< 1 Nyakati 8 >

1 Wana watano wa Benjamini walikuwa Bela mwana wake wa kwanza, Asibeli, Ahara, 2 Noha, na Rafa. 3 Wana wa Bela walikuwa Adari, Gera, Abihudi, 4 Abishau, Naamani, Ahoa, 5 Gera, Shefufani, na Huramu. 6 Hawa walikuwa uzao wa Ehudi ambao walikuwa vichwa vya koo kwa wakazi wa Geba, ambao walihimizwa kuhamia Manahati: 7 Naamani, Ahijahi, na Gera. Wa mwishi, Gera, aliwaongoza katika kuhama. Alikuwa baba wa Uza na Ahihudi. 8 Shaharaimu akawa baba wa watoto katika ardhi ya Moabu, baada ya kuwatariki wake zake Hushimu na Baara. 9 kwa mke wake Hodeshi, Shaharaimu akawa baba wa Yobabu, Zibia, Mesha, Malkamu, 10 Yeuzi, Shachia, na Mirima. Hawa walikuwa wana wake, viongozi katika koo zao. 11 Alikwisha kuwa baba wa Abitubi, na Elipaali kwa Hushimu. 12 Wana wa Elipaali walikuwa Eba, Mishamu, na Shemedi ( ambao walijenga Ono na Lod pamoja na vijiji vilivyozunguka.) 13 Pia walikuwako Beria na Shema. Walikuwa vichwa vya koo walizoishi Aijalon, Ambao waliwaondoa wakazi wa Gati. 14 Beria alikuwa na wana watatu: Ahio, Shashaki, Jeremothi, 15 Zebadia, Aradi, Eda, 16 Mikaeli, Ishipa, na Joha. 17 Elipaa alikuwa na wana hawa: Zebadia, Meshulamu, Hiziki, Heba, 18 Ishimerai, Izilia, na Yobabu. 19 Shimei alikuwa na wana hawa: Yokimu, Zikri, Zabdi, 20 Elienai, Zilletai, Elieli, 21 Adaia, Beraia, na Shimrati. 22 Shashaki alikuwa na wana hawa: Ishipani, Eba, Elieli, 23 Abdoni, Zikri, Hanani, 24 Hanania, Elamu, Antotoja, 25 Ifdeia, na Penueli. 26 Yerohamu alikuwa na wana hawa: Shamsherai, Sheharia, Atli, 27 Yaareshia, Elija, na Zikri. 28 Hawa walikuwa vichwa vya koo na viongozi walioishi Yerusalemu. 29 Baba wa Gibeoni, Jeieli, ambaye mke wake aliitwa Maaka, aliishi ndani ya Gibeoni. 30 Uzao wake wa kwanza alikuwa Abdoni, akafatia Zuri, Kishi, Baali, Nadab, 31 Gedori, Ahio, na Zekari. 32 Mwana mwingine wa Yeieli alikuwa Mikloti, ambaye akaja kuwa baba wa Shimea. Pia wanaishi karibu na ndugu zao Yerusalemu. 33 Neri alikuwa baba wa Kishi. Kishi alikuwa baba wa Sauli. Sauli alikuwa baba wa Yonathani, Malkishua, Abinadabu, na Ishbaali. 34 Mwana wa Yonathani alikuwa Meribu Baali. Meribu Baali alikuwa baba wa Mika. 35 Wana wa Mika walikuwa Pithoni, Meleki, Tarea, and Ahazi. 36 Ahazi akawa baba wa Yehoada. Yehoada alikuwa baba wa Amelethi, Azimavethi, na Zimri. Zimri alikuwa baba wa Moza. 37 Moza alikuwa baba wa Binea. Binea alikuwa baba wa Rafa. Rafa alikuwa baba wa Eleasa. Eleasa alikuwa baba wa Azeli. 38 Azeli alikuwa na wana sita: Azrikamu, Bokeru, Ishimaeli, Obadia, na Hanani. Wote hawa walikuwa wana wa Azeli. 39 Wana wa Esheki, kaka yake, walikuwa Ulamu mzaliwa wake wa kwanza, Yeushi wa pili, na Elifeleti wa tatu. 40 Wana wa Ulamu walikuwa wanaume wa mapambano na warusha mishale wa zuri. Walikuwa na wana wengi na wajukuu, jumla ya 150. Wote hawa walikuwa uzao wa Benjamini.

< 1 Nyakati 8 >