< 1 Nyakati 2 >

1 Hawa ndio wana wa Israeli: Reubeni, Simioni, Lawi, Yuda, Isakari, Zebuloni, 2 Dani, Yusufu, Benyamini, Naftali, Gadi, na Asheri. 3 Wana wa Yuda walikuwa Eri, Onani, na Shela, ambao walizaliwa na binti wa Shua, Wakanaani. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa muovu katika macho ya Yahweh, na Yahweh akamwua. 4 Tamari, mkwe wake, alimzalia Peresi na Zera. Yuda alikuwa na wana wa kiume wa tano. 5 Wana wa Peresi walikuwa Hesroni na Hamuli. 6 Wana wa Zera walikuwa Zimri, Ethani, Hemani, Kalikoli na Darda, wote kwa jumla ni watano. 7 Mwana wa Karmi alikuwa ni Akani, aliye leta taabu katika Israeli alipo iba kile kilicho hifadhiwa kwa ajili ya Mungu. 8 Mwana wa Ethani alikuwa Azaria. 9 Wana wa Hezroni walikuwa ni Yerameeli, Ramu, na Kalebu. 10 Ramu akawa baba wa Aminadabu, na Aminadabu akawa baba wa Nashoni, kiongozi miongoni uzao wa Yuda. 11 Nashoni akawa baba wa Salmoni, na Salmon akawa baba wa Boazi. 12 Boazi akawa baba wa Obedi, na Obedi akawa baba wa Yese. 13 Yese akawa baba wa mzaliwa wake wa kwanza Eliabu, wa pili Abinadabu, wa tatu Shama. 14 Nethaneli wa nne, Radai wa tano. 15 Ozemu wa sita, na Daudi wa saba. 16 Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa Abishai, Yoabu, na Asaheli, jumla watatu. 17 Abigali akamzaa Amasa, ambaye baba yake alikuwa Yetheri Mwishmaeli. 18 Kalebu mwana wa Hesroni akawa baba wa watoto wa Azubu mkewe, na Yeriothi. Wanawe walikuwa Yesheri, Shobabu, na Ardoni. 19 Azuba akafa, na Kalebu akamuoa Efrathi, aliye mzalia Huri. 20 Huri akawa baba wa Uri, na Uri akawa baba wa Besaleli. 21 Baadae Hesroni (alipo kuwa na miaka sitini) akamuoa binti wa Makiri, baba wa Gileadi. Akamzalia Segubu. 22 Segubu akawa baba wa Yairi, aliye miliki miji ishirini na mitatu katika nchi ya Gileadi. 23 Geshuri na Aramu wakawapokonya miji ya Yairi na Kenathi, pamoja na miji sitini iliyo zunguka. Hawa wakazi wote walikuwa ni uzao wa Makiri, baba wa Gileadi. 24 Baada ya kifo cha Hesroni, Kalebu akalala na Efrata, mke wa baba yake Hesroni. Akamzalia Ashuri, baba wa Tekoa. 25 Wana wa Yerameeli, mzaliwa wa kwanza wa Hesroni, walikuwa ni Ramu mzaliwa wa kwanza, Buna, Oreni, Ozemu, na Ahiya. 26 Yerameeli alikuwa na mke mwingine, Jina lake lilikuwa Atara. Yeye alikuwa mama wa Onamu. 27 Wana wa Ramu, mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli, walikuwa Maasi, Yamini, na Ekeri. 28 Wana wa Onamu walikuwa ni Shamai na Yada. Wana wa Shamai walikuwa ni Nadabu na Abishuri. 29 Jina la mke wa Abishuri lilikuwa Abihaili, na akamzalia Abani na Molidi. 30 Wana wa Nadabu walikuwa Seledi na Apaimu, lakini Seledi alikufa pasipo watoto. 31 Mwana wa Apaimu alikuwa Ishi. Mwana wa Ishi alikuwa Sheshani. Mwana wa Sheshani alikuwa Alai. 32 Wana wa Yada, kaka yake Shamai, walikuwa Yetheri na Yonathani. Yetheri alikufa pasipo mtoto. 33 Wana wa Yonathani walikuwa Pelethi na Zaza. Hawa ndio uzao wa Yerameeli. 34 Sasa Sheshani hakuwa na watoto wa kiume, bali wa kike pekee. Sheshani alikuwa na mtumishi, wa Kimisri, ambaye jina lake lilikuwa Yariha. 35 Sheshani alimkabidhi binti yake kwa Yariha mtumishi wake kama mke wake. Akamzalia Atai. 36 Atai akawa baba wa Nathani, na Nathani akawa baba wa Zabadi. 37 Zabadi akawa baba wa Efalali, na Afalali akawa baba wa Obedi. 38 Obedi akawa baba wa Yehu, na Yehu akawa baba wa Azaria. 39 Azaria akawa baba wa Helesi, na Helesi akawa baba wa Eleasa. 40 Eleasa akawa baba wa Sismai, na Sismai akawa baba wa Shalumu. 41 Shalumu akawa baba wa Yekamia, na Yekamia akawa baba wa Elishama. 42 Wana wa Kalebu, kaka yake Yerameeli, walikuwa ni Mesha mzaliwa wake wa kwanza, aliye kuwa baba wa Zifu. Mwanae wa pili, Maresha, allikuwa baba wa Hebroni. 43 Wana wa Hebroni walikuwa Kora, Tapua, Rekemu, na Shema. 44 Shema akawa baba wa Rahamu, baba wa Yorkeamu. Rekemu akawa baba wa Shamai. 45 Mwana wa Shamai alikuwa Maoni, na Maoni alikuwa baba wa Bethsuri. 46 Efa, suria wa Kalebu, alimza Harani, Mosa, na Gazezi. Harani akawa baba wa Gazezi. 47 Wana wa Yadai walikuwa Regemu, Yothamu, Geshani, Peleti, Efa, na Shaafa. 48 Maaka, suria wa Kalebu, alimza Sheberi na Tirhana. 49 Pia akamza Shaafu baba wa Madmana, Sheva baba wa Makbena na baba wa Gibea. Binti wa Kalebu alikuwa Aksa. Hawa walikuwa uzao wa Kalebu. 50 Hawa walikuwa wana wa Huri, mzaliwa wake wa kwanza kwa Efratha: Shobali baba wa Kiriath-Yearimu. 51 Salma baba wa Bethlehemu, na Harefu baba wa Beth-gaderi. 52 Shobali baba wa kiriath-Yearimu alikuwa na uzao: Haroe, nusu ya watu Wamenuthite, 53 na ukoo wa Kiriath-Yearimu: Waithri, Waputhi, Washumathi, na Wamishrai. Wasorathi na Waeshtaoli walitoka huku. 54 Ukoo wa Salma ulikuwa kama ufatao: Bethlehemu, Wanetofathi, Atroth-Beth-Yoabu, na nusu ya Wamenuhothi na Wazori, 55 ukoo wa waandishi walio ishi Yabesi: Watirathi, Washimeathi, na Wasukathi. Hawa walikuwa Wakeni walio toka katika uzao wa Hamathi, babu wa Warekabu.

< 1 Nyakati 2 >