< Maombolezo 3 >

1 Mimi ndiye mtu aliyeona mateso kwa fimbo ya ghadhabu yake.
אני הגבר ראה עני בשבט עברתו
2 Amenifukuzia mbali na kunifanya nitembee gizani wala si katika nuru;
אותי נהג וילך חשך ולא אור
3 hakika, amegeuza mkono wake dhidi yangu tena na tena, mchana kutwa.
אך בי ישב יהפך ידו כל היום
4 Amefanya ngozi yangu na nyama yangu kuchakaa na ameivunja mifupa yangu.
בלה בשרי ועורי שבר עצמותי
5 Amenizingira na kunizunguka kwa uchungu na taabu.
בנה עלי ויקף ראש ותלאה
6 Amenifanya niishi gizani kama wale waliokufa.
במחשכים הושיבני כמתי עולם
7 Amenizungushia ukuta ili nisiweze kutoroka, amenifunga kwa minyororo mizito.
גדר בעדי ולא אצא הכביד נחשתי
8 Hata ninapoita au kulia ili kuomba msaada, anakataa kupokea maombi yangu.
גם כי אזעק ואשוע שתם תפלתי
9 Ameizuia njia yangu kwa mapande ya mawe, amepotosha njia zangu.
גדר דרכי בגזית נתיבתי עוה
10 Kama dubu aviziaye, kama simba mafichoni,
דב ארב הוא לי אריה (ארי) במסתרים
11 ameniburuta kutoka njia, akanirarua na kuniacha bila msaada.
דרכי סורר ויפשחני שמני שמם
12 Amevuta upinde wake na kunifanya mimi niwe lengo kwa ajili ya mishale yake.
דרך קשתו ויציבני כמטרא לחץ
13 Alinichoma moyo wangu kwa mishale iliyotoka kwenye podo lake.
הביא בכליתי בני אשפתו
14 Nimekuwa kichekesho kwa watu wangu wote, wananidhihaki kwa wimbo mchana kutwa.
הייתי שחק לכל עמי נגינתם כל היום
15 Amenijaza kwa majani machungu na kunishibisha kwa nyongo.
השביעני במרורים הרוני לענה
16 Amevunja meno yangu kwa changarawe, amenikanyagia mavumbini.
ויגרס בחצץ שני הכפישני באפר
17 Amani yangu imeondolewa, nimesahau kufanikiwa ni nini.
ותזנח משלום נפשי נשיתי טובה
18 Kwa hiyo nasema, “Fahari yangu imeondoka na yale yote niliyokuwa nimetarajia kutoka kwa Bwana.”
ואמר אבד נצחי ותוחלתי מיהוה
19 Nayakumbuka mateso yangu na kutangatanga kwangu, uchungu na nyongo.
זכר עניי ומרודי לענה וראש
20 Ninayakumbuka vyema, nayo nafsi yangu imezimia ndani yangu.
זכור תזכור ותשיח (ותשוח) עלי נפשי
21 Hata hivyo najikumbusha neno hili na kwa hiyo ninalo tumaini.
זאת אשיב אל לבי על כן אוחיל
22 Kwa sababu ya upendo mkuu wa Bwana, hatuangamii, kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe.
חסדי יהוה כי לא תמנו כי לא כלו רחמיו
23 Ni mpya kila asubuhi, uaminifu wako ni mkuu.
חדשים לבקרים רבה אמונתך
24 Nimeiambia nafsi yangu, “Bwana ni fungu langu, kwa hiyo nitamngojea.”
חלקי יהוה אמרה נפשי על כן אוחיל לו
25 Bwana ni mwema kwa wale ambao tumaini lao ni kwake, kwa yule ambaye humtafuta;
טוב יהוה לקוו לנפש תדרשנו
26 ni vyema kungojea kwa utulivu kwa ajili ya wokovu wa Bwana.
טוב ויחיל ודומם לתשועת יהוה
27 Ni vyema mtu kuchukua nira bado angali kijana.
טוב לגבר כי ישא על בנעוריו
28 Na akae peke yake awe kimya, kwa maana Bwana ameiweka juu yake.
ישב בדד וידם כי נטל עליו
29 Na azike uso wake mavumbini bado panawezekana kuwa na matumaini.
יתן בעפר פיהו אולי יש תקוה
30 Na atoe shavu lake kwa yule ampigaye, na ajazwe na aibu.
יתן למכהו לחי ישבע בחרפה
31 Kwa kuwa watu hawakatiliwi mbali na Bwana milele.
כי לא יזנח לעולם אדני
32 Ingawa huleta huzuni, ataonyesha huruma, kwa kuwa upendo wake usiokoma ni mkuu.
כי אם הוגה ורחם כרב חסדיו
33 Kwa maana hapendi kuwaletea mateso au huzuni watoto wa wanadamu.
כי לא ענה מלבו ויגה בני איש
34 Kuwaponda chini ya nyayo wafungwa wote katika nchi,
לדכא תחת רגליו כל אסירי ארץ
35 Kumnyima mtu haki zake mbele za Aliye Juu Sana,
להטות משפט גבר נגד פני עליון
36 kumnyima mtu haki: Je, Bwana asione mambo kama haya?
לעות אדם בריבו אדני לא ראה
37 Nani awezaye kusema nalo likatendeka kama Bwana hajaamuru?
מי זה אמר ותהי אדני לא צוה
38 Je, si ni kwenye kinywa cha Aliye Juu Sana ndiko yatokako maafa na mambo mema?
מפי עליון לא תצא הרעות והטוב
39 Mwanadamu yeyote aliye hai aweza kulalamika wakati anapoadhibiwa kwa ajili ya dhambi zake?
מה יתאונן אדם חי גבר על חטאו
40 Tuzichunguze njia zetu na kuzijaribu, na tumrudie Bwana Mungu.
נחפשה דרכינו ונחקרה ונשובה עד יהוה
41 Tuinue mioyo yetu pamoja na mikono yetu kwa Mungu mbinguni, na tuseme:
נשא לבבנו אל כפים אל אל בשמים
42 “Tumetenda dhambi na kuasi nawe hujasamehe.
נחנו פשענו ומרינו אתה לא סלחת
43 “Umejifunika mwenyewe kwa hasira na kutufuatilia; umetuchinja bila huruma.
סכותה באף ותרדפנו הרגת לא חמלת
44 Unajifunika mwenyewe kwa wingu, ili pasiwe na ombi litakaloweza kupenya.
סכותה בענן לך מעבור תפלה
45 Umetufanya takataka na uchafu miongoni mwa mataifa.
סחי ומאוס תשימנו בקרב העמים
46 “Adui zetu wote wamefumbua vinywa vyao wazi dhidi yetu.
פצו עלינו פיהם כל איבינו
47 Tumeteseka kwa hofu kuu na shida ya ghafula, uharibifu na maangamizi.”
פחד ופחת היה לנו השאת והשבר
48 Vijito vya machozi vinatiririka kutoka machoni mwangu, kwa sababu watu wangu wameangamizwa.
פלגי מים תרד עיני על שבר בת עמי
49 Macho yangu yatatiririka machozi bila kukoma, bila kupata nafuu,
עיני נגרה ולא תדמה מאין הפגות
50 hadi Bwana atazame chini kutoka mbinguni na kuona.
עד ישקיף וירא יהוה משמים
51 Lile ninaloliona huniletea huzuni nafsini kwa sababu ya wanawake wote wa mji wangu.
עיני עוללה לנפשי מכל בנות עירי
52 Wale waliokuwa adui zangu bila sababu wameniwinda kama ndege.
צוד צדוני כצפור איבי חנם
53 Walijaribu kukomesha maisha yangu ndani ya shimo na kunitupia mawe;
צמתו בבור חיי וידו אבן בי
54 maji yalifunika juu ya kichwa changu, nami nikafikiri nilikuwa karibu kukatiliwa mbali.
צפו מים על ראשי אמרתי נגזרתי
55 Nililiitia jina lako, Ee Bwana, kutoka vina vya shimo.
קראתי שמך יהוה מבור תחתיות
56 Ulisikia ombi langu: “Usikizibie masikio yako kilio changu nikuombapo msaada.”
קולי שמעת אל תעלם אזנך לרוחתי לשועתי
57 Ulikuja karibu nilipokuita, nawe ukasema, “Usiogope.”
קרבת ביום אקראך אמרת אל תירא
58 Ee Bwana, ulichukua shauri langu, ukaukomboa uhai wangu.
רבת אדני ריבי נפשי גאלת חיי
59 Umeona, Ee Bwana, ubaya niliotendewa. Tetea shauri langu!
ראיתה יהוה עותתי שפטה משפטי
60 Umeona kina cha kisasi chao, mashauri yao yote mabaya dhidi yangu.
ראיתה כל נקמתם--כל מחשבתם לי
61 Ee Bwana, umesikia matukano yao, mashauri yao yote mabaya dhidi yangu:
שמעת חרפתם יהוה כל מחשבתם עלי
62 kile adui zangu wanachonongʼona na kunungʼunikia dhidi yangu mchana kutwa.
שפתי קמי והגיונם עלי כל היום
63 Watazame! Wakiwa wameketi au wamesimama, wananidhihaki katika nyimbo zao.
שבתם וקימתם הביטה אני מנגינתם
64 Uwalipe kile wanachostahili, Ee Bwana, kwa yale ambayo mikono yao imetenda.
תשיב להם גמול יהוה כמעשה ידיהם
65 Weka pazia juu ya mioyo yao, laana yako na iwe juu yao!
תתן להם מגנת לב תאלתך להם
66 Wafuatilie katika hasira na uwaangamize kutoka chini ya mbingu za Bwana.
תרדף באף ותשמידם מתחת שמי יהוה

< Maombolezo 3 >