< Zaburi 121 >

1 Wimbo wa kwenda juu. Nayainua macho yangu nitazame vilima, msaada wangu utatoka wapi? 2 Msaada wangu hutoka kwa Bwana, Muumba wa mbingu na dunia. 3 Hatauacha mguu wako uteleze, yeye akulindaye hatasinzia, 4 hakika, yeye alindaye Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi. 5 Bwana anakulinda, Bwana ni uvuli wako mkono wako wa kuume, 6 jua halitakudhuru mchana, wala mwezi wakati wa usiku. 7 Bwana atakukinga na madhara yote, atayalinda maisha yako, 8 Bwana atakulinda unapoingia na unapotoka, tangu sasa na hata milele.

< Zaburi 121 >