< 1 Nyakati 4 >

1 Uzao wa Yuda ulikuwa Peresi, Hesroni, Karmi, Huri, na Shobali. 2 Shobali alikuwa baba wa Reaya. Reaya alikuwa baba wa Yahathi. Yahathi alikuwa baba wa Ahumai na Lahadi. Hawa walikuwa mababu wa koo za Wasorathi. 3 Hawa walikuwa mababu wa ukoo katika mji wa Etamu: Yezreeli, Ishma, na Idbashi. Babu yao alikuwa Haselelponi. 4 Penueli alikuwa babu wa koo katika mji wa Gedori. Ezeri alikuwa muanzilishi wa koo katika Husha. Hawa walikuwa uzao wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi na muanzilishi wa Bethelehemu. 5 Ashuri baba wa Tekoa alikuwa na wake wawili, Hela na Naara. 6 Naara alimzalia Ahuzamu, Heferi, Temeni na Ahashtari. Hawa walikua wana wa Naara. 7 Wana wa Hela walikua Serethi, Ishari, Ethnani, 8 na Kozi, alikua baba wa Anubu na Sobeba, na koo zilizotoka kwa Aharheli mwana wa Harumu. 9 Yabesi aliheshimika zaidi ya kaka zake. Mama yake alimuita Yabesi. Alisema, “Kwasababu nimemzaa katika huzuni.” 10 Yabesi akamuita Mungu wa Israeli na kusema, “Kama tu utanibariki mimi, ongeza mipaka yangu, na mkono wako ukuwa juu yangu. Ukifanya hivi utaninusuru na mabaya, ili kwamba niwe huru na huzuni!” Kwa hivyo Mungu akamjalia maombi yake. 11 Kelubu kaka wa Shuha akawa baba wa Mehiri, aliyekuwa baba wa Eshtoni. 12 Eshtoni akawa baba wa Beth-Rafa, Pasea, na Tehina, ambaye alianzisha mji wa Nahashi. Hawa ni wanaume walioishi Reka. 13 Wana wa Kenazi walikua Othinieli na Seraia. Wana wa Othinieli walikuwa Hathathi na Meonothai. 14 Meonothai akawa baba wa Ofara, na Seraia akawa baba wa Yohabu, mwanzilishi wa Ge Harashimu, ambao watu wake walikua wahunzi. 15 Wana wa Kalebu mwana wa Yefune walikua Iru, Ele na Namu. Wana wa Ela alikua Kenazi. 16 Wana wa Yehaleli walikua Zifi, Zifa, Tiriya, na Azareli. 17 Wana wa Ezra walikua Yetheri, Meredi, Eferi, na Yaloni. 18 Mke wake Meredi wa Kimisri alimzalia Miriamu, Shamai, na Ishibahi, aliyekua baba wa Eshitemoa. Hawa walikua wana wa Bithia, binti wa Farao, ambaye Meredi alimuoa. Mke wa Kiyahudi wa Meredi alimzalia Yeredi, ambaye alikua baba wa Gedore; Heberi, aliyekua baba wa Soko; na Yekuthieli aliyekua baba wa Zanoa. 19 Kati ya watoto wawili wa mke wa Hodia, dada wa Nahamu, mmoja wao kawa baba wa Keila Mgarimite. Mwingine alikua Eshitemoa Mmakathite. 20 Wana wa Shimoni walikua Amnoni, Rina, Beni Hanani, na Tilon. Wana wa Ishi walikua Zohethi na Beni Zoheti. 21 Uzao wa Shela mwana wa Yuda, Ulikua ni Eri baba wa Leka, Laada baba wa Maresha na koo za wafanyakazi wa kushona kule Beth Ashbea, 22 Yoakimu, Wanaume wa Kozeba, na Yoashi na Sarafi, waliokua na mali huko Moabu, lakini walirudi Bethlehemu. ( Maelezo haya yametoka kwenye nakala za zamani.) 23 Baadhi ya watu hawa walikuwa ni wafinyanzi walioishi Netaimu na Gedera na wakawa wafanyakazi wa Mfalme. 24 Uzao wa Simeoni ulikua Jamini, Jaribu, Zera, na Shauli. 25 Shalumu alikua mwana wa Shauli, Mibisamu mwana wa Shalumu, na Mishima mwana wa Mibisamu. 26 Ukoo wa Mishima ulikua Hamueli mwana wake, Zakuri mjukuu wake, na Shimei kitukuu chake. 27 Shimei alikua na wana kumi na sita na mabinti sita. Kaka yake hakua na watoto wengi, Hivyo koo zao hazikuongezeka kwa idadi kubwa kama wato wa Yuda walivyoongezeka. 28 Waliishi Beasheba, Molada, na Hazari Shuali. 29 Pia waliishi Bilha, Ezemu, Toladi, 30 Bethueli, Horma, Zikilagi, 31 Bethi Markabothi, Hazari Susimi, Bethi Biri, na Shaaraimu. Hii ilikua miji yao mpaka utawala wa Daudi. 32 Vijiji vyao vitano vilikua Etamu, Aini, Tocheni, na Ashani, 33 pamoja na mipaka ya vijiji kwa umbali wa Baali. Haya yalikua makazi yao, na walitunza kumbukumbu za uzao wao. 34 Viongozi wa ukoo walikua Meshobabu, Yamileki, Yoshahi mwana wa Amazia, 35 Yoeli, Yehu mwana wa Yoshibia mwana wa Seraia mwana wa Asieli, 36 Elioenai, Yaakoba, Yeshohaia, Asaia, Adieli, Yesimieli, Benaia, 37 na Ziza mwana wa Shifi mwana wa Aloni mwana wa Yedaia mwana wa Shimiri mwana wa Shemaia. 38 Hawa walio orodheshwa kwa majina walikua viongozi wa koo zao, na koo zao ziliongezeka sana. 39 Walienda karibu na Gedori, mashariki mwa bonde, kutafuta malisho ya mifugo yao. 40 Walipata malisho mengi na mazuri. Nchi ilikua tambarare, tulivu na ya amani. Wahamu waliishi hapo awali. 41 Hao walio orodheshwa hapo kwa majina walikuja katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda, na wakashambulia makazi ya Wahamu na Wameuni, ambao pia walikua hapo. Waliwaangamiza kabisa na kuishi hapo sababu walipata malisho kwa ajili ya mifugo yao. 42 Wanaume mia tano wa kabila la Simeoni walienda katika mlima Seiri, na viongozi wao Pelatia, Nearia, Refaia, na Uzieli, wana wa Ishi. 43 Waliwashinda wakimbizi wa Waamaleki waliobakia, na wakaishi hapo hadi siku hii.

< 1 Nyakati 4 >