< Isaías 10 >

1 ¡Ay de los que establecen leyes injustas, y determinando determinan tiranía:
Ole wao watimizao sheria zisizo za haki na waandikao sheria zisizo na haki.
2 Por apartar del juicio a los pobres, y por quitar el derecho a los afligidos de mi pueblo: por despojar las viudas, y robar los huérfanos!
Wanawanyima wahitaji haki yao, wanawaibia watu wangu walio masikini haki zao, wajane mateka wao, na kuwafanya waliofiwa na baba zao mawindo yao!
3 ¿Y qué haréis en el día de la visitación? ¿y a quién os acogeréis que os ayude, cuando viniere de lejos el asolamiento? ¿y en dónde dejaréis vuestra gloria?
Hutafanya nini siku ya hukumu pale siku ya uaribifu itakapokuja kutoka mbali, utakimbilia msaada kwa nani? na utauacha utajiri wako wapi?
4 Sin mí se inclinaron entre los presos; y cayeron entre los muertos. Ni con todo eso cesará su furor, antes todavía su mano extendida.
Hakuna kitakachobaki, utaota miongoni mwa wafungwa au kuanguka miongoni mwa wauwaji. Katika mambo yote haya, hasira yake haijapungua; badala yake mkono wake ameunjoosha hata sasa.
5 O! Asur, vara de mi furor, y palo él mismo, mi enojo en la mano de ellos.
Ole kwa watu wa Asiria klabu ya asira yangu, fimbo ya asira yangu!
6 Enviarle he contra nación fingida; y sobre pueblo de mi ira le enviaré, para que despoje despojos, y robe presa, y que lo ponga que sea hollado, como lodo de las calles.
Nimemtuma juu ya taifa lenye kiburi na juu ya watu waliobeba uwingi wa hasira. Ninaamuru chukua nyara, chukua mawindo, na kuwakanyaga wao kama matope mitaani.
7 Aunque él no lo pensará así, ni su corazón lo imaginará de esta manera: mas su pensamiento será de desarraigar, y cortar naciones no pocas.
Lakini hichi sicho alichomaanisha, wala sivyo afikiriavyo. Maana katika moyo wake ni kuharibu na kuondoa mataifa.
8 Porque él dirá: ¿Mis príncipes no son todos reyes?
Maana amesema, '' wakuu wote sio wafalme?
9 ¿No es Calno como Carcamis; Armad como Arfad; y Samaria como Damasco?
Je? kalno si kama Karkemish? Je Hamathi si kama Arpadi? Je Samaria si kama Demeski?
10 Como halló mi mano los reinos de los ídolos, siendo sus imágenes más que Jerusalem y Samaria:
Kama mikono yangu imeshinda falme za ibada ya sanamu, ikiwa sanamu zao za kuchonga ni bora kuliko sanamu za Yerusalemu
11 Como hice a Samaria y a sus ídolos, ¿no haré también así a Jerusalem y a sus ídolos?
na Kama nilivyofanya kule Samaria na sanamu zake zisizo na maana, je sitaweza kufanya hivyo Yerusalemu na sanamu zake?''
12 Mas acontecerá, que después que el Señor hubiere acabado toda su obra en el monte de Sión, y en Jerusalem, visitaré sobre el fruto de la soberbia del corazón del rey de Asiria, y sobre la gloria de la altivez de sus ojos:
Pindi ambapo Bwana alipoimaliza kazi kwenye mlima Sayuni na juu ya Yerusalemu, nitayaadhibu maneno ya moyo wenye kiburi ya mfalme wa Asiria na majivuno yake.
13 Porque dijo: Con fortaleza de mi mano lo he hecho, y con mi sabiduría, porque he sido prudente: que quité los términos de los pueblos, y sus tesoros saqueé; y derribé como valiente los que estaban sentados.
Kwa maana amesema, ''Kwa nguvu zangu na kwa hekima yangu niliyoifanya. na Nimeelewa, na nimeondoa mipaka ya watu. nimewaibia akiba yao, ni kama nilioileta chini kwa wenyeji wake.
14 Y halló mi mano las riquezas de los pueblos, como nido; y como se cojen los huevos dejados, así apañé yo toda la tierra; y no hubo quien moviese ala, o abriese boca y graznase.
Na mkono wangu umezitoa mali za mataifa kama vile mtu ayakusanyavyo mayai, kama nilivyokusanya dunia yote. Hakuna atakayeperusha mabawa yake au kufungua midomo yake au kulia.''
15 ¿Gloriarse ha la segur contra el que corta con ella? ¿ensoberbecerse ha la sierra contra el que la mueve? como si el bordón se levantase contra los que lo levantan; como si la vara se levantase: ¿no es leño?
Je shoka lijisifu lenyewe juu ya mtu anayelitumia? Je litajisifia lenyewe zaidi ya yule anaelitumia kukatia? Au fimbo imuinuae yeye ambaye si mti.
16 Por tanto el Señor Jehová de los ejércitos enviará flaqueza sobre sus gordos; y debajo de su gloria encenderá encendimiento, como encendimiento de fuego.
Hivyo basi Yahwe wa majeshi atatuma wadhaifu miongoni mwa wasomi wa kijeshi; na chini ya utukufu na kuteketea kama kuteketea kwa moto.
17 Y la luz de Israel será por fuego, y su Santo por llama que abrase y consuma en un día sus cardos y sus espinas.
Mwanga wa Isreli utakuwa moto, na Mtakatifu wake atakuwa ni moto unaoteketeza na kula mbigiri siku moja.
18 La gloria de su breña, y de su campo fértil consumirá desde el alma hasta la carne; y será como deshecha de alférez.
Yahwe atauteketeza utukufu wa msitu wake na shamba lake linalostawi, vyote nafsi na mwili; itakuwa kama vile mgonjwa apotezae maisha yake.
19 Y los árboles que quedaren en su breña, serán por cuenta, que un niño los pueda contar.
Mabaka ya miti ya misitu itakuwa michache sana, ambayo mtoto anaweza kuyahesabu.
20 Y acontecerá en aquel tiempo, que los que hubieren quedado de Israel, y los que hubieren quedado de la casa de Jacob, nunca más estriben sobre el que los hirió; porque estribarán sobre Jehová, Santo de Israel, con verdad.
Siku hiyo, mabaki ya Israeli, familia ya Yakobo ambayo imekimbia, hawatategemea kushindwa, lakini watamtegemea Yahwe, Mtakatifu wa Israeli.
21 Los restos se convertirán, los restos de Jacob, al Dios fuerte.
Mabaki ya Yakobo yatarudi kwa Mungu mwenye nguvu.
22 Porque si tu pueblo, o! Israel, fuere como las arenas de la mar, los restos se convertirán en él. La consumación fenecida inunda justicia.
Kwa kupitia watu wako, Israeli ni kama mchanga kama pwani ya bahari, Mabaki yao tu ndio yatakayorudi. Uaribifu wa amri, na mahitaji ya wingi wa haki.
23 Por tanto el Señor Jehová de los ejércitos hará consumación, y fenecimiento en medio de toda la tierra.
Maana Bwana wa majeshi, anakaribia kuleta uharibifu utachukua nafasi kubwa kitika nchi.
24 Por tanto el Señor Jehová de los ejércitos dice así: No temas, pueblo mío, morador de Sión, del Asur. Con vara te herirá, y contra ti alzará su palo por la vía de Egipto:
Hivyo basi Bwana Yahwe wa majeshi anasema, ''watu wangu mhishio Sayuni, msiwaogope watu wa Asiria. Atawangamiza nyie kwa fimbo na atawanyua wafanyakazi juu yenu, kama ilivyotokea kwa Wamisri.
25 Mas desde aun poco, un poquito, se acabará el furor, y mi enojo, para fenecimiento de ellos.
Msimuogope, kwa mda mfupi hasira yangu itakwisha juu yenu, na hasira yangu italeta uharibifu.''
26 Y levantará Jehová de los ejércitos azote contra él, como la matanza de Madián a la peña de Horeb; y alzará su vara sobre la mar, por la vía de Egipto.
Hivyo Yahwe wa majeshi atapiga mjeledi juu yenu kama vile alivyoishinda Midiani karibu na mwamba Orebu. Na atanyanyua fimbo yake juu ya bahari kama alivyofanya kule Misri.
27 Y acaecerá en aquel tiempo, que su carga será quitada de tu hombro, y su yugo de tu cerviz; y el yugo se empodrecerá delante de la unción.
Siku hiyo mzigo wake utanyanyuliwa kwenye mabeba yako na nira katika shingo yako, nayo nira itaharibiwa kwa sababu ya unene.
28 Vino hasta Ajad, pasó hasta Migrón: en Micmas contará su ejército.
Adui amekuja Aiathi na amepitia Migroni; katika Michmashi ameyahifadhi mahitaji yake.
29 Pasaron el vado: alojaron en Geba: Rama tembló: Gabaa de Saul huyó.
Wamevuka juu ya njia na wamepunzika huko Geba. Rama inatetemeka na Gibea ya Sauli imekimbia.
30 Grita a alta voz hija de Gallim: Laisa, haz que te oiga la pobrecilla Anatot.
Lia kwa sauti, ewe binti wa Galimu! sikiliza, Laishashi! Maskini Anathothi!
31 Madmena se alborotó: los moradores de Gebim se juntarán.
Madmena ni mkimbizi na mkazi wa Gebuni wamejikusanya wanakimbia kutafuta msada.
32 Aun vendrá día cuando reposará en Nob: alzará su mano al monte de la hija de Sión, al collado de Jerusalem.
Siku hizi za leo atasimulia huko Nobi na atatingisha mlima wa binti Sayuni, mlima wa Yerusalemu.
33 He aquí que el Señor Jehová de los ejércitos desgajará el ramo con fortaleza; y los de grande altura serán cortados, y los altos serán humillados.
Tazama, Bwana Yahwe wa majeshi atapunguza matawi kwa nguvu za kutisha; miti mirefu itakatwa chini, wanaojivuna wataangushwa.
34 Y cortará con hierro la espesura de la breña; y el Líbano caerá con fortaleza.
Atang'oa vichaka vya msitu kwa shoka, Lebanoni na utukufu wake utaanguka.

< Isaías 10 >