< Luka 12 >

1 Kwa wakati wo maelfu ganambone gabandu balikusangika pamoja kiasi cha tumbwa libatana atumbwi bayana banafunzi bake muhidhali na chachu ya mafarisayo ambayo nga unafiki.
Kwa wakati huo, maelfu mengi ya watu walikusanyika pamoja, kiasi cha kuanza kukanyagana, akaanza kusema na wanafunzi wake kwanza, “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo ambayo ni unafiki”
2 Na pabali na siri yai iyilwe ambayo ya umukulilwalii wala jambo laliiyilwe ambalo latangani kwali.
Na hapatakuwepo na siri iliyofichika ambayo haitafunuliwa, wala jambo lililofichwa ambalo halitajulikana.
3 Na lyolyoi laumbayit palibindu layanika pabwega. Na gogota gamubajite munachikilo nkati ya yumba yinu ya nkati yamuyigile gatangazwa panani ya nyumba.
Na lolote mlilolisema katika giza, litasikiwa katika mwanga. Na yoyote mliyoyasema kwenye sikio ndani ya vyumba vyenu vya ndani vilivyofungwa yatatangazwa juu ya paa la nyumba.
4 Nenda kuabakia mabwiga lyangu kana mwayoghope balu bababulagayiga na mtupu kile chingi chabakipanga.
Nawaambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili na kisha hawana kitu kingine cha kufanya,
5 Lakini ni palakuabula ywakunyogopa. mungogope yulu ambaye baada ya bulaga aina ngupu ya kukutailya jehanamu elo nendakuabakia mwenga munyogopenywo. (Geenna g1067)
Lakini nitawaonya mtakaye mwogopa. Mwogopeni yule ambaye baada ya kuwa ameua, ana mamlaka ya kutupa jehanamu. Ndiyo, nawaambiani ninyi, mwogopeni huyo. (Geenna g1067)
6 Je shomoro batano bapimiali shilingi ibele? hata ivyo mtupu hata yamo ywabapala kumbalya mbele ya Nnongu.
Je shomoro watano hawauzwi kwa sarafu mbili? hata hivyo hakuna hata mmoja wao atakayesahaulika mbele za Mungu.
7 Lakini mtange kuwa nywili ya mumitwee yinu itibalangwilwa kana muyogope. mwenga muina thamani ngulu kuliko shomoro baingi.
Lakini mjue kuwa, nywele za vichwa vyenu vimehesabiwa. Msiogope. Ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi.
8 Ninda kuabakia, ywaniyikitiya nenga nninge ya bandu, mwana wa Adamu anyiyikitya nnonge ya malaika na Nnongo.
Ninawaambia, yeyote atakayenikiri Mimi mbele za watu, Mwana wa Adamu atamkiri mbele za malaika wa Mungu.
9 Lakini ywoywoti ywanikana nnonge ya bandu ni ywembe akanikiya nnongi ya malaika ba Nnongo.
Lakini yeyeyote atakayenikana mbele za watu naye atakanwa mbele ya Malaika wa Mungu.
10 Ywoywoti nywabaya lineno kunani ya mwana wa Adamu, asamehelwa, lakini ywoywoti ywa mkufuru Roho mpeletau, asamehelwa kwaa,
Yeyote atakayesema neno baya juu ya Mwana wa Adamu, atasamehewa, lakini yeyote atakayemkufuru Roho Mtakatifu, hatasamehewa.
11 Bapampeleka nnongi ya wakolo ba masinagogi, atawala, ni bene mamlka, kana muyogope husu namna ya longela katika kuitetea au kile cha baya,
Watakapowapeleka mbele za wakuu wa masinagogi, watawala, na wanye mamlaka, msiogope juu na namna ya kuongea katika kujitetea au nini mtakachosema,
12 Kwa kuwa Roho Mpeletau ampundisha namani mwampala baya kwa wakati woo,”
kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha namna mtakavyosema kwa wakati huo.”
13 Mundu yumo katika likusanyiko ammakiye, mwalimu, umakiye nnunangu ampei sehemu ya urithi wango,”
Mtu mmoja katika kusanyiko akamwambia, “Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie sehemu ya uruthi wangu.”
14 Yesu an'yangwi, ni nyai ywa nibikite panga namwamuzi ni wanipatanisha kati yinu?
Yesu akamjibu, ni nani aliye niweka kuwa mwamuzi na mpatanishi kati yenu?
15 Nga aabakiya, muiadhari ni kila namna ya tamaa, kwa sababu ukto wa mundu ubile kwaa katika wingwa ilibe yabile nayo.”
Ndipo akawaambia, Jihadharini na kila namna ya tamaa, kwa sababu uzima wa mtu hauko katika wingi wa vitu alivyo navyo.”
16 Yesu aabakiye mfano, kabaya, nng'unda wa mundu yumo tajiri yatipambika muno.
Yesu akawaambia mfano, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilizaa sana,
17 ni atikuilokiya nkati yake, kabaya, mbange namani kwani ntopo mahali pabika yakya yango?
na akajiuliza ndani yake, akisema, nitafanyaje kwani sina mahali pa kuhifadhi mazao yangu?
18 Ngabaya mbapanga nyaa, mbatekwana magolo gango machunu ni chenga balibile likolo ni kuibika yakulya yango yoti ni ile yenge.
Akasema, nitafanya hivi. Nitavunja ghala zangu ndogo na kujenga iliyo kubwa, na kuyahifadhi mazao yangu yote na vitu vingine.
19 Naibakiya nafsi yango, “Nafsi, uibekii akii ya ile yanambone kwa miaka yanambone upumuli, ulye, unywee ni ustalee.”
Nitaiambia nafsi yangu, “Nafsi, umejiwekea akiba ya vitu vingi kwa miaka mingi. Pumzika, ule, unywe na kustarehe.”
20 Lakini Nongo ammakiye, wenga mundu mpumbavu, kiloo cha lino tupala mwoyo buka kwako, ni ilee yoti yaniandaite yapanga ya nyai?
Lakini Mungu akamwambia, ewe mtu mpumbavu, usiku wa leo wanahitaji roho kutoka kwako, na vitu vyote ulivyoviandaa vitakuwa vya nini?
21 Nga yapanga kwa kila mundu ywa ibekya mali ni kuitayalisha kwaajili ya Ngwana.
Ndivyo itakavyokuwa kwa kila mtu anayejiwekea mali na si kujitajirisha kwa ajili ya Bwana.
22 Yesu aabakiye benepuzi bake, kwa nyo nenda kuwabakiya kana muyogope husu maisha yinu ya kwale mwa lyaa namani au husu yega yinu mwa wala namani.
Yesu akawaambia wanafunzi wake, Kwa hiyo nawaambia msihofu juu ya maisha yenu ya kuwa mtakula nini au juu ya miili yenu ya kuwa mtavaa nini
23 kwa kuwa maisha nga muno kuliko chakulya, ni yega muno kuliko ngobo.
Kwa kuwa maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi.
24 Muilinge iyuni ya angani, balima kwaa wala bauna kwaa. Ntopo chumba wa lighulo lya bikya, lakini Tati bitu anda kuwaleleya mwenga bora kwaa kuliko iyuni!
Angalieni ndege wa angani, hawalimi wala hawavuni. Hawana chumba wala ghala ya kuhifadhia, lakini Baba yenu huwalisha. Ninyi si bora zaidi kuliko ndege!
25 Ywako nkati yinu ambaye ywaisumbua awesa yongeya dhiraa imo katika maisha gake?
Ni yupi kati yenu ambaye akijisumbua ataweza kuongeza dhiraa moja katika maisha yake?
26 Mana basi mngwecha kwaa panga hacho kichunu chakibile rahisi kwa namani kuisumbwa hago genge?
Ikiwa basi hamuwezi kufanya hicho kitu kidogo kilicho rahisi kwa nini basi kusumbukia hayo mengine?
27 Mugalinge maluba mwagakula. Gapanga kwaa kazi wala gapota kwaa. Lakini nenda kuwabakia hata Suleimani katika utukufu bake boti ban'gwalike kwaa kati yimo yapo haga.
Angalieni maua -yanavyomea. Hayafanyi kazi wala hayasokoti. Lakini nawaambia, hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama mojawapo ya haya,
28 Mana Nnongo ugawalika vizuri maakapi ga mmendi, ambago leno gabile, ni malau ugataikwa pa mwoto. Buli mwenga muno kwaa aweza kun'gwalika? mwenga imani njunu!
Kama Mungu huyavika vizuri majani ya kondeni, ambayo leo yapo, na kesho hutupwa kwenye moto. Je si zaidi atawavika ninyi? enyi wa imani haba!
29 Kana msumbukii husu mwa lyaa namani au mwa nywa namani wala kana m'be ni hofu.
Msisumbukie juu ya kuwa mtakula nini au mtakunywa nini, wala msiwe na hofu.
30 Kwa kuwa mataifa goti ga kilambo basumbukiya mambo gabe. Ni Tati binu atangite kuwa mpala ago.
Kwa kuwa Mataifa yote ya dunia husumbukia mambao yao. Na Baba yenu anajua ya kuwa mnahitaji hayo.
31 Lakini muupale ufalme wake kwanza, ni ago genge anyongekeya.
Lakini tafuteni ufalme wake kwanza, na hayo mengine mtazidishiwa,
32 Kana muyogope mwenge mwa likundi lichini kwasababu Tati binu apulaikya kwapea ufalme.
msiogope, enyi kundi dogo, kwa sababu Baba yenu anafurahia kuwapa ninyi huo ufalme.
33 Mupimeye mali yinu mukaapeiimaskini, muhipangii mifuko yangali yomoka hazina ya kunani yanga yomoka, sehemu ambayo baii bakalibia kwaa wala nondo aweza kwaa alibu.
Uzeni mali zenu na mkawape maskini, mjifanyie mifuko isiyoishiwa hazina ya mbinguni isiyokoma, sehemu ambapo wezi hawatakaribia wala nondo haitaweza kuharibu.
34 Kwa kuwa paibile hazina yako, nga mwoyo wako paupabaa.
Kwa kuwa palipo na hazina yako, ndipo na roho yako itakapokuwepo.
35 Ngobo yinu ndachi ibe itabilwe kwa nkanda, ni taa yinu muhakikishe kuwa kaiyendelya yakaa.
Nguo zenu ndefu ziwe zimefungwa kwa mkanda, na taa zenu zihakikishwe kuwa zinaendelee kuwaka,
36 ni m'be kati bandu babannolekea Ngwana wabe buka kusheree ya ndoa, linga mana aichile ni kumbwa ulibawecha kunyughulya nniyango kwa haraka.
na muwe kama watu wanaomtazamia Bwana wao kutoka kwenye sherehe ya harusi, ili kwamba akija na kupiga hodi, wataweze kumfungulia mlango kwa haraka.
37 Batibarikiwa balu atumishi ambao Ngwana aakolya bai minyo. Hakika atabaa ngobo yake ndacho kwa nkanda alafuatawika pae kwa chakulya, ni kubahudumia.
Wamebarikiwa wale watumishi, ambao Bwana atawakuta wako macho. Hakika atafunga nguo yake ndefu kwa mkanda, kisha atawaketisha chini kwa chakula, na kisha kuwahudumia.
38 Kati Ngwana aaicha kwa zamu yeneibele ya lindela lya kilo, au hata zamu yene itatu ya lindela, ni kunkolya wabiile tayari, yabaa heri kwa abo atumishi.
Kama Bwana atakuja kwa zamu ya pili ya ulinzi ya usiku, au hata zamu ya tatu ya ulinzi, na kuwakuta wakiwa tayari, itakuwa ni heri kwa hao watumishi.
39 zaidi ya ago mutange linga, kati ngwana mwene nyumba akatangage saa ambayo mwii andaicha, apeilekali nyumba yake tekwana.
Zaidi ya hayo, mjue hili, kama bwana mwenye nyumba angelijua saa ambayo mwivi anakuja, asingeliruhusu nyumba yake ifunjwe.
40 Mube tayari kai kwani mutangite kwaa ni wakati gani mwana wa Adamu abuyangana.
Iweni tayari pia kwani hamjui ni wakati gani mwana wa Adamu atarudi.
41 Petro abayite, “Ngwana, utubakia twenga mfano yii, au umakiya kila mundu?
Petro akasema, “Bwana, watuambia sisi wenyewe hii mifano, au unamwambia kila mtu?
42 Ngwana amm'bakiye, nyai mwanda mwaminifu au mwene hekima ambaye ngwana wake amika panani ya abanda benge lenga abagane chakulya chabe kwa wakati wapalikwa?
Bwana akawaambia, “Ni nani mtumwa mwaminifu au mwenye hekima ambaye bwana wake atamweka juu ya watumishi wengine, ili awagawie chakula chao kwa wakati mwafaka?
43 Atibarikiwa mmanda yolo ambaye bwana wake mana aichile ukolya kapanga galo ganagile.
Amebarikiwa mtumishi yule, ambaye bwana wake akija atamkuta akifanya yale aliyoagizwa.
44 Hakika nindakuwabakiya mwenga ya kuwa ami'ka manani ya mali yake yoti.
Hakika nawaambia ninyi ya kuwa atamweka juu ya mali yake yote.
45 Lakini mmanda yolo mana abayite pa mwoyo wake,'bwana wango achia buya, nga nyoo ngatumbwa kuangumbwa abanda alalume ni alwawa alafu atumbwa lyaa, nywaa ni lobya.
Lakini Mtumishi yule akisema moyoni mwake, “bwana wangu anachelewa kurudi; hivyo akaanza kuwapiga wale watumishi wa kiume na wa kike, kisha akaanza kula, kunywa na kulewa,
46 Bwana wake yolo mmanda aicha katika lichuba yanga kwaa kuitegemea ni lisaa langa kwaa kulitanga, ywembe ankata ipande ipande ni kummeka katika sehemu imo ni banga kwaa aaminifu.'
bwana wake yule mtumwa atakuja katika siku asiyotegemea na saa asiyoijua, naye atamkata vipande vipande na kumuweka katika sehemu pamoja na wasiokuwawaaminifu'
47 Mmanda ywa yowa mapenzi ga bwana wake, aindaite kwaa wala apangite sawa sawa ni penda kwake, akumbulwa iboko iingi.
Mtumishi, anayejua mapenzi ya bwana wake, naye hakujiandaaa wala hakufanya sawa sawa na mapenzi yake, atapigwa viboko vingi.
48 Lakini mmanda ywa tangite kwaa mwapendi bwana wake, lakini apangite gagapalikwa adhabu, angumbulwa iboko njunu. kwa kuwa ywembe ywa peilwe yanambone, apalongelwa buka kwake ni ywembe ywaaminilwe kwa yanambone, kwake alongelwa yanambone muno.
Lakini mtumishi asiyejua mapenzi ya bwana wake, lakini akafanya yanayostahili adhabu, atapigwa viboko vichache. Kwa kuwa yeye aliyepewa vingi, vingi hudaiwa kutoka kwake, na yeye aliyeaminiwa kwa vingi, kwake vitadaiwa vingi zaidi.
49 Niichile koya mwoto mukilambo ni nenda tamaniya ibe inda yaka,
Nimekuja kuwasha moto duniani, na natamani iwe umekwishawaka,
50 Lakini nina ubatizo ambao mbabatizwa, ni nina kyoto mpaka paukamilika.
Lakini nina ubatizo ambao nitabatizwa, na nina huzuni mpaka utkapokamilika!
51 Buli mufikilia kuwa niichi leta amani mukilambo? Nyoli, ninda kuwabakiya, badala yake niletite mutalanganike.
Je mnafikiri kuwa nimekuja kuleta amani duniani? Hapana, Nawaambieni, badala yake nimeleta mgawanyiko.
52 Tangu nambeambe ni yendelya paba, ni bandu batano. Katika nyumba yimo babaganike, ni atatu kinyume ni abele abele bapanga kinyume ni atatu.
Tangu sasa na kuendelea kutakuwa na watu watano katika nyumba moja wamegawanyika, na watatu watakuwa kinyume na wawili, na wawili watakuwa kinyume na watatu.
53 Babaganika, tati apanga kinyume ni mwana wake, ni mwana ni mwana apanga kinyume ni tate bake, Mao apanga kinyume ni mwana wake, ni mwana apanga kinyume ni mabake, mwile apanga kinyume ni mkwano, ni mkwano apanga kinyume ni mabake.
Watagawanyika, baba atakuwa kinyume na mwanae, na mwanae atakuwa kinyume na babaye, mama atakuwa kinyume na binti yake, na binti atakuwa kinyume na mama yake, Mama mkwe atakuwa kinyume na mkwe wake naye mkwe atakuwa kinyume na mama mkwe wake.
54 Yesu ende kuabakia makutano kae, pa mona maunde kugapita kundondi, mwaya wakati wa ula wandaicha, ni nga chai bile.
Yesu akawa anawaambia makutano pia, “Mara muonapo mawingu yakitokea magharibi, mnasema nyakati za mvua zimewadia; na ndivyo inavyo kuwa,
55 Ni mchunga wa kusimana uvumilite mmaya paba ni lyoto likali, ni nga chai baa.
Na upepo wa kusini ukivuma, mnasema, Patakuwepo na joto kali, na ndivyo inavyokuwa.
56 Mwenga mwa lau, muweza tafsiri mmoneka wa kilambo ni kunani, lakini iba buli nngwecha kwaa tafsiri wakati waubile?
Enyi wanafiki, mnaweza kutafsiri mwonekano wa nchi na anga, lakini inakuwaje hamuwezi kuutafsiri wakati uliopo?
57 Ni kwa namani kila yumo kana alipambanue lali la kweli kwake kulipanga wakati pa bi ni nafsi ya panga nyo?
Ni kwa nini kila mmoja wenu asipambanue lililo sahihi kwake kulifanya wakati ambapo angali na nafasi ya kufanya hivyo?
58 Maana mana uyihi ni ywakushitakiya nnongi ya hakimu, uitahidi patana na ywa kushitakya mungali balo mundela kana akupeleke kwa hakimu, ni hakimu akupeleki kwa afisa akutaikwa muligereza.
Maana mkienda na mshitaki wako mbele ya hakimu, jitahidi kupatana na mshitaki wako mungali bado mko njiani asije akakupeleka kwa hakimu, na hakimu akupeleka kwa ofisa, na ofisa akakutupa gerezani.
59 Ninda kuwabakiya wapita mwo adi ulepite mpaka lusenti lwa mwisho.
Nakuambia, hutatoka huko hadi umelipa mpaka senti ya mwisho.

< Luka 12 >