< Marko 12 >

1 Yesu katumbua kuayegana kwa mifano. Kakoya mundu apandike nngonda wa mizabibu, kuliteteleya lubego na kuemba likinga la kusudikia mvinyo. kasema mnara na kaupangisha nngonda wa zabibu kwa alemi wa zabibu kaboka kutalu.
Kisha Yesu alianza kuwafundisha kwa mifano. Akasema, “Mtu alipanda shamba la mizabibu, akalizungushia uzio, na akachimba shimo la kusindika mvinyo. Akajenga mnara na kisha akalipangisha shamba la mizabibu kwa wakulima wa mizabibu. Kisha alisafiri safari ya mbali.
2 Palyo muda uike, amtumike mtumishi kwa alemi ba zabibu kupokya matunda kuoma kumigonda ya zabibu.
Wakati ulipofika, alimtuma mtumishi kwa wakulima wa mizabibu kupokea kutoka kwao baadhi ya matunda ya shamba la mizabibu.
3 Kaba m'boywa, kabampumunda, na kabam'benga bila ya kumpaya kilebe.
Lakini walimkamata, wakampiga, na wakamfukuza bila chochote.
4 Kantuma kwabe ntumishi ywenge, kabampumunda kumutwe ni kuntendeya mambo ya oni.
Akamtuma kwao mtumishi mwingine, wakamjeruhi kichwani na kumtendea mambo ya aibu.
5 Bado kantuma ywenge yeya, ni yono yumo kabambulaga. Na benge kabantenda mahoba kati aga. Kaba ankombwa benge kaaam'bulaga.
Bado alimtuma mwingine, na huyu mmoja walimwua. Waliwatendea wengine wengi mambo kama hayo hayo, wakiwapiga na wengine kuwaua.
6 Aigile mundu yumo wa kuntuma mwana mpendwa. Ni ywembe awi wa mwisho kutumwa kwabe. Kakoya “Watamsheshim mwanango.”
Alikuwa bado na mtu mmoja zaidi wa kumtuma, mwana mpendwa. Naye alikuwa wa mwisho aliyetumwa kwao. Akisema, “Watamheshimu mwanangu”.
7 Lakini wapangaji kabakoyana bene kwa bene “Yono ndie mrithi. Isaye, tum'bulage ni mrithi wa ba witu.”
Lakini wapangaji walisemezana wao kwa wao, “Huyu ndiye mrithi. Njoni, hebu na tumwue, na urithi utakuwa wetu.”
8 Kaba n'yola, kaba m'bulaga ni kuntaga kunza ya nngonda wa mizabibu.
Walimvamia, wakamuua na kumtupa nje ya shamba la mizabibu.
9 Kwa eyo, atenda kele mwene n'ngonda wa mizabibu? Aisa ni kubaangamiza alemi ba mizabibu na kuapaya benge n'gonda wa zabibu.
Kwa hiyo, Je! Atafanya nini mmiliki wa shamba la mizabibu? Atakuja na kuwaangamiza wakulima wa mizabibu na atalikabidhi shamba la mizabibu kwa wengine.
10 Msomike kwaa andiko elo? Libwe ambalo ajenzi balikani, libi libwe la kumbwega.
Hamjapata kusoma andiko hili? “Jiwe ambalo wajenzi walilikataa, limekuwa jiwe la pembeni.
11 Leno lapii kwa Bwana, na lakukanganya kumminyo gitu.
Hili lilitoka kwa Bwana, na ni la ajabu machoni petu.”
12 Bapai kunkamwa Yesu, lakini baypgwipe kipenga sa bandu, batangike kuba aabakiye mfano wa kilebe soo. Eyo kabanneka kaba boka.
Walitafuta kumkamata Yesu, Lakini waliwaogopa makutano, kwani walijua kuwa alikuwa amenena mfano huo dhidi yao. Hivyo walimwacha na wakaenda zao.
13 Kabatuma mafarisayo ni Maherodia ili kuntega kwa mayegeyo.
Kisha wakawatuma baadhi ya mafarisayo na maherodia kwake ili kumtega kwa maneno.
14 Palyo baike, kabankokeya, “Mwalimu, tutangike ukani mayegeyo gegote ni upendelya kwaa bandu. Uyengana ndela ya Nnongo bwiso. Je, inoike kulepa kodi kwa kaisari au la? Je tulepe au tukotoke?”
Walipofika, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba hujali maoni ya yeyote na huonyeshi upendeleo kati ya watu. Unafundisha njia ya Mungu katika ukweli. Je! Ni haki kulipa kodi kwa Kaisari au la? Je! Twaweza kulipa au la?
15 Yesu kabayangwa uboso wabe nikuakokeya, “Mwalowa kele mwando n'geya? Mbayaye Dinari ni ilole.”
Lakini Yesu alijua unafiki wao na kuwaambia, “Kwa nini mnanijaribu? Nipeni dinari niweze kuitazama.”
16 Kabaleta yimo kwa Yesu, kabaakokeya ni sura ya nyai ni gano maandishi ga nyai? kabakoya “Ya kaisari.”Kabakokeya
Wakaleta moja kwa Yesu, Akawaambia, “Je! ni sura ya nani na maandishi yaliyopo hapa ni ya nani? Wakasema, “Ya Kaisari.”
17 Yesu kabakokeya, mpayaye kaisari ilebe ya kaisari ni Nnongo ilebe ya Nnongo.”Kabankanganya.
Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari vitu vya Kaisari na Mungu vitu vya Mungu.” Wakamstaajabia.
18 Kisha Masadukayo, bakoyae ntopo mfufuo, kaban'yendelelya. kabannokiya, kabakoya,
Kisha Masadukayo, wasemao hakuna ufufuo, walimwendea. Wakamuwuliza, wakisema,
19 “Mwalimu Musa atuandikie kuba, mana mundu awile ni kunleka nnwawa kiogo yake, lakini alei kwa nwawa, mundu kantola wa nnwawa wa nlongoe, ni kuipatia bana mwalo wa nlongoe.
“Mwalimu, Musa alituandikia kuwa, 'Ikiwa ndugu ya mtu akifa na kumwacha mke nyuma yake, lakini hakuacha mtoto, mtu atamchukua mke wa ndugu yake, na kujipatia watoto kwa ajili ya ndugu yake.'
20 Kwai ni alongo saba, wakwanza atweti nnwawa kawaa, alei kwa bana,
Kulikuwa na ndugu saba, wa kwanza alitwaa mke na kisha akafa, hakuacha watoto.
21 Wa nya ibele kantola ni ywembe kawaa, alei kwaa bana. Na wanyaitatu iyeya.
Kisha wa pili alimchukua naye akafa, hakuacha watoto. Na wa tatu hali kadhalika.
22 Ni wasaba awile bila yakuleka bana. mwisho ywa nnwawa ni ywembe kawaa.
Na wa saba alikufa bila kuacha watoto. Mwishowe na mwanamke pia akafa.
23 Wakati wa ufufuo, kabayoka tena. Je, aba nyumbo wa nyai? Balyo alongo saba bote bai nyumbo wabe.
Wakati wa ufufuo, watakapofufuka tena, Je! Atakuwa mke wa nani? Kwani wale ndugu wote saba walikuwa waume wake.”
24 Yesu kabakokeya, “Je hii mwalo ntebosolwa, mwalo ntangike kwaa maandiko wa ngupu ya Nnongo?”
Yesu aliwaambia, “Je! Hii si sababu kuwa mmepotoshwa, kwa sababu hamjui maandiko wala nguvu za Mungu?”
25 Wakati wa kuyoka kubaa kuoma kuwaa, batola kwaa wala kuyingiya malisengele, baba kati malaika wa mbinguni.
Wakati wa kufufuka toka kwa wafu, hawataoa wala kuingia katika ndoa, bali watakuwa kama malaika wa mbinguni.
26 Kuhusu kuyoka kuoma bandu bawile, msomike kwaa kitabu sa Musa, muhabari za kichaka, Ya Nnongo akoya ni kunkokeya, Nenga Nnongo wa Abrahimu, ni Nnongo wa Isaka, ni Nnongo wa Yakobo?'
Lakini, kuhusu wafu ambao wanafufuliwa, Je! Hamkusoma kutoka katika kitabu cha Musa, katika habari za kichaka, jinsi Mungu alivyosema na kumwambia, 'Mimi ni Mungu wa Abrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo?'
27 Ywembe Nnongo kwa wa bandu bawile, bali Nnongo wa akoto. Ni kunza kunza mpotile.”
Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Ni dhahiri mmepotoka.”
28 Mwandisi yumo aisi ni kugayowa malongelo ago abweni; Yesu ayangwi bwiso. Kanlokiya “Je ni amri gani iliyo ya muhimu muno kuliko yenge?”
Mmoja wa waandishi alikuja na kuyasikia mazungumzo yao; aliona kwamba Yesu aliwajibu vema. Alimwuliza, “Je! ni amri ipi iliyo ya muhimu zaidi katika zote?”
29 Yesu kayangwa, “ya muhimu yeno, “Yekanya, Israel Nnongo witu, Bwana yumo bai.
Yesu alimjibu, “Iliyo ya muhimu ni hii, “Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu, Bwana ni mmoja.
30 Umpende Nnongo wako kwa moyo wako gote, kwa roho yako yote, kwa malango gako gote, ni kwa ngupu yako yote.'
Lazima umpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako yote, kwa roho yako yote, kwa akili yako yote, na kwa nguvu zako zote.'
31 Amri ya nyaibele yeno, “Mpende jirani kati ya uipenda ya uipenda wa mwene.” Ntopo yenge ngolo kupita yeno. `
Amri ya pili ni hii, 'Lazima umpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.' Hakuna amri nyingine kuu zaidi ya hizi.”
32 mwandishi kakoya, “bwiso mwalimu ukoya kweli kuba Nnongo yumo bai na ntopo ywenge zaidi yake.
Mwandishi akasema, “Vema Mwalimu! Umesema kweli kwamba Mungu ni mmoja, na kwamba hakuna mwingine zaidi yake.
33 Kumpenda ywembe kwa moyo gote, kwa malango gote, ni kwa ngupu zako zote ni kumpenda jirani yako kati mwene, ni muhimu kuliko mapitio ni dhabuhu za kuteketeza.
Kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama mwenyewe, ni muhimu mno kuliko matoleo na dhabihu za kuteketeza.”
34 Palyo Yesu abweni apiiye jibu la busara, kaankokeya “Wenga hauko kutalu ni upwalume wa Nnongo” kuoma hapo ntopo hata yumo annokiye Yesu swali lolote.
Wakati Yesu alipoona ametoa jibu la busara, alimwambia, “Wewe hauko mbali na ufalme wa Mungu.” Baada ya hapo hakuna hata mmoja aliye thubutu kumwuliza Yesu maswali yoyote.
35 Ni Yesu kayangwa, wakati apundisha mu hekalu, kakoya, “je, baandishi hukoya kuwa Kristo ni mwana wa Daudi?
Na Yesu alijibu, wakati alipokuwa akifundisha katika hekalu, akasema, “Je! waandishi husemaje kuwa Kristo ni mwana wa Daudi?
36 Daudi mwene muroho mtakatifu, akoiye, “Bwana akoiye kwaa bwana wango, tama kuluboko lwango lwa mmayo, mpaka niatei maadui wako kuba pae ya magolo gako.'
Daudi mwenyewe katika Roho Mtakatifu, alisema, 'Bwana alisema kwa Bwana wangu, keti katika mkono wangu wa kuume, mpaka niwafanye maadui wako kuwa chini ya miguu yako.'
37 Mwene Daudi ankema Kristo,'Bwana' Je, ni mwana wa Daudi buli? Na bandu banyansima bampekanyi kwa Pulaa.
Daudi mwenyewe humwita Kristo, 'Bwana' Je! ni mwana wa Daudi kwa jinsi gani?” Na kusanyiko kuu lilimsikiliza kwa furaha.
38 Mmayegano gake Yesu kakoya, Ntame kutalu ni aandishi bapenda alyanga ni nganzi ndaso ni kusali miano kwenye masoko.
Katika mafundisho yake Yesu alisema, “Jihadharini na waandishi, wanaotamani kutembea na kanzu ndefu na kusalimiwa kwenye masoko
39 Ni kutama mukiti sa akolo mmasinagogi na musiku kuu mwa pandu pa akolo.
na kuketi kwenye viti vya wakuu katika masinagogi na katika sikukuu kwa maeneo ya wakuu.
40 Pia balya mmisengo ya ajane ni kuyopa mayopo malaso ili bandu bababone. Bano bandu bapokya hukumu ngolo.
Pia wanakula nyumba za wajane na wanaomba maombi marefu ili watu wawaone. Hawa watu watapokea hukumu iliyo kuu.”
41 Kisha Yesu atami pae pambwega ya lisanduku la sadaka nkati ya eneo la hekalu, ai kalola bandu kabayeya pwela yabe musanduku. Matajiri bingi babei pwela ya nsima.
Kisha Yesu aliketi chini karibu na sanduku la sadaka ndani ya eneo la hekalu; alikuwa akitazama watu waliokuwa wakitia pesa zao ndani ya sanduku. Watu wengi matajiri waliweka kiasi kikubwa cha pesa.
42 Kisha nnwawa mjane nkeba kayeya ipande ibele thamani ya senti.
Kisha mwanamke mjane maskini alikuja na kutia vipande viwili, thamani ya senti.
43 Kabakema benepunzi bake ni kuakokeya, “Amini nandokubakiya yono mjane ayeyi kiasi kikolo muno ya balyo bote bapiye mulisanduku la sadaka.
Kisha akawaita wanafunzi wake na kuwaambia, “Amini nawaambia, mwanamke huyu mjane ametia kiasi kikubwa zaidi ya wote ambao wameshatoa katika sanduku la sadaka.
44 Bingi bapiiye kuoma ni ukolo wa kipato sabe. Lakini yonooo nnwawa mjane, kuoma ni ukeba wake ayeyi pwela yote ya utumi mmaisha gake.'
Kwani wote wametoa kutokana na wingi wa mapato yao. Lakini mwanamke mjane huyu, kutoka katika umaskini wake, katia pesa yote ambayo alipaswa kuitumia kwa maisha yake.”

< Marko 12 >