< Luka 19 >

1 Yesu atijingya ni peta katikati ya Yeriko.
Yesu aliingia na kupita katikati ya Yeriko.
2 Napo pabile ni mundu yumo akemelwa Zakayo, ywembe abile nkolo wa watoza ushuru kae mundu tajiri.
Na hapo palikuwa na mtu mmoja aitwaye Zakayo. Ambaye alikuwa mkuu wa watoza ushuru tena mtu tajiri.
3 Abile kapaya kubona Yesu ni mundu wa namna gani, lakini awezite kwaa kum'bona kwasababu ya bandu banyanisima, kwa kuwa abile mwipi wa kimo.
Alikuwa anajaribu kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, lakini hakuweza kuona kwa sababu ya umati wa watu, kwa kuwa alikuwa mfupi wa kimo.
4 Nga nyo, atilongoliya lubelo nnonge ya bandu, anaoboka kunanin ya mkuyu lenga aweche kum'bona, kwasababu Yesu atikaribiya pita kundela yelo.
Hivyo, alitangulia mbio mbele za watu, akapanda juu ya mkuyu ili aweze kumwona, kwa sababu Yesu alikaribia kupita njia hiyo.
5 Wakati Yesu paikite mahali palo, atilinga kunani ni kum'bakiya, Zakayo, uluka upesi, maana leno ni lachima shinda kunyumba yako!
Wakati Yesu alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwambia, 'Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazima nishinde nyumbani mwako.'
6 Apangite haraka, uluka ni kumkaribisha kwa puraha.
Akafanya haraka, akashuka na kumkaribisha kwa furaha.
7 Bandu boti pababweni galo, batilalamika, nabaya,'Ayei kutembelia mundu mwene sambi.'
Watu wote walipoona hayo, wakalalamika, wakisema, 'Amekwenda kumtembelea mtu mwenye dhambi.'
8 Zakayo atiyema nakum'bakiya Ngwana, lola Ngwana nusu ya mali yango nibapeya maskini, ni ikiwa nimpokonyite mundu yeyoti kilebe, mnakumkeboliya mara ncheche.'
Zakayo akasimama akamwambia Bwana, Tazama Bwana nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimemnyang'anya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne. '
9 Yesu atikum'bakiya,'leno wokovu uikite katika nyumba yeno, kwa sababu yembe ni mwana wa Ibrahimu.
Yesu akamwambia, 'Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa sababu yeye pia ni mwana wa Ibrahimu.
10 Kwa maana mwana wa mundu aichile pala ni lopwa bandu babaobite.'
Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa watu waliopotea. '
11 Pabayowine aga, atiyendeliya longela ni piya mfano, kwa sababu abii papii ni Yerusalemu anabo batangite ya kuwa ufalme wa nnonge wabile papipi na bonekana mara jimo.
Waliposikia hayo, aliendelea kuongea na alitoa mfano, kwa sababu alikuwa karibu na Yerusalemu, na wao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu ulikuwa karibu kuonekana mara moja.
12 Nga atikuwabakiya,'afisa yumo atiyenda kukilambo chakulipite lenga pokiya ufalme ni boka po buya.
Hivyo akawaambia, 'Ofisa mmoja alikwenda nchi ya mbali ili apokee ufalme na kisha aurudi.
13 Atikubakema atumishi bake komi, nakubapeya mafungu komi, nakuabakiya, mukapangie biashara mpaka panibuya!
Aliwaita watumishi wake kumi, akawapa mafungu kumi, akawaambia, 'fanyeni biashara mpaka nitakaporudi.'
14 Lakini bananchi bake batikasirika ni kwa nyoo batilagiya ajumbe bayende, kumkengama ni buya,'atakiwa kwaa mundu yono kututawala,'
Lakini wananchi wake walimchukia na hivyo wakatuma wajumbe waende kumfuata na kusema, 'Hatutaki mtu huyu atutawale.'
15 Pabile pabuite kaya baada ya pangilwa mpwalme, atiamuru balo atumishi abapeile mbanje bakemelwa kwake, apate tanga faida gani yabaipatike kwa panga biashara.
Ikawa aliporudi nyumbani baada ya kufanywa mfalme, akaamuru wale watumishi aliokuwa amewaachia fedha waitwe kwake, apate kujua faida gani waliyoipata kwa kufanya biashara.
16 Wa kwanza aichile, nabaya, Ngwana, fungu lyako lipangite mafungu komi zaidi,
Wa kwanza akaja, akasema, `Bwana, fungu lako limefanya mafungu kumi zaidi. '
17 Yolo afisa atikum'bakiya, vema, wa mmanda mwema, kwasababu wabile mwaminifu katika kikowe kichunu, upala panga ni madaraka kunani ya miji komi.'
Huyo Ofisa akamwambia, Vema, mtumishi mwema. Kwa sababu ulikuwa mwaminifu katika jambo dogo, utakuwa na madaraka juu ya miji kumi. '
18 Wa na ibele, abaite, Ngwana, fungu lyako lipangite mafungu matano.'
Wa pili akaja, akasema, 'Bwana, fungu lako limefanya mafungu matano.'
19 yolo afisa atikumbakiya,'tola mamlaka ga kunani ya miji itano.'
Huyo Afisa akamwambia, 'Chukua mamlaka juu ya miji mitano.'
20 Ni ywenge aichile, ni baya,'Ngwana yeno pano, banje yako, naibekite salama katika kitambala.
Na mwingine akaja, akasema, `Bwana hii hapa fedha yako, ambayo niliihifadhi salama katika kitambaa,
21 kwa maana natiyogopa kwa sababu, wenga nga mundu nkale, undaboya chelo cha ukibekite ni una chaupandike kwaa.'
kwa maana niliogopa kwa sababu wewe ni mtu mkali. Unaondoa kile usichokiweka na kuvuna usichopanda. '
22 hayo afisa atikum'bakiya, kwa maneno yako mwene, nipala kumhukumu, ewe mtumishi mbaya, watangite nenga na mundu nkale, nitola chani bekite kwaa ni una chanipandike kwaa.
Huyo Ofisa akamwambia, 'Kwa maneno yako mwenyewe, nitakuhukumu, ewe mtumishi mbaya. Ulijua kwamba mimi ni mtu mkali, nachukua nisichokiweka na kuvuna ambacho sikupanda.
23 Bai mbona wabekite kwaa mbanje yango katika benki, lenga paniboya nitole pamope ni faida?
Basi, mbona hukuweka fedha yangu katika benki, ili nikirudi niichukue pamoja na faida?
24 Afisa atikubabakiya bandu bababile batiyema hapo,'munyang, anye alyo lifungu ni kumpeya yolo mwene mafungu komi.
Ofisa akawaambia watu waliokuwa wamesimama hapo, 'Mnyang'anyeni hilo fungu na kumpa yule mwenye mafungu kumi.'
25 Bakam'bakiya,'Ngwana, yembe abi na mafungu komi.'
Wakamwambia, `Bwana, yeye ana mafungu kumi. '
26 Nindakuwabakiya kila mundu ywabile nacho apala peilwa zaidi, lakini ntopo, hata kiche kilebe abile nacho kipala tolekwa.
'Nawaambia, kila mtu ambaye anacho atapewa zaidi, lakini ambaye hana, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
27 Lakini aba maadui bango, babakani nipange mpwalume wabe, baletwe pano ni kuba bulaga nnonge yango.”
Lakini hawa maadui zangu, ambao hawakutaka niwe Mfalme wao, waleteni hapa na kuwaua mbele yangu. ''
28 Baada ya baya gano, atiyendeleya nnonge panda yenda Yerusalemu.
Baada ya kusema hayo, aliendelea mbele akipanda kwenda Yerusalemu.
29 Pabile pakaribie Bethfage ni Bethania, papipi ni kitombe cha mizeituni, atikubatuma anapunzi bake abele,
Ikawa alipokaribia Bethfage na Bethania, karibu na mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili,
30 Atibaya,'Muyende katika ijiji ya jirani, pamujingya, mpala kumkoliya mwana mbunda anapandilwa kwaa balo, muyogoli, mumleti kwango.
akisema: `Nendeni katika kijiji cha jirani. Mkiingia, mtakuta mwana-punda hajapandwa bado. Mfungueni, mkamlete kwangu.
31 Kati mundu abalokiye, “Mbona mundakumyogoliya” mubaye, “Ngwana andakumpala”.
Kama mtu akiwauliza, `Mbona mnamfungua? ' Semeni, “Bwana anamhitaji. ''
32 Balo babalagilwe batiyenda nakum'bona mwana mbonda kati Yesu chabakiye.
Wale waliotumwa wakaenda wakamwona mwana-punda kama Yesu alivyokuwa amewaambia.
33 Babile banda kumyogoliya mwana mbonda wamiliki baka wabakiya,'kitumbwe namani munda kumyogoliya mwana mbunda yono?
Walipokuwa wanamfungua mwana punda wamiliki wakawaambia, 'Kwa nini mnamfungua mwana punda huyu?'
34 Batibaya, “Ngwana andakumpala.”
Wakasema, `Bwana anamhitaji. '
35 Bai, batikumpelekia Yesu, batikumtandika ngobo yabe kunani ya mwana mbonda ni bakamoboya Yesu kunani yake.
Basi, wakampelekea Yesu, wakatandika nguo zao juu ya mwana punda na wakampandisha Yesu juu yake.
36 Pabile kayenda bandu batitandza mavazi yabe mundela.
Alipokuwa akienda watu wakatandaza mavazi yao barabarani.
37 Pabile anatelemka pakitombe sa mizeituni, jumuiya yoti ya benepunzi bake batumbwile shangiliya ni kumtukuza Nnongo kwa lilobe likolo, kwa sababu ya makowe makolo bayabweni.
Alipokuwa anateremka mlima wa Mizeituni, jumuiya yote ya wanafunzi wakaanza kushangilia na kumtukuza Mungu kwa sauti kubwa, kwa sababu ya mambo makuu waliyoyaona,
38 Batibaya, “nga yembe mbarikiwa mpwalume yaichile kwa lina Ngwana! Amani kumaunde, ni utukufu kunani!'
wakisema, 'Ndiye mbarikiwa Mfalme ajaye kwa jina la Bwana! Amani mbinguni, na utukufu juu!'
39 Baadhi ya Mafarisayo katika makutano batikum'bakiya, mwalimu, ubanyamazishe benepunzi bako.
Baadhi ya Mafarisayo katika mkutano wakamwambia, Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako. '
40 Yesu kayangwa ni kubaya, “nindakuwabakiya, kati haba batituliya, maliwe yapala kombwa malobe.'
Yesu akajibu, akasema, `Nawaambieni, kama hawa wakinyamaza, mawe yatapaza sauti. '
41 Yesu paaukaribiye mji atiuleliya.
Yesu alipoukaribia mji aliulilia,
42 Atibaya, “Laiti mwatangite hata wenga, katika lichoba lino makowe gagaleta amani! lakini nambeambe yatiya mminyo pako.
akisema, laiti ungelijua hata wewe, katika siku hii mambo ambayo yanayokuletea amani! Lakini sasa yamefichika machoni pako.
43 Kwa kuwa lichoba lindaicha ambapo adui bako apala chenga boma papipi ni wenga, ni kukutindiya ni kukukandamiza boka kila upande.
Kwa kuwa siku zinakuja ambapo adui zako watajenga boma karibu na wewe, na kukuzunguka na kukukandamiza kutoka kila upande.
44 Bapala kutomboya pae wenga na bana bako. bapala kukuleka kwaa hata liwe limo kunani ya jenge, kwa sababu upala tambwa kwaa wakati Nnongo pabile kapaya kukulopwa!'
Watakuangusha chini wewe na watoto wako. Hawatakuachia hata jiwe moja juu ya jingine, kwa sababu haukutambua wakati Mungu alipokuwa anajaribu kukuokoa'.
45 Yesu ajingile muhekalu, atumbwi kuwabenganga balo babile bakipemeya,
Yesu aliingia Hekaluni, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza,
46 Atikuwabakiya, “Itiandikwa, nyumba yango ipala panga numba ya sala, lakini mwenga muipangite kuwa likolo lya anyang'anyi.'
akiwaambia, “Imeandikwa, 'Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala,' lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi”.
47 Kwa nyoo, Yesu abile atipundisha kila lichoba muhekalu, Makuhani akolo ni Alimu ba saliya ni iongozi ba bandu bapalite kumuhukumu.
Kwa hiyo, Yesu alikuwa akifundisha kila siku hekaluni. Makuhani wakuu na walimu wa Sheria na viongozi wa watu walitaka kumuua,
48 Lakini wawezite kwaa pata ndela ya panga nyoo, kwa sababu bandu boti babile bakimpekaniya kwa makini.
lakini hawakuweza kupata njia ya kufanya hivyo, kwa sababu watu wote walikuwa wakimsikiliza kwa makini.

< Luka 19 >