< 1 Nyakati 24 >

1 Makundi vya kazi kulingana na uzao wa Aroni yalikuwa haya: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari. 2 Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao kufa. Walikuwa hawana watoto, kwahiyo Eleazari na Ithamari walitumika kama makuhani. 3 Daudi pamoja na Zadoki, uzao wa Eleazari, na Ahimeleki, uzao wa Ithamari, waliwagawanya katika makundi yao ya kazi kama makuhani. 4 Kulikuwa na wanaume viongozi zaidi kati ya uzao wa Eleazari kuliko kati ya uzao wa Ithamari, kwahiyo waligawanya uzao wa Eleazari katika makundi kumi na sita. Walifanya hivyo na viongozi wa ukoo na uzao wa Ithamari. Magawanyo haya yalikuwa nane kwa idadi, sambamba na koo zao. 5 Waliwagawanya bila upendeleo kwa kura, kwa kuwa walikuwa waamuzi watakatifu na waamuzi wa Mungu, kutoka pande zote uzao wa Eleazari na uzao wa Ithamari. 6 Shemaia mwana wa Nethaneli mwandishi, Mlawi, aliandika majina yao mbele ya mfalme, muamuzi, kuhani Zadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa makuhani na familia za Walawi. Ukoo mmoja ulichaguliwa kwa kura kutoka uzao wa Eleazari, na kisha uliofata utachaguliwa kutoka uzao wa Ithhamari. 7 Kura ya kwanza ilienda kwa Yehoiaribu, ya pili kwa Yedaia, 8 ya tatu kwa Harimu, ya nne kwa Seorimu, 9 ya tano kwa Malikija, ya sita kwa Mijamini, 10 ya saba kwa Hakozi, ya nane kwa Abija, 11 ya tisa kwa Yeshua, ya kumi kwa Shekania, 12 ya kumi na moja kwa Eliashibu, ya kumi na mbili kwa Yakimu, 13 ya kumi na tatu kwa Hupa, ya kumi na nne kwa Yesheheabu, 14 ya kumi na tano kwa Biliga, ya kumi na sita kwa Imma, 15 ya kumi na saba kwa Heziri, ya kumi na nane kwa Hapizezi, 16 ya kumi na tisa kwa Pethaia, ya ishirini kwa Yehezikeli, 17 ya ishirini na moja kwa Yakini, ya ishirini na mbili kwa Gamuli, 18 ya ishirini na tatu kwa Delaia, na ya ishirini na nne kwa Maazia. 19 Hii ilikuwa taratibu ya utumishi wao, walipo kuja kwenye nyumba ya Yahweh, wakifuata utaratibu waliopewa na Aruni babu yao, kama Yahweh, Mungu wa Israeli, alivyo waagiza. 20 Hawa walikuwa Walawi waliobakia: Wana wa Amiramu, Shebueli; wana wa Shebaeli, Yedeia. 21 Wana wa Rehabia: wana wa Rehabia, Ishia kiongozi. 22 Wa Waizari, Shelomothi; mwana wa Shelomothi, Yahathi. 23 Wana wa Hebroni: Yeria kiongozi, Amaria wapili, Yahazieli watatu, na Yekameamu wanne. 24 Wana wa uzao wa Uzieli ulimjumuisha Mika. Uzao wa Mika ulimjumuisha Shamiri. 25 Kaka wa Mika alikuwa Ishia. Wana wa Ishia akijumuishwa Zakaria. 26 Wana na Merari: Mahli na Mushi. Mwana wa Yaazia, Beno. 27 Wana wa Merari: Yaazia, Beno, Shohamu, Zakuri, na Ibrri. 28 Wana wa Mahili: eleazari, ambaye alikuwa hana wana. 29 Wana wa Kishi: Yerameli 30 wana wa Mushi: Mahli, Eda, na yerimothi. Walikuwa walawi, walio orodheshwa na familia zao. 31 Wanaume hawa ambao walikuwa vichwa katika nyumba za baba zao na kila wadogo zao, walipiga kura katika uwepo wa Mfalme Daudi, na Zadoki na Ahimeleki, pamoja na viongozi wa familia wa makuhani na Walawi. Walirusha kura kama uzao wa Aroni walivyofanya.

< 1 Nyakati 24 >