< Luka 15 >

1 Basi watoza ushuru na wenye dhambi wote walikuwa wanakusanyika ili wapate kumsikiliza Yesu.
Basi watoza ushuru wote na wengine wenye dhambi walikuja kwa Yesu na kumsikiliza.
2 Lakini Mafarisayo na walimu wa sheria wakanungʼunika wakisema, “Huyu mtu anawakaribisha wenye dhambi na kula nao.”
Mafarisayowaote na waandishi wakanung'unika wakisema, “Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi na hata hula nao.”
3 Ndipo Yesu akawaambia mfano huu:
Yesu akasema mfano huu kwao, akisema
4 “Ikiwa mmoja wenu ana kondoo mia moja, naye akapoteza mmoja wao, je, hawaachi wale tisini na tisa nyikani na kwenda kumtafuta huyo aliyepotea mpaka ampate?
“Nani kwenu, kama ana kondoo mia moja na akipotelewa na mmoja wao, hatawaacha wale tisini na tisa nyikani, na aende akamtafute yule aliyepotea hadi amwone?
5 Naye akishampata, humbeba mabegani mwake kwa furaha
Naye akisha kumpata humweka mabegani pake na kufurahia.
6 na kwenda nyumbani. Kisha huwaita rafiki zake na majirani, na kuwaambia, ‘Furahini pamoja nami; nimempata kondoo wangu aliyepotea.’
Afikapo kwenye nyumba, huwaita rafiki zake na jirani zake akawaambia furahini pamoja nami, kwa kuwa nimempata kondoo wangu aliyepotea.'
7 Nawaambieni, vivyo hivyo kutakuwa na furaha zaidi mbinguni kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu.”
nawaambia vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, zaidi ya wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu
8 “Au ikiwa mwanamke ana sarafu za fedha kumi, naye akapoteza moja, je, hawashi taa na kufagia nyumba na kuitafuta kwa bidii mpaka aipate?
Au kuna mwanamke gani mwenye sarafu kumi za fedha, akipotewa na sarafua moja, hata washa taa na kufagia nyumba na kutafuta kwa bidii hadi atakapoipata?
9 Naye akiisha kuipata, huwaita rafiki zake na majirani na kuwaambia, ‘Furahini pamoja nami; nimeipata ile sarafu yangu ya fedha iliyopotea.’
Na akiisha kuiona huwaita rafiki zake na jirani zake akawaambia furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena sarafu yangu niliyokua nimeipoteza.
10 Vivyo hivyo, nawaambia, kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu juu ya mwenye dhambi mmoja atubuye.”
Hata hivyo nawaambia kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.”
11 Yesu akaendelea kusema: “Kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa na wana wawili.
Na Yesu akasema, “Mtu mmoja alikua na wana wawili
12 Yule mdogo akamwambia baba yake, ‘Baba, nipe urithi wangu.’ Hivyo akawagawia wanawe mali yake.
yule mdogo akamwambia babaye, Baba nipe sehemu ya mali inayonistali kuirithi. Hivyo akagawanya mali zake kati yao.
13 “Baada ya muda mfupi, yule mdogo akakusanya vitu vyote alivyokuwa navyo, akaenda nchi ya mbali, na huko akaitapanya mali yake kwa maisha ya anasa.
Siku si nyingi yule mdogo akakusanya vyote anavyomiliki akaenda nchi ya mbali, na huko akatapanya hela zake, kwa kununua vitu asivyo vihitaji, na kutapanya fedha zake kwa anasa.
14 Baada ya kutumia kila kitu alichokuwa nacho, kukawa na njaa kali katika nchi ile yote, naye akawa hana chochote.
Nae alipokua amekwisha tumia vyote njaa kuu iliingia nchi ile naye akaanza kuwa katika uhitaji.
15 Kwa hiyo akaenda akaajiriwa na mwenyeji mmoja wa nchi ile ambaye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe.
Akaenda na kujiajiri mwenyewe kwa mmoja wa raia wa nchi ile, naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe.
16 Akatamani kujishibisha kwa maganda waliyokula wale nguruwe, wala hakuna mtu aliyempa chochote.
Na akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe kwa sababu hakuna mtu aliempa kitu chochote apate kula.
17 “Lakini alipozingatia moyoni mwake, akasema, ‘Ni watumishi wangapi walioajiriwa na baba yangu ambao wana chakula cha kuwatosha na kusaza, bali mimi hapa nakufa kwa njaa!
Ila yule mwana mdogo alipozingatia moyoni mwake, alisema 'ni watumishi wangapi wa baba yangu wanachakula kingi cha kutosha na mimi niko hapa, ninakufa na njaa!
18 Nitaondoka na kurudi kwa baba yangu na kumwambia: Baba, nimetenda dhambi mbele za Mungu na mbele yako.
Nitaondoka na kwenda kwa baba yangu, na kumwambia, “Baba nimekosa juu ya mbingu na mbele ya macho yako.
19 Sistahili tena kuitwa mwanao; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.’
Sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.”
20 Basi akaondoka, akaenda kwa baba yake. “Lakini alipokuwa bado yuko mbali, baba yake akamwona, moyo wake ukajawa na huruma. Akamkimbilia mwanawe, akamkumbatia na kumbusu.
Ndipo akaondoka akaenda kwa baba yake. Alipokua angali mbali baba yake alimuona akamwonea huruma akaenda mbio na kumkumbatia na kumbusu.
21 “Yule mwana akamwambia baba yake, ‘Baba, nimekosa mbele za Mungu na mbele yako. Sistahili kuitwa mwanao tena.’
Yule mwana akamwambia, 'baba nimekosa juu ya mbingu na mbele ya macho yako sistahili kuitwa mwana wako.'
22 “Lakini baba yake akawaambia watumishi, ‘Leteni upesi joho lililo bora sana, tieni pete kidoleni mwake na viatu miguuni mwake.
Yule baba aliwaambia watumishi wake, 'lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike mtieni na pete kidoleni na viatu miguuni.
23 Leteni ndama aliyenona, mkamchinje ili tuwe na karamu, tule na kufurahi.
Kisha mleteni ndama yule alienona mkamchinje tule na kufurai.
24 Kwa maana huyu mwanangu alikuwa amekufa na sasa yu hai tena; alikuwa amepotea na sasa amepatikana!’ Nao wakaanza kufanya tafrija.
Kwa kuwa mwanangu alikua amekufa naye yu hai. Alikua amepotea nae ameonekana wakaanza kushangilia.
25 “Wakati huo, yule mwana mkubwa alikuwa shambani. Alipokaribia nyumbani, akasikia sauti ya nyimbo na watu wakicheza.
Basi yule mwanae mkubwa alikuwako shamba. Alipokuwa akija na kuikaribia nyumba alisikia sauti ya nyimbo na michezo.
26 Akamwita mmoja wa watumishi na kumuuliza, ‘Kuna nini?’
Akaita mtumishi mmoja akamuuliza mambo haya maana yake nini?
27 Akamwambia, ‘Ndugu yako amekuja, naye baba yako amemchinjia ndama aliyenona kwa sababu mwanawe amerudi nyumbani akiwa salama na mzima.’
Mtumishi akamwambia mdogo wako amekuja na baba yako amemchinjia ndama aliyenona kwa sababu amerudi salama.'
28 “Yule mwana mkubwa akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi baba yake akatoka nje na kumsihi.
Mwana mkubwa akakasirika akakataa kuingia ndani na babaye alitoka nje kumsihi.
29 Lakini yeye akamjibu baba yake, ‘Tazama! Miaka yote hii nimekutumikia na hata siku moja sijaacha kutii amri zako, lakini hujanipa hata mwana-mbuzi ili nifurahi na rafiki zangu.
Ila akamjibu babayake akisema, 'Tazama mimi nimekutumikia miaka mingi, wala sijakosa amri yako, lakini hujanipa mwana mbuzi, ili niweze kusherehekea na rafiki zangu.
30 Lakini huyu mwanao ambaye ametapanya mali yako kwa makahaba aliporudi nyumbani, wewe umemchinjia ndama aliyenona!’
Lakini alipokuja huyu mwana wako aliyetapanya mali yako yote pamoja na makahaba umemchinjia ndama alienona.
31 “Baba yake akamjibu, ‘Mwanangu, umekuwa nami siku zote na vyote nilivyo navyo ni vyako.
Baba akamwambia, 'Mwanangu, wewe u pamoja nami siku zote na vyote nilivyo navyo ni vyako.
32 Lakini ilitubidi tufurahi na kushangilia kwa sababu huyu ndugu yako alikuwa amekufa na sasa yu hai; alikuwa amepotea naye amepatikana.’”
Ila ilikua vyema kwetu kufanya sherehe na kufurahi, huyu ndugu yako alikua amekufa, na sasa yu hai; alikua amepotea naye ameonekana.”

< Luka 15 >