< Salmos 60 >

1 Dios, desechástenos, disipástenos; airástete, vuélvete a nosotros.
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Shushani Eduthi.” Utenzi wa Daudi wa kufundisha. Wakati alipopigana na Waaramu kutoka Aramu-Naharaimu na Aramu-Soba, naye Yoabu akarudi nyuma na kuwaua Waedomu 12,000 katika Bonde la Chumvi. Ee Mungu, umetukataa na kutokea ghafula juu yetu, umekasirika: sasa turejeshe upya!
2 Hiciste temblar la tierra, abrístela; sana sus quebraduras, porque titubea.
Umetetemesha nchi na kuipasua; uiponye mavunjiko yake, kwa maana inatetemeka.
3 Hiciste ver a tu pueblo duras cosas: hicístenos beber vino de temblor.
Umewaonyesha watu wako nyakati za kukata tamaa; umetunywesha mvinyo unaotuyumbisha.
4 Has dado a los que te temen una bandera que alcen por amor de la verdad. (Selah)
Kwa wale wanaokucha wewe, umewainulia bendera, ili iweze kutwekwa dhidi ya upinde.
5 Para que se escapen tus amados: salva con tu diestra, y óyeme.
Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume, ili wale uwapendao wapate kuokolewa.
6 Dios habló en su santidad: Yo me alegraré: partiré a Siquem, y mediré al valle de Socot.
Mungu amenena kutoka patakatifu pake: “Nitaigawa Shekemu kwa ushindi na kulipima Bonde la Sukothi.
7 Mío es Galaad, y mío es Manasés: y Efraím es la fortaleza de mi cabeza; Judá mi legislador;
Gileadi ni yangu na Manase ni yangu; Efraimu ni kofia yangu ya chuma, nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala.
8 Moab, la olla de mi lavatorio: sobre Edom echaré mi zapato; sobre mí triunfa, o! Palestina.
Moabu ni sinia langu la kunawia, juu ya Edomu natupa kiatu changu; nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.”
9 ¿Quién me llevará a la ciudad fortalecida? ¿quién me llevará hasta Idumea?
Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome? Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu?
10 Ciertamente tú, o! Dios, que nos habías desechado; y no salías, o! Dios, con nuestros ejércitos.
Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi, na hutoki tena na majeshi yetu?
11 Dános socorro contra el enemigo, que vana es la salud de los hombres.
Tuletee msaada dhidi ya adui, kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu.
12 En Dios haremos proezas; y él pisará nuestros enemigos.
Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi, naye atawaponda adui zetu.

< Salmos 60 >