< 1 Nyakati 13 >

1 Daudi akashuriana na wakuu wa jeshi la maelfu na mamia, na kila kiongozi. 2 Daudi akasema kwa kusanyiko la Isaraeli, “Kama itakuwa vyema, na kama hii inatoka kwa Yahweh Mungu wetu, na tutume wajumbe kila sehemu kwa ndugu zetu walio baki maeneo yote ya Israeli, na kwa makuhani na Walawi walio kwenye miji yao. Waambiwe wajiunge nasi. 3 Na tulete sanduku la Mungu wetu, kwa kuwa hatukutafuta mapenzi yake katika siku za Sauli.” 4 Kusanyiko lote liliafiki kufanya haya yote, kwa kuwa yalionekana sawa machoni pa watu wote. 5 Kwaiyo Daudi akakusanya Israeli yote, kutoka mto Shihori ulio Misri hadi Lebo Hamathi, kuleta sandaku la Mungu kutoka Kiriathi Yearimu. 6 Daudi na Israeli yote walienda mpaka Baala, ambayo ni, Kiriathi Yearimu, ambao ni ya Yuda, kuleta sanduku la Mungu, ambalo linaitwa kwa jina la Yahweh, Yahweh, ambaye ameketi juu ya makerubi. 7 Kwaiyo wakaketisha sanduku la Mungu juu ya chombo kipya cha matairi. Wakaleta nje ya nyumba ya Abinadabu. Uza na Ahio walikuwa wakilinda hicho chombo. 8 Daudi na Israeli yote walikuwa wakishangilia mbele za Mungu kwa nguvu zao zote. Walikuwa wakiimba na vyombo vya uzi, vinubi, upatu, na tarumbeta. 9 Walipo kuja eneo la kupeta mazao huko Kidoni, Uza alinyoosha mkono wake kuzuia sandaku, sababu ng'ombe aliyekuwa amebeba sanduku aliyumba. 10 Hasira ya Yahweh ikawaka juu ya Uza, na Yahweh akamua kwasababu Uza alishika na mkono wake sanduku. Akafa pale mbele za Mungu. 11 Daudi alipatwa na hasira kwa kuwa Yahweh alimshambulia Uza. Hiyo sehemu inaitwa Perezi Uza hadi leo. 12 Daudi alimuogopa Mungu hiyo siku. Akasema, “Nawezaje kuleta sanduku la Mungu nyumbani mwangu?” 13 Kwaiyo Daudi hakuleta sanduku kwenye mji wa Daudi, lakini aliweka pembeni mwa nyumba ya Obedi Edomu Mgiti. 14 Sanduku la Mungu lilibaki nyumbani mwa Obedi Edomu kwa miezi mitatu. Kwaiyo Yahweh akabariki nyumba yake na yote aliyo miliki.

< 1 Nyakati 13 >