< 1 Nyakati 22 >

1 Kisha Daudi akasema, “Hapo ndipo nyumba ya Yahweh Mungu itakuwepo, na madhabahu ya sadaka za kuteketezwa za Israeli.” 2 Hivyo Daudi akaagiza watumishi wake wawakusanye pamoja wageni wote wanao ishi katika nchi ya Israeli. Aliwapangia kuwa wachonga mawe, kuchonga matofali ya mawe, ilikuweza kujenga nyumba ya Mungu. 3 Daudi alisambaza idadi kubwa ya chuma kwa ajili ya misumari na vitasa vya kuweka kwenye malango. Pia alitoa shaba zaidi kushinda kipimo, 4 na miti ya mierezi zaidi ya kipimo. (Wasidoni na Watiria walileta mboa nyingi za mierezi kwa Daudi azihesabu.) 5 Daudi akasema, “Mwanangu Sulemani ni mdogo na hana uzoefu, na nyumba itayo jengwa kwa Yahweh lazima iwe maridadi, ilikwamba iwe maarufu na ya utukufu kwa nchi zingine. Hivyo nitaanda ujenzi wake.” Hivyo Daudi akafanya maandalizi ya kina kabla ya mauti yake. 6 Akaagiza Sulemani mwanae kuitwa na kumuamuru ajenge nyumba ya Yahweh, Mungu wa Israeli. 7 Daudi akasema kwa Sulemani, “Mwanangu, ilikuwa dhamira yangu kujenga nyumba mwenyewe, kwa ajili ya jina la Yahweh Mungu wangu. 8 Lakini Yahweh alikuja kwangu na kusema, 'Wewe umemwaga damu nyingi na umepigana mapambono mengi. Hauta jenga nyumba kwa jina langu, kwasababu umemwaga damu nyingi kwenye ardhi machoni pangu. 9 Walakini, utapata mwana ambaye atakuwa mtu wa amani. Nitampa kupumzika na maadui zake kwa kila upande. Kwa kuwa jina lake litaitwa Sulemani, na nitatoa amani na utulivu kwa Israeli katika siku zake. 10 Ata jenga nyumba kwa jina langu. Ata kuwa mwana wangu, na nitakuwa baba yake. Nitaimarisha kiti cha enzi cha ufalme wake juu ya Israeli. 11 Sasa, mwanangu, Yahweh awe nawe na kukuwezesha kufanikiwa. Uweze kujenga nyumba ya Yahweh Mungu wako, kama alivyo sema utajenga. 12 Yahweh tu akupe uwelewa na ufahamu, ili utii sheria ya Yahweh Mungu wako, ata kapokuweka kiongozi juu ya Israeli. 13 Kisha utafanikiwa, kama tu ukitii maagizo na amri Yahweh alizo mpa Musa kuhusu Israeli. Kuwa hodari na mshujaa. Usiogope wala kufadhaika. 14 Sasa, ona, kwa bidii kubwa nimeandaa kwa ajili ya nyumba ya Yahweh talanta 100, 000 za dhahabu, talanta milioni moja za fedha, na shaba na chuma katika idadi kubwa. Pia nimetoa mbao na mawe. Lazima uongeze zaidi katika haya. 15 Una wafanya kazi wengi: wachonga mawe, maseremala, wanaume wenye ujuzi mbali mbali, 16 wenye uwezo wa kufanya kazi na dhahabu, fedha, shaba, na nishati. Hivyo anza kufanya kazi, na Yahweh awe nawe. 17 Daudi akawaagiza viongozi wote Waisraeli wamsaidie Sulemani mwanae, akisema, 18 “Yahweh Mungu wenu yupo nanyi na amewapa amani kila pande. Amewakabidhi mikononi mwangu wenyeji wote mkoa. Mkoa umetiishwa mbele za Yahweh na watu wake. 19 Sasa mtafuteni Yahweh Mungu wenu kwa moyo wenu wote na nafsi. Simameni na mjenge sehemu takatifu ya Yahweh Mungu. Kisha mwaweza kuleta sanduku la agano la Yahweh na vitu vya Mungu ndani ya nyumba iliyo jengwa kwa ajili ya jina la Yahweh.

< 1 Nyakati 22 >