< Zaburi 16 >

1 Utenzi wa Daudi. Ee Mungu, uniweke salama, kwa maana kwako nimekimbilia. 2 Nilimwambia Bwana, “Wewe ndiwe Bwana wangu; pasipo wewe sina jambo jema.” 3 Kwa habari ya watakatifu walioko duniani, ndio walio wa fahari ambao ninapendezwa nao. 4 Huzuni itaongezeka kwa wale wanaokimbilia miungu mingine. Sitazimimina sadaka zao za damu au kutaja majina yao midomoni mwangu. 5 Bwana umeniwekea fungu langu na kikombe changu; umeyafanya mambo yangu yote yawe salama. 6 Alama za mipaka zimeniangukia mahali pazuri, hakika nimepata urithi mzuri. 7 Nitamsifu Bwana ambaye hunishauri, hata wakati wa usiku moyo wangu hunifundisha. 8 Nimemweka Bwana mbele yangu daima. Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume, sitatikisika. 9 Kwa hiyo moyo wangu unafurahia, na ulimi wangu unashangilia; mwili wangu nao utapumzika salama, 10 kwa maana hutaniacha kaburini, wala hutamwacha Mtakatifu Wako kuona uharibifu. (Sheol h7585) 11 Umenijulisha njia ya uzima; utanijaza na furaha mbele zako, pamoja na furaha za milele katika mkono wako wa kuume.

< Zaburi 16 >