maeneo ya juu, kwa sababu hapakuwa bado na nyumba iliyokuwa imejengwa kwa jina la BWANA. 3 Sulemani alionyesha upendo wake kwa BWANA kwa kutembea katika maagizo ya Daudi baba yake, isipokuwa tu alitoa dhabihu na kuchoma uvumba mahali pa juu. 4 Mfalme akaenda Gibioni kutoa sadaka kule, kwa kuwa hilo ndilo lilikuwa eneo kuu la juu. Sulemani katoa sadaka maelfu katika madhabu hiyo. 5 BWANA akaonekana kwa Sulemani huko Gibioni katika ndoto ya usiku; akasema, “Omba! uanataka nikupe nini?” 6 Kwa hiyo Sulemani akasema, “umeonyesha uaminifu wa agano mkuu kwa mtumishi wako, Daudi baba yangu, kwa sababu alitembea mbele yako kwa ukweli na uaminifu, katika haki ya moyo na katika unyofu wa moyo. Umetunza kwa ajili yake hili agano kuu kwa uaminifu na umempa mwana wake kuketi kwenye kiti chake cha enzi leo. 7 Na sasa, BWANA, Mungu wangu, umemfanya mtumishi wako kuwa mfalme katika nafasi ya Daudi baba yangu, japo mimi ni mtoto mdogo. Sijui namna ya kuiingia na kutoka. 8 Mtumishi wako yuko katikati ya watu wako uliowachagua, kundi kubwa, watu wangi wasiohesabika. 9 Kwa hiyo umpe mtumishi wako moyo wa uelewa wa kuwahukumu watu wako. Kwani ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi?” 10 Ombi hili la Sulemani likampendeza Bwana. 11 Kwa hiyo Mungu akamwambia. “Kwa sababu umeomba jambo hili na haujajiombea maisha marefu au utajiri au uhai wa maadui wako, lakini umeomba ufahamu wa kutambua hukumu ya haki, 12 Tazama sasa nitafanya yote uliyoniomba wakati uliponipa ombi lako. Ninakupa moyo wa hekima na ufahamu, kwa kuwa hapajawahi kuwa na mtu wa kuwa kama wewe kabla yako, na hakuna wa kuwa kama wewe atakayeinuka baada yako. 13 Pia ninakupa hata ambayo hujaomba, vyote heshima na utajiri, ili kwamba pasije pakawa na mfalme wa kuwa kama wewe katika siku zako zote. 14 Kama utatembea katika njia zangu na kuyatunza maagizo yangu na maagizo yangu, kama alivyofanya baba yako Daudi, ndipo nitakapoziongeza siku zako.” 15 Kisha Sulemani alipoamka, na tazama, ilikuwa ndoto. Akaja Yerusalemu na akasimama mbele ya sanduku na agano la Bwana. Akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, na akawafanyia sherehe watumishi wake wote. 16 Kisha wanawake wawili waliokuwa makahaba wakaja mbele ya mfalme wakasimama mbele yake. 17 Mwanamke mmoja akasema, “Aa, bwana wangu, mwanamke huyu na mimi tunaishi katika nyumba moja, Nilizaa mtoto tukiwa pamoj na yeye katika nyumba yetu. 18 Ikatokea siku ya tatu baada ya kujifungua na yeye akajifungua. Tulikuwa sisi tu. Hapakuwepo na mtu mwingine yeyote katika nyumba yetu, ila sisi tu wawili katika hiyo nyumba. 19 Kisha mtoto wa mwanamke huyu akafa wakati wa usiku, kwa sababu alimlalia. 20 kwa hiyo akamka wakati huo wa usiku wa manane akamchukua mwanangu toka pembeni yangu, wakati mimi mtumishi wako nilipokuwa usingizini, na akamlaza kwenye kifua chake, na akamlaza mtoto wake aliyekufa juu ya kifua changu. 21 Asubuhi nilipoamka ili kumhudumia mwanangu, nikaona kuwa alikuwa amekufa. Lakini nilipomwangalia kwa makini wakati huo wa asubuhi, nikagundua kuwa hakuwa yule mwanangu niliyezaa,” 22 Yule mwanamke mwingine akasema, “Hapana, Huyu aliye hai ndiye wangu. Na yule aliyekufa ndiye wako.” Yule mwanamke wa kwanza akasema, “Hapana, Yule mtoto aliyekufa ndiye mwanao, na huyu aliye hai ndiye wangu.” Hivi ndivyo walivyoongea mbele ya mfalme. 23 Kisha mfalme akasema, “Mmoja wenu anasema, 'huyu aliye hai ni wangu, na kumbe mwanao ndiye aliye kufa,'na mwingine naye anasema, 'Hapana, mwanao ni yule aliyekufa, na mwanangu ni huyu aliye hai.'” 24 Mfalme akasema, ''Nileteeni upanga.” Kwa hiyo wakaleta upanga kwa mfalme. 25 Kisha mfalme akasema, “Mgawe mtoto aliye hai katika vipande viwili, na huyu mwanamke apewe nusu na yule mwingine naye apewe nusu.” 26 Yule mwanamke mwenye mtoto aliyekuwa hai akamwambia mfalme, kwa kuwa moyo wake ulikuwa na huruma sana kwa mwanae, akasema, “Aa, bwana wangu, mpatie huyu mtoto aliye hai, na usimwue kamwe.” Lakini yule mwanamke mwingine akasema, “Hatakuwa wangu wala wako. Mgawe.” 27 Ndipo mfalme aliposema, “Mpe yule mwanamke wa kwanza mtoto aliye hai, na kamwe usimwue. Yeye ndiye mama wa mtoto huyu.” 28 Israeli wote waliposikia hukumu ambayo mafalme ametoa, walimwogopa mfalme, kwa sababu waliona kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake kwa ajili ya kutoa kuhukumu.

< 1 Wafalme 3 >