< Ufunuo 1 >

1 Nyaa nga cha umukulilwe Yesu Kirisitu ambao Nnungu apelwe kualangya abandu bake makowew ambago lazima ga pa pilya karibuni. Apangite gatanganikwe kwabkumtuma malaika wake kwa mbanda wake Yohana.
Huu ni ufunuo wa Yesu Kristo ambao Mungu alimpa ili kuwaonesha watumishi wake mambo ambayo lazima yatokee karibuni. Aliyafanya yajulikane kwa kumtuma malaika wake kwa mtumishi wake Yohana.
2 Yohana apiya ushuhuda wa kila kilibe cha kibweni usiana na likowe lya Nnungu ni kwa ushuhuda wa upiite husu Yesu Kirisitu.
Yohana alitoa ushuhuda wa kila kitu alichoona kuhusiana na neno la Mungu na kwa ushuhuda uliotolewa kuhusu Yesu Kristo.
3 Abalikiwe ywembe ywa soma kwa lilobe na balu babayua maneno ga unabii gano na kugatii chakiandikilwe muno, kitumbu muda uti karibia.
Amebarikiwa yeye asomaye kwa sauti na wale wote wanaoyasikia maneno ya unabii huu na kutii kilichoandikwa humo, kwa sababu muda umekaribia.
4 Yohana kwa makanisa saba ga gabile Asia: neema ibe kwinu na amani buka kwa ywabile, ywapabaa, na ywapaicha na buka kwa Roho saba bababile nnongi ya kitigo chake cha enzi.
Yohana, kwa makanisa saba yaliyoko Asia: neema iwe kwenu na amani kutoka kwake aliyepo, aliyekuwepo, na atakayekuja, na kutoka kwa roho saba walio mbele ya kiti chake cha enzi,
5 Na buka kwa Yesu Kirisitu ambeye nga shahidi mwaminifu mmelkekwa wa kwanza ba bawile, na ntawala wa mfalme dunia yino, kwa ywembe ywatupendile na atubikite huru buka mmalau gitu kwa damu yake.
na kutoka kwa Yesu Kristo ambaye ni shahidi mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mtawala wa wafalme wa dunia hii. Kwake yeye atupendaye na ametuweka huru kutoka katika dhambi zetu kwa damu yake,
6 Atupangite panga ufalme wa makuhani wa Nnungu na Tate bake kwake panga tukuka na ngupu milelebdaima. Amina. (aiōn g165)
ametufanya kuwa ufalme, makuhani wa Mungu na Baba yake - kwake kuwa utukufu na nguvu milele daima. Amina. (aiōn g165)
7 Linga andaicha na maunde kila lio lipakumwona pamoja boti babamwomite. Na kabila yoti ya dunia bapakukulika kwake. Ndiyo, Amina.
Tazama, anakuja na mawingu; kila jicho litamwona, pamoja na wote waliomchoma. Na kabila zote za dunia wataomboleza kwake. Ndiyo, Amina.
8 Nenga nga Alfa na Omega abaya Ngwana Nnungu, ywembe ywabile na ywapabaa, na ambaye andaicha mwene ngupu.
“Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu, “Yeye aliyepo, na aliyekuwepo, na ambaye anakuja, Mwenye nguvu.”
9 Nenga Yohana nuna winu na kati yinu ywa shiriki mateso na ufalme na uvumumilia thabiti wa ubile katika Yesu; nabile pa kisiwa cha kikemelwa Patimo kitumbu cha neno la Nnungu na ushuhuda usu Yesu.
Mimi, Yohana - ndugu yenu na mmoja anayeshiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu thabiti ulio katika Yesu; nilikuwa katika kisiwa kiitwacho Patimo kwa sababu ya neno la Mungu na ushuhuda kuhusu Yesu.
10 Nabile katika Roho lichuba la Ngwana, nayuwine nchugu yangu lilobe la kunani kati ya tarumbeta,
Nilikuwa katika Roho siku ya Bwana. Nilisikia nyuma yangu sauti ya juu kama ya tarumbeta,
11 Yaibaya, uandike katika kitabu ga ugabona na ugatume kwa makanisa saba yenda Efeso, yenda Smima, yenda Pergamo, yenda Thiatira, yenda Sardi, yenda Philadelphia na yenda Laodikia.
ikisema, “andika katika kitabu unayo yaona, na uyatume kwa makanisa saba, kwenda Efeso, kwenda Smirna, kwenda Pergamo, kwenda Thiatira, kwenda Sardi, kwenda Philadelphia, na kwenda Laodikia.”
12 Nitigalambuka linga ni lilobe lya nyai ywabile kalongela na nee, na panigalambwike nabweni kinara cha dhahabu cha taa saba.
Nikageuka kuona ni sauti ya nani aliyekuwa akiongea nami, na nilipogeuka niliona kinara cha dhahabu cha taa saba.
13 Pakatikati ya kinara cha taa abile yumo kati mwana wa Adamu, aweti ngamu ndacho yaukite pai ya magulu gake, na mkanda wa dhahabu tindia pa kiuba.
Katikati ya kinara cha taa alikuwemo mmoja kama Mwana wa Adamu, amevaa kanzu ndefu iliyofika chini ya miguu yake, na mkanda wa dhababu kuzunguka kifua chake.
14 Mtwe wakwe na nywili yake yai uu kati pamba kati barafu na minyo gake gabi mwali wa mwoto.
Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe kama theluji, na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto.
15 Njayo yake yabi kati shaba yahikutilwe sana, kati shaba yaipitile katika mwoto, na lilobe lyake yabi kati machi maingi gaga yenda kwa haraka.
Nyayo zake zilikuwa kama shaba iliyosuguliwa sana, kama shaba ambayo imekwisha pitishwa katika moto, na sauti yake ilikuwa kama sauti ya maji mengi yanayotiririka kwa kasi.
16 Abi akamwi ndondwa saba katika luboko lwake wa mmalyo, na buka mukano wake mwabi na lipanga likale wene makale kuno na kuno. Kuminyo yake kwende ng'araa kati mwenga nkalee walichuba.
Alikuwa ameshikilia nyota saba katika mkono wake wa kuume, na kutoka kinywani mwake kulikuwa na upanga mkali wenye makali kuwili. Uso wake ulikuwa uking'aa kama mwanga mkali wa jua.
17 Pamweni, natitumbuka pamagulu gake kati mundu nywa wile. Abikite luboko lwake mmalyo panani yangu na baya “Kana uyogope” Ninga na wa kwanza na wa mwisho.
Nilipomwona, nikaanguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kulia juu yangu na kusema, “Usiogope! Mimi ni wa kwanza na wa Mwisho,
18 Na ambaye nenda ishi. Nati waa, lakini linga nenda ishi bila waa! Na nibile na funguo ya mautiu na kuzimu. (aiōn g165, Hadēs g86)
na ambaye ninaishi. Nalikuwa nimekufa, lakini tazama, ninaishi milele! Na ninazo funguo za mauti na kuzimu. (aiōn g165, Hadēs g86)
19 Kwaiyo ugaaandike ga ugabweni nambiambi, na galo gagapita baadaye,
Kwa hiyo, yaandike uliyoyaona, yaliyopo sasa, na yale yatakayotokea baada ya haya.
20 kwa maana yaiyubite husu ndondwa saba yauibweni katika luboko lwangu lwa mmalyo, na chilo kinara kinara cha dhahabu cha taa saba: ndondwa saba nga malaika wa makanisa saba, na kinara cha taa saba nga galo makanisa saba.
Kwa maana iliyojificha kuhusu nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na kile kinara cha dhahabu cha taa saba: nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba, na kinara cha taa saba ni yale makanisa saba.”

< Ufunuo 1 >