< Baefeso 2 >

1 Kati yelo mwabile mwawile mu'makosa na sambi yinu.
Kama vile mlivyo kuwa mmekufa katika makosa na dhambi zenu.
2 Yabile mu'aga kwanza mwatiyenda lingana na nyakati ya ulimwengu huu. Mwabile mwatiboka kwa kunkengama ntawala wa mamlaka ya kumaunde. Ayee nga roho yake yolo apangaye kazi mu, bana ba kuasi. (aiōn g165)
Ilikuwa katika haya kwamba kwanza mlienenda kulingana na nyakati za ulimwengu huu. Mlikuwa mkienenda kwa kufuata mtawala wa mamlaka ya anga. Hii ndiyo roho yake yule afanyaye kazi katika wana wa kuasi. (aiōn g165)
3 Twenga wote twabile nkati ya balo baaminiya kwaa hapo mwanzo. Twabile tupangite kwa namna ya tamaa inoite kwaa ya yega yitu. Twabile twapanga mapenzi ga yega yitu ni ufahamu witu. Twabile kwa asili ya bana ba dhahabu kati benge.
Sisi wote hapo mwanzo tulikuwa miongoni mwa hawa wasioamini. Tulikuwa tukitenda kwa namna ya tamaa mbaya za miili yetu. Tulikuwa tukifanya mapenzi ya mwili na ufahamu wetu. Tulikuwa kwa asili wana wa ghadhabu kama wengine.
4 Lakini Nnongo ywabile ni rehema yanyansima kwa sababu ya lipendo lyake likolo lyaatupendile twenga.
Lakini Mungu ni mwingi wa rehema kwa sababu ya pendo lake kubwa alilotupenda sisi.
5 Muda twabile mu'kiwo mu'makosa yitu, atuletya pamope mu'maisha gaayambe nkati ya Kristo. Ni kwa neema kuwa nati lopolelwa.
Wakati tulipokuwa wafu katika makosa yetu, alituleta pamoja katika maisha mapya ndani ya Kristo. Ni kwa neema kwamba mmeokolewa.
6 Nnongo kayogolya mpamo ni kutupanga tama pamope mu'pandu pa'kumaunde nkati ya Kristo Yesu.
Mungu alitufufua pamoja na kutufanya kukaa pamoja katika mahali pa mbingu ndani ya Kristo Yesu.
7 Apangite nyoo ili muda waisa aweze kutubonekea utajiri nkolo wa neema yake. Utubonekeya twenga alee kwa ndela ya wema wake nkati ya Kristo Yesu. (aiōn g165)
Alifanya hivi ili katika nyakati zijazo aweze kutuonesha utajiri mkuu wa neema yake. Hutuonesha sisi hili kwa njia ya wema wake ndani ya Kristo Yesu. (aiōn g165)
8 Kwa neema mupangilwe akochopoli kwa ndela ya imani. Na yee iboka kwaa kwitu. Ni zawadi ya Nnongo.
Kwa neema mmeokolewa kwa njia ya imani. Na hii haikutoka kwetu. Ni zawadi ya Mungu.
9 Itokana kwaa ni makowe. Matokeo gake, abile kwaa mundu yumo ywa kujisifu.
Haitokani na matendo. Matokeo yake, asiwepo mmoja wapo wa kujisifu.
10 Kwa sababu twenga twabile kazi ya Nnongo. tuumbilwe mu'Kristo Yesu upanga makowe yanoite. Ni makowe aga ambayo Nnongo agapangite tangu zamani za kale kwaajili yitu, ili tutyange mu'agoo.
Kwa sababu sisi tu kazi ya Mungu, tumeumbwa katika Kristo Yesu kutenda matendo mema. Ni matendo haya ambayo Mungu aliyapanga tangu zamani za kale kwa ajili yetu, ili tutembee katika hayo.
11 Kwa nyo mukumbukye kuwa kunchogo mwabile bandu ba mataifa kwa namna ya yega. Mkemelwa”mbile kwaa ni tohara” kwa chelo chakemelwa tohara ya yega yapangilwe kwa maboko ga bandu.
Kwa hiyo kumbukeni kwamba hapo zamani mlikuwa watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili. Mnaitwa “msio na tohara” kwa kile kinachoitwa tohara ya mwili inayofanywa kwa mikono ya binadamu.
12 Kwa muda woo mwabile mwati tengwa na Kristo. Mwabile ageni kwa bandu ba Israeli. Mwabile ageni kwa liagano lya ahadi. Mwabile kwaa ni uhakika wa muda uisile. Mwabile bila Nnongo mu'ulimwengu.
Kwa wakati huo mlikuwa mmetengwa na Kristo. Mlikuwa wageni kwa watu wa Israel. Mlikuwa wageni kwa agano la ahadi. Hamkuwa na uhakika wa wakati ujao. Mlikuwa bila Mungu katika ulimwengiu.
13 Lakini nambeambe mu'Kristo Yesu mwenga ambao kunchogo mwabile kutalu ni Nnongo mpangilwe papipi ni Nnongo kwa mwai ya Kristo.
Lakini sasa katika Kristo Yesu ninyi ambao hapo mwanzo mlikuwa mbali na Mungu mmeletwa karibu na Mungu kwa damu ya Kristo.
14 Kwa mana ywembe nga amani yitu. Apangite abele kuwa yumo. Kwa yega yake atikuuharibu ukuta wa utengano wabile utitenganisha, huo uadui.
Kwa maana yeye ndiye amani yetu. Alifanya wawili kuwa mmoja. Kwa mwili wake aliuharibu ukuta wa utengano ambao ulikuwa umetutenganisha, huo uadui.
15 Kwamba atikuikomesha saliya ya amri na kanuni ili aumbile mundu yumo wayambe nkati yake. Apangite amani.
Kwamba alikomesha sheria ya amri na kanuni ili kwamba aumbe mtu mmoja mpya ndani yake. Akafanya amani.
16 Apangite nyoo ili kubakwembanisha makundi abele ya bandu kuwa yega yimo kwa Nnongo petya msalaba. Kwa ndela ya msalaba aupangite uadui kuwa kiwo
Alifanya hivi ili kuwapatanisha makundi mawili ya watu kuwa mwili mmoja kwa Mungu kupitia msalaba. Kwa njia ya msalaba aliufisha uadui.
17 Yesu aisile ni kutangaza amani kwinu mwenga mwabile kutalu ni amani kwa balo babile papipi.
Yesu alikuja na kutangaza amani kwenu ninyi mliokuwa mbali na amani kwao wale waliokuwa karibu.
18 Kwa mana kwa ndela ya Yesu twenga abele tubile na nafasi kwa yolo Roho yumo kuyingya kwa Tate.
Kwa maana kwa njia ya Yesu sisi wote wawili tuna nafasi kwa yule Roho mmoja kuingia kwa Baba.
19 Nyoo bai, mwenga bandu ba mataifa mwasafiri kwaa ni ageni kae. Ila mwa wenyeji pamope ni balo batengwile kwa ajili ya Nnongo ni ajumbe mu'nyumba ya Nnongo.
Hivyo basi, ninyi watu wa mataifa si wasafiri na wageni tena. Bali ni wenyeji pamoja na wale waliotengwa kwa ajili ya Mungu na wajumbe katika nyumba ya Mungu.
20 Mchengwilwe nnani ya msingi wa mitume ni manabii. Kristo Yesu mwene abile liwe kolo lya mbembeni.
Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii. Kristo Yesu mwenyewe alikuwa jiwe kuu la pembeni.
21 Mu'ywembe lyengo lyoti latikuunganisha pamope ni kukua kati hekalu nkati ya Ngwana.
Katika yeye jengo lote limeungamanishwa pamoja na kukua kama hekalu ndani ya Bwana.
22 Ni nkati yake mwenga mchengwilwe pamope kati mahali pa tamya pa Nnongo mu'Roho.
Ni ndani yake ninyi nanyi mnajengwa pamoja kama mahali pa kuishi pa Mungu katika Roho.

< Baefeso 2 >