< Yohana 7 >

1 Na baada ya makowe aga Yesu atisafiri mu'Galilaya, kwa sababu apendile kwaa kuyenda Uyahudi kwa sababu Bayahudi babile bakipanga mipango ya kummulaga.
Na baada ya mambo haya Yesu alisafiri hivi katika Galilaya, kwa sababu hakupenda kwenda Uyahudi kwa sababu wayahudi walikuwa wakifanya mipango ya kumwua.
2 Nambeambe sikukuu ya Ayahudi, sikukuu ya vibanda, yabile papipi.
Sasa sikukuu ya Wayahudi, sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu.
3 Nga alongo bake batikummakiya, “Uboke pandu hapa uyende Uyahudi, ili kwamba anapunzi bako nyonyonyo bayabone makowe uyapangayo.
Ndipo ndugu zake walipomwambia, “Ondoka mahali hapa uende Uyahudi, ili kwamba wanafunzi wako vile vile wayaone matendo ufanyayo.
4 Ntopo ywapanga lolote kwa siri iwapo ywembe mwene apala kutangikana wazi. Iwapo upanga makowe aga, ujibonekeye wamwene kwa ulimwengu.”
Hakuna afanyaye lolote kwa siri iwapo yeye mwenyewe anataka kujulikana wazi. Iwapo unafanya mambo haya, jionyeshe mwenyewe kwa ulimwengu.”
5 Hata nnongo bake bamwaminiye kwaa.
Hata ndugu zake pia hawakumwamini.
6 Nga Yesu kammakiya, “Muda wango uikite kwaa bado, lakini muda winu kila mana ubile tayari.
Ndipo Yesu alipowaambia, “Wakati wangu haujafika bado, lakini wakati wenu kila mara uko tayari.
7 Ulimwengu waweza kwaa kubachukiya mwenga, ila wanichukiya nenga kwa kuwa niashuhudia kuwa makowe gake ni mabou.
Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, bali unanichukia mimi kwa sababu ninaushuhudia kuwa matendo yake ni maovu.
8 Mubokange kuyenda mu'sikukuu: nenga niyenda kwaa mu'sikukuu yee kwa sababu muda wangu ukamilika bado.”
Pandeni kwenda katika sikukuu; mimi siendi katika sikukuu hii kwa sababu muda wangu haujakamilika bado.”
9 Baada ya kulongela makowe ago kwabe, atami Galilaya.
Baada ya kusema mambo hayo kwao, alibaki Galilaya.
10 Hata nyoo, nongo bake pababile mu'sikukuu, nga ni ywembe atiyenda, sio kwa wazi bali kwa siri.
Hata hivyo, ndugu zake walipokuwa wamekwenda katika sikukuu, ndipo naye alienda, siyo kwa wazi bali kwa siri.
11 Ayahudi pabile pakimpala mu'sikukuu no baya, “Abile kwaako?”
Wayahudi walikuwa wakimtafuta katika sikukuu na kusema, “Yuko wapi?”
12 Pabile ni malongelo ganyansima nkati ya makutano nnani yake. Benge batibaya, “Ni mundu mwema,” Benge babayite, “Hapana, uwapotosha bandu.”
Kulikuwa na majadiliano mengi miongoni mwa makutano juu yake. Wengine walisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walisema, “Hapana, huwapotosha makutano.”
13 Hata nyoo ntopo ywalongela wazi nnani yake kwa kuwaogopa Ayahudi.
Hata hivyo hakuna aliyezungumza wazi juu yake kwa kuwaogopa Wayahudi.
14 Muda wa sikukuu waikite katikati, Yesu kayenda mu'hekalu ni kuanza kupundisha.
Wakati sikukuu ilipofika katikati, Yesu alipanda kwenda Hekaluni na kuanza kufundisha.
15 Ayahudi babile batishangala no kubaya, “Kwa jinsi yanamani mundu yee ayatangite makowe ganyansima? Asoma kwaa kamwe.”
Wayahudi walikuwa wakishangaa na kusema, “Kwa jinsi gani mtu huyu anajua mambo mengi? Hajasoma kamwe.”
16 Yesu kabayangwa ni kuamakiya, “Mapundisho gango nga yango kwaa, ila ni ya yolo ywanitumile.
Yesu akawajibu na kuwaambia, “Mafundisho yangu siyo yangu, bali ni yake yeye aliyenituma.
17 Iwapo yeyote ywapenda panga mapenzi gake ywembe, atangite kuhusu mapundisho aga, kati yatiboka kwa Nnongo, au kati nialongela kuoma kwango mwene.
Iwapo yeyote atapenda kufanya mapenzi yake yeye, atajua kuhusu mafundisho haya, kama yanatoka kwa Mungu, au kama ninazungumza kutoka kwangu mwenyewe.
18 Kila ywalongela yaboite kwake mwene upala utukufu wake, ila kila yaa aupala utukufu wake ywembe ywamtumile, mundu yoo nga wa kweli, ni nkati yake ntopo kutenda ubou.
Kila anayezungumza yatokayo kwake mwenywe hutafuta utukufu wake, bali kila atafutaye utukufu wake yeye aliyemtuma, mtu huyo ni wa kweli, na ndani yake hakuna kutotenda haki.
19 Musa awapeile kwaa mwenga saliya? Lakini ntopo hata yumo nkati yinu ywaipangite saliya. Mwanja namani mwapala kunibualaga?
Musa hakuwapa nyinyi sheria? Lakini hakuna hata mmoja kati yenu atendaye sheria. Kwa nini mnataka kuniua?
20 Bandu kabannyangwa, “Ubile ni nchela, nyai ywapala kukubulaga?
Makutano wakajibu, “Una pepo. Nani anataka kukuua?”
21 Yesu kayangwa ni kuamakiya, nipangite kazi yimo, ni mwenga mwabote mwatishangala kwa sababu ya yelo kazi.
Yesu akajibu na akawaambia, “Nimetenda kazi moja, nanyi nyote mmeshangazwa kwa sababu yake.
22 Musa atikuwapea mwenga tohara (iboite kwaa boka kwa Musa, ila yelo yaboite kwa tate), ni nkati ya Sabato mwastahili mundu.
Musa aliwapa tohara (siyo kwamba inatoka kwa Musa, bali ile inatoka kwa mababa), na katika Sabato mnamtahili mtu.
23 Mana abile mundu ywapokya tohara mu'siku ya Sabato ili saliya ya Musa itekwanike, kwa mwanja namani mwanikasirikya nenga kwa sababu nimpangite mundu kuwa nkoto kabisa mu'sabato?
Iwapo mtu atapokea tohara katika siku ya Sabato ili kwamba sheria ya Musa isivunjwe, kwa nini mnanikasirikia mimi kwa sababu nimemfanya mtu kuwa mzima kabisa katika Sabato?
24 Kana mhukumu lengana na mwonekano, ila muhukumu kwa haki.
Msihukumu kulingana na mwonekano, bali hukumuni kwa haki.
25 Baadhi yabe baboka Yerusalemu kababaya, “Yolo kwaaa wampala kummulaga?
Baadhi yao kutoka Yerusalemu wakasema, “Siye huyu wanayemtafuta kumwua?
26 No linga, alongela waziwazi, nga balongela kwaa chochote nnani yake. Iwezekana kwaa ibile kwamba atawala batangite kweli kuwa ayoo nga Kristo, yawezana batangite?
Na tazama, anaongea wazi wazi, na hawasemi chochote juu yake. Haiwezi ikawa kwamba viongozi wanajua kweli kuwa huyu ni Kristo, inaweza kuwa?
27 Twayowine kuwa mundu yolo aboka kwaako. Kristo paaisa, hata nyoo, ntopo ywatangite abokakwaako.
Tunajua huyu mtu anatokea wapi. Kristo atakapokuja, hata hivyo, hakuna atakayejua wapi anakotoka.”
28 Yesu abile akombwa lilobe lyake mu'hekalu, kapundisha no baya, “Mwenga mwabote mtangite paniboka. Niisile kwaa kwa nafasi yango, ila ywembe ywanitumile nga wa kweli, na muntangite kwaa ywembe.
Yesu alikuwa akipaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema, “Ninyi nyote mnanijua mimi na mnajua nitokako. Sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye aliyenituma ni wa kweli, na hamumjui yeye.
29 Nintangite ywembe kwa mana niboka kwake nga anitumite.”
Ninamjua yeye kwa sababu nimetoka kwake na alinituma.”
30 Babile kabajaribu kuntaba, lakini ntopo hata yumo ywauluwa luboko lwake nnani yake kwa kuwa saa yake yabile bado iikite.
Walikuwa wanajaribu kumkamata, lakini hakuna hata mmoja aliyeinua mkono wake juu yake kwa sababu saa yake ilikuwa bado haijafika.
31 Hata nyoo, baingi mu'bandu baaminiya. Kababaya, “Kristo paaisile, alowa panga ishara zanyansima kuliko za azipangite mundu yolo?”
Hata hivyo, wengi katika makutano walimwamini. Walisema, “Kristo atakapokuja, atafanya ishara nyingi kuliko alizofanya mtu huyu?”
32 Mafarisayo babayowine bandu kabalongela bembe makowe aga husu Yesu, ni akolo ba makuhani ni Mafarisayo watikubatuma maafisa ili kuntaba.
Mafarisayo waliwasikia makutano wakinong'onezana mambo haya kuhusu Yesu, na wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakatuma maafisa ili kumkamata.
33 Palyo Yesu kabaya, “Bado kwabile ni muda nchunu nabile pamope ni mwenga, ni baadae nalowa boka kuyenda kwake ywembe ywanitumile.
Ndipo Yesu aliposema, “Bado kuna muda kitambo niko pamoja nanyi, na baadaye nitakwenda kwake yeye aliyenituma.
34 Mwalowa kunipala ila munibweni kwaa; kolyo kaniyenda, muweza kwaa kuisa.
Mtanitafuta wala hamtaniona; kule niendako, hamtaweza kuja.”
35 Kwa nyo Ayahudi kabalongela bene kwa bene, “Mundu yoo ayenda kwaako ambako twaweza kwaa kummona? Ayenda kwa batawanyike nkati ya Ayunani ni kubapundisha Ayunani?
Kwa hiyo Wayahudi wakasemezana wao kwa wao, “Mtu huyu atakwenda wapi kwamba tusiweze kumuona? Ataenda kwa Waliotawanyika kati ya Wayunani na kuwafundisha Wayunani?
36 Ni neno lyaako lee alibayite,'Mwalowa kunipala wala mwanibweni kwaa, kolyo niyenda muweza kwaa kuisa?”
Ni neno gani hili alilolisema, 'Mtanitafuta wala hamtaniona; kule niendako hamtamweza kuja'?”
37 Nambeambe mu'lisiku lya mwisho, lisoba likolo lya sikukuu, Yesu ayemi kakombwa lilobe, kabaya, “Mana itei yeyote abile na kiu, aise kwango anywe.
Sasa katika siku ya mwisho, siku kubwa ya sikukuu, Yesu alisimama akapaza sauti, akisema, “Ikiwa yeyote ana kiu, na aje kwangu anywe.
38 Ywembe ywaniaminiye nenga, kati maandiko gabayite, kuoma nkati yake yatitiririka mito ya mase ya ukoto.
Yeye aniaminiye mimi, kama maandiko yalivyosema, kutoka ndani yake itatiririka mito ya maji ya uzima.”
39 Lakini abayite aga kuhusu Roho, ywabile wao watikumwamini walowa kumpoteza; Roho abile bado tolewa kwa sababu Yesu abile atukuzwa kwaa bado.
Lakini aliyasema haya kuhusu Roho, ambaye wao wamwaminio watampokea; Roho alikuwa bado hajatolewa kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa bado.
40 Baadhi ya bandu, pabayowine maneno aga, babayite, “Kweli yolo ni nabii.”
Baadhi ya makutano, waliposikia maneno haya, walisema, “Kweli huyu ni nabii.”
41 Benge babayite, “Ayoo nga Kristo.” Lakini benge babayite, “Kristo aweza kwaa boka Galilaya?
Wengine walisema, “Huyu ni Kristo.” Lakini wengine walisema, “nini, Kristo aweza kutoka Galilaya?
42 Maandiko gabayite kwaa kuwa Kristo aboka mu'lukolo lwa Daudi ni kuoma Bethlehemu, kijiji ambacho Daudi abile?
Maandiko hayajasema kuwa Kristo atatokea katika ukoo wa Daudi na kutoka Bethlehemu, kijiji ambacho Daudi alikuwa?
43 Nyo, patiuluka mgawanyiko nkati ya bandu kwa ajili yake.
Hivyo, pale ukainuka mgawanyiko katikati ya makutano kwa ajili yake.
44 Benge nkati yabe balowa kuntaba, lakini ntopo ywauluwa maboko gake nnani yake.
Wengine kati yao wangelimkamata, lakini hakuna aliyenyoosha mikono yake juu yake.
45 Nga balo maofisa kababuyangine kwa akolo ba makuhani ni mafarisayo, nabo wakaakokeya, “Kwa mwanja namani munletike kwaa?
Ndipo wale maofisa wakarudi kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, nao wakawaambia, “Kwa nini hamjamleta?”
46 Maofisa kaayangwa, “Ntopo mundu ywaweza longela kati yolo kabla.”
Maofisa wakajibu, “Hakuna mtu aliyewahi kuzungumza kama huyu kabla.”
47 Nga mafarisayo kabayangwa, “Ni mwenga pia mwatipotoshwa?
Ndipo Mafarisayo walipowajibu, “Na nyinyi pia mmepotoshwa?
48 Kwabile ni yoyoti nkati ya atawala amwaminiye, au yeyote wa Mafarisayo?
Kuna yeyote kati ya watawala anayemwamini, au yeyote wa Mafarisayo?
49 Ila aba bandu baitangite kwaa saliya-balaanilwe.”
Bali hawa makutano wasiojua sheria - wamelaaniwa.”
50 Nikodemo kaabakiya (ywembe atikunyendea Yesu zamani, abile yumo ywa Mafarisayo),
Nikodemo akawaambia (yeye aliyemwendea Yesu zamani, akiwa mmoja wa Mafarisayo),
51 “Je saliya yitu yaweza kumhukumu mundu ila abile atikusikilizwa kwanza ni kuyowa chaakipangite?
“Je sheria yetu inamhukumu mtu isipokuwa amesikilizwa kwanza na kujua anachokifanya?”
52 Kabanyangwa ni kummakiya, “Ni wenga uboka Galilaya? Tafuta ni ubone kwamba ntopo nabii ywaboka Galilaya.”
Walijibu na kumwambia, “Na wewe pia unatokea Galilaya? Tafuta na uone kwamba hakuna nabii aliyetokea Galilaya.”
(Zingatia: Baadhi ya maneno ya Yohana 7: 53 - 8: 11 hayamo katika nakala bora za kale). Kisha kila mtu alienda nyumbani kwake.

< Yohana 7 >