< 1 Nyakati 7 >

1 Isiakari alikuwa na wana wanne Tola, Pua, Yashubi, na Shimironi. 2 Wana wa Tola walikuwa Uzi, Refaia, Yerie, Yamai, Ibisami, Shemueli. Walikua vichwa katika nyumba za baba yao, toka uzao wa Tola na waliorodheshwa kama mashujaa hodari miongoni mwa kizazi chao. Katika siku za Daudi walikua na idadi ya 22, 600. 3 Mwana wa Uzi alikua Izrahia. Mwana wake alikua Michaeli, Obadia, Yoeli, na Ishia, wote watano walikua viongozi wa ukoo 4 Pamoja nao walikua na jeshi la watu elfu thelathini na sita kwa mapambano, Kwa mujibu wa orodha zilizomilikiwa na koo za mababu zao, kwa kuwa walikuwa na wake wengi pamoja na wana. 5 Kaka zao, kabila la Isakari, walikua na wanaume wa vita themanini na saba, kwa mujibu wa orodha zilizomilikiwa na koo za mababu zao. 6 Wana watatu wa Benjamini walikuwa Bela, Beka, na Yediaeli. 7 Wana watano wa Bela walikuwa Ezibono, Uzi, Uzieli, Yerimoti, na Iri. Walikua ni wanajeshi na waanzilishi wa koo. Watu wao walikuwa na idadi ya wanaume wa vita 22, 034, kwa mujibu wa orodha zilizomilikiwa na koo za mababu zao. 8 Wana wa Beka walikuwa Zemira, Yoashi, Elieza, Elionai, Omri, Yeremoti, Abiya, Anatoti, na Alemeti. Wote hawa walikuwa wana wake. 9 Orodha ya koo zao ilikua na idadi ya 20, 200 viongozi wa familia na wanaume wa vita. 10 Mwana wa Yediaeli alikuwa Bilhani. Wana wa Bilhani walikuwa Yeushi, Benjamini, Ehudi, Kenaana, Zetani, Tarishishi, na Ahishahari. 11 Wote hawa waikuwa wana wa Yediaeli. Waliorodheshwa katika ukoo orodha ilikuwa 17, 200 viongozi na wanaume wa vita imara kwa kazi ya jeshi. 12 (Shupimu na Hupimu walikuwa wana wa Iri, na Hushimu alikuwa mwana wa Aheri.) 13 Wana wa Naftali walikuwa Yazieli, Guni, Yezeri, na Shalumu. Hawa walikuwa wajukuu wa Bilhahi. 14 Manasse alikua na mtoto wa kiume aliitwa Asrieli, Ambaye suria wake wa Kiaramia alimzalia. Pia alimzaa na Makiri, baba wa Gileadi. 15 Makiri alimchukua mke wake kutoka Hupite na Shupite. Jina la dada yake lilikuwa Maaka. Mwingine wa uzao wa Manasse alikuwa Zalofehadi, ambaye alikuwa na mabinti pekee. 16 Maaka mke wa Makiri, alimzaa mwana na alimuita Pereshi. Kaka yake aliitwa Shereshi, na wana wake walikuwa Ulamu na Rakemu. 17 Mwana wa Ulami alikuwa Bedani. Hawa walikuwa uzao wa Gileadi mwana wa Makiri mwana wa Manase. 18 Dada wa Gileadi Hamoleketi alimzaa Ishihodi, Abi Ezeri, na Mahila. 19 Wana wa Shemida walikuwa Ahiana, Shekemu, Liki, na Aniamu. 20 Uzao wa Efraimu ulikuwa kama ifuatavyo: Efraimu mwana wa Shutela. Shutela mwana wa Beredi. Beredi mwana wa Tahati. 21 Tahati mwana wa Eleada. Eleada mwana wa Shutela. (Eza na Eleadi waliuawa na wanaume wa Gati, wenyeji wa nchi, walipoenda kuiba mifugo yao. 22 Efraimu baba yao aliomboleza kwa siku nyingi, na kaka zake walikuja kumfariji. 23 Alilala na mkewe. Akapata mimba akamzaa mwana. Efraimu akamuita Beria, kwa sababu maafa yalishakuja nyumbani mwake. 24 Binti yake alikuwa Sheera, ambaye alijenga miji juu na chini Beth Horon na Uzzen Sheerah.) 25 Mwana wake alikuwa Rafa. Mwana wa Rafa alikuwa Reshefi. Mwana wa Reshafi alikuwa Tela. Mwana wa Tela alikuwa Tahani. 26 Mwana wa Tahani alikuwa Ladani. Mwana wa Ladani alikuwa Amihudi. Mwana wa Amihudi alikuwa Elishama. 27 Mwana wa Elishama alikuwa Nuni. Mwana wa Nuni alikuwa Joshua. 28 Mali zao na makazi yao yalikuwa Betheli na yalizungukwa na vijiji. Waliongeza upande wa mashariki hadi Naarani na upande wa magharibi hadi Gezeri na vijiji vyake, na Shekemu na vijiji vyake hadi Aya na vijiji vyake. 29 Katika mipaka pamoja na Manasse kulikuwa na Beti shani na vijiji vyake, Taanaki na vijiji vyake, Megido na vijiji vyake, na Dori na vijiji vyake. Katika huu mji waliishi uzao wa Josefu mwana wa Israeli. 30 Wana wa Asha walikuwa Imna, Ishiva, Ishivi, na Beria. Sera alikuwa dada yao. 31 Wana wa Beria walikuwa Heberi na Malchieli, Ambaye alikuwa baba wa Birzaiti. 32 Wana wa Heberi walikuwa Yafeti, Shomer, na Hotamu. dada yao alikuwa Shua. 33 Wana wa Yafeti walikuwa Pasach, Bimhali, na Ashivati. hawa walikuwa watoto wa yafeti. 34 shoma, kaka wa Yafeti alikuwa na wana hawa: Roga, Yehuba, Aram. 35 Kaka yake Shema, Helemu, alikuwa na wana hawa: Zofa, Imna, Sheleshi na Amali. 36 Wana wa Zofa walikuwa Sua, Harinefa, Shua, Beri, IMra, 37 Beza, Hodi, Shamma, Shilsha, Ithrani, na Beera. 38 Wana wa Yeta walikuwa Jefune, Pispa, na Ara. 39 Wana wa Ulla walikwa Ara, Hannieli, na Rizia. 40 Hawa wote walikuwa uzao wa Asha. Walikua mababu wa ukoo, viongozi wa familia, wananume wa kipekee, wanaume wa vita, na machifu kati ya viongozi. Kulikuwa na wanaume elfu ishirini na sita walioorodheshwa waliokuwa imara kwa kazi ya jeshi, kwa mujibu wa idadi iliyo orodheshwa.

< 1 Nyakati 7 >