< Akolosai 1 >

1 Paulo mmanda wa Kristo kwa mapenzi ga Nnongo, ni Timotheo nongo yitu,
Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu,
2 kwa baumini ni alongo baaminifu mu'Kristo babile Kolosai. Neema ibe kwinu, na amani kuoma kwa Nnongo Tate yitu.
kwa waumini na ndugu waaminifu katika Kristo walioko Kolosai. Neema iwe kwenu, na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu.
3 Twampeya shukrani Nnongo, Tate wa Ngwana witu Yesu Kristo, ni twalowa kualobia mara kwa mara.
Tunatoa shukrani kwa Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, na tunawaombea mara kwa mara.
4 Twayowine imani yinu mu'Yesu Kristo ni upendo mbile nabo kwa balo bote babile batengwa kwa ajili ya Nnongo.
Tumesikia imani yenu katika Yesu Kristo na upendo mlionao kwa wale wote waliotengwa kwa ajili ya Mungu.
5 Mwabile ni upendo woo kwa sababu ya litaraja lya uhakika lyalibekilwe kumaunde kwa ajili yinu. Muyowine kuhusu litaraja lee lya uhakika kabla mu'lineno lya kweli, injili,
Mna upendo huu kwa sababu ya taraja la uhakika lililohifadhiwa mbinguni kwa ajili yenu. Mlisikia kuhusu taraja hiyo ya uhakika kabla katika neno la kweli, injili,
6 ambayo iisile kwinu. Injili yee ipambike matunda ni kuenea mu'ulimwengu woti. Yabile ipanga nyoo nkati yinu kae boka lisoba mwamuiyowine na kuipunza kuhusu neema ya Nnongo mu'kweli.
ambayo imekuja kwenu. Injili hii inazaa tunda na inaenea ulimwenguni kote. Imekuwa ikifanya hivi ndani yenu pia tangu siku mlipoisikia na kujifunza kuhusu neema ya Mungu katika kweli.
7 Ayee nga innjili mwaifunzile boka kwa Epafra, mpendwa witu mmanda mwaitu, ywabile ni mmanda mwaminifu wa Kristo kwa niaba yitu.
Hii ndiyo injili mliyojifunza kutoka kwa Epafra, mpendwa wetu mtumishi mwenzetu, ambaye ni mtumishi mwaminifu wa Kristo kwa niaba yetu.
8 Epafra aupangite uyowanike kwitu upendo winu mu'Roho.
Epafra ameufanya ujulikane kwetu upendo wenu katika Roho.
9 Kwa sababu ya upendo woo, boka lisoba twatuyowine lee, tulekite kwaa kuwalobia. Twabile tukiloa kuwa mjazilwe ni maarifa ga mapenzi yake mu'hekima yoti ni ufahamu wa kiroho.
Kwa sababu ya upendo huu, tangu siku tuliposikia hivi, hatujaacha kuwaombea. Tumekuwa tukiomba kwamba mtajazwa na maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa kiroho.
10 Twabile tukiloba kwamba mwalowa tyanga kwa ustahamilivu wa Ngwana mu'ndela yaipendilwe. Twabile tukiloba kuwa mwalowa pambika matunda mu'kila likowe linoite ni kuwa mwalowa kuwa mu'maarifa ga Nnongo.
Tumekuwa tukiomba kwamba mtatembea kwa ustahimilivu wa Bwana katika njia zipendezazo. Tumekuwa tukiomba kwamba mtazaa tunda katika kila tendo jema na kwamba mtakua katika maarifa ya Mungu.
11 Twatiloba muweze kupeyelwa likakala mu'kila uwezo lingana na likakala lya utukufu wake mu'uvumilivu ni ustahamilivu woti.
Tunaomba mweze kutiwa nguvu katika kila uwezo kulingana na nguvu za utukufu wake katika uvumilivu na ustahimilivu wote.
12 Twaloba kuwa, kwa puraha, mwalowa mpeya shukrani Tate, ywabapanga mwenga muweze kuwa ni sehemu mu'urithi wa baumini mu'bweya.
Tunaomba kwamba, kwa furaha, mtatoa shukrani kwa Baba, aliyewafanya ninyi mweze kuwa na sehemu katika urithi wa waumini katika nuru.
13 Atitulopwa boka mu'utawala wa libendo ni kutubeka mu'upwalume wa Mwana wake ywampendile.
Ametuokoa kutoka katika utawala wa giza na kutuhamishia katika ufalme wa Mwana wake mpendwa.
14 Pitya mwana wake twabile ni ukochopoli. msamaha wa sambi.
Katika Mwanae tuna ukombozi, msamaha wa dhambi.
15 Mwana nga mpwano wa Nnongo ywabonekana kwaa. Ni mbeleki wa kwanza wa uumbaji woti.
Mwana ni mfano wa Mungu asiyeonekana. Ni mzaliwa wa kwanza wa uumbaji wote.
16 Kwa kuwa kwa ywembe ilebe yoti iumbilwe, vyabile kumaunde ni vyabile mu'dunia, ilebe ibonekana na ibonekana kwaa. mana itei ni vya enzi au mamlaka au utawala au wabile ni likakala, ilebe yoti iumbilwe ni ywembe na kwaajili yake.
Kwakuwa kwa yeye vitu vyote viliumbwa, vile vilivyoko mbinguni na vilivyoko duniani, vitu vinavyoonekana na visivyoonekana. ikiwa ni vya enzi au mamlaka au utawala au wenye nguvu, vitu vyote viliumbwa na yeye na kwa ajili yake.
17 Ywembe ywabile kabla ya ilebe yoti, ni nkati ya ywembe vyatishikana mpamo.
Yeye amekuwepo kabla ya vitu vyote, na katika yeye vitu vyote vinashikamana pamoja.
18 Ni ywembe nga ntwe wa yega yaani likanisa, ywembe nga mwanzo na mbeleki wa kwanza kuoma nkati ya bandu ba kiwo, nga nyoo, abile ni nafasi ya kwanza nkati ya ilebe yoti.
Na yeye ndiye kichwa cha mwili yaani kanisa, yeye ni mwanzo na mzaliwa wa kwanza kutoka miongoni mwa wafu, hivyo, ana nafasi ya kwanza miongoni mwa vitu vyote.
19 Kwa kuwa Nnongo atipendezwa kuwa utimilifu wake woti utami nkati yake,
Kwa kuwa Mungu alipendezwa kwamba utimilifu wake wote uishi ndani yake,
20 ni kupatanisha ilebe yoti kwake kwa ndela ya mwana wake. Nnongo apangite amani petya mwai ya msalaba wake. Nnongo atikuwapatanisha ilebe yoti kwake mwene, mana itei ni ilebe ya mu'dunia au ile ya kumaunde.
na kupatanisha vitu vyote kwake kwa njia ya Mwanawe. Mungu alifanya amani kupitia damu ya msalaba wake. Mungu alipatanisha vitu vyote kwake mwenyewe, ikiwa ni vitu vya duniani au vitu vya mbinguni.
21 Mwenga kae, kwa muda umo mwabile ni ageni kwa Nnongo, na mwabile maadui wake mu'akili ni makowe mabou.
Nanyi pia, kwa wakati mmoja mlikuwa wageni kwa Mungu na mlikuwa maadui wake katika akili na matendo maovu.
22 Lakini nambeambe atikwapatanisha mwenga kwa yega wake pitya mu'kiwo. Apangite nyoo ili kubaleta mwenga atakatifu, babile kwaa ni lawama ni bila disari nnonge yake,
Lakini sasa amewapatanisha ninyi kwa mwili wake kupitia kifo. Alifanya hivi ili kuwaleta ninyi watakatifu, wasio na lawama na bila dosari mbele yake,
23 kati mwatiyendelea mu'imani, mwabile mwatiimarishwa ni kuwa thabiti, pabile kwaa kudondoshwa kutalu kuoma mu'litaraja lya ujasiri lya injili mwaiyowine. Ayee nga injili itangazilwe kwa kila mundu ywaumbilwe pae ya kumaunde. Ayee nga injili yabile kwake nenga, Paulo nabile mmanda.
kama mkiendelea katika imani, mliyoimarishwa na kuwa thabiti, pasipo kuondoshwa mbali kutoka kwenye taraja la ujasiri la injili mliyoisikia. Hi ndiyo injili iliyotangazwa kwa kila mtu aliyeumbwa chini ya mbingu. Hii ndiyo injili ambayo kwayo mimi, Paulo, nimekuwa mtumishi.
24 Nambeambe napuraikiya mateso gango kwa ajili yinu. Nenga nalitimiza mu'yega yango chakipungwi kwa mateso ga Kristo kwa ajili ya yega wake, wabile ni likanisa.
Sasa nafurahia mateso yangu kwa ajili yenu. Nami natimiliza katika mwili wangu kinachopungua kwa mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, ambao ni kanisa.
25 Nenga na mmanda wa likanisa lee, sawa sawa ni wajibu wanipeilwe boka kwa Nnongo kwa ajili yinu, kulijaza neno lya Nnongo.
Mimi ni mtumishi wa kanisa hili, sawasawa na wajibu niliopewa kutoka kwa Mungu kwa ajili yenu, kulijaza neno la Mungu.
26 Awoo nga ukweli wa siri yaibile iyowanika kwaa kwa miaka yanansima kwa ibeleko. Lakini nambeambe iyowanike kwa bote baaminio mu'ywembe. (aiōn g165)
Huu ni ukweli wa siri iliyokuwa imefichwa kwa miaka mingi na kwa vizazi. Lakini sasa imefunuliwa kwa wote waaminio katika Yeye. (aiōn g165)
27 Ni kwa balo ambao Nnongo apala kuafunua ubile utajiri wa utukufu wa siri ya ukweli woo nkati ya mataifa. Ni kwamba Kristo abile nkati yinu, ujasiri wa utukufu waisa.
Ni kwa wale ambao Mungu alitaka kufunua kulivyo utajiri wa utukufu wa siri ya ukweli huu miongoni mwa Mataifa. Ni kwamba Kristo yumo ndani yenu, ujasiri wa utukufu ujao.
28 Ayoo nga tumbayaye. Twankanikiya kila mundu, na kumfundisha kila mundu mkamilifu mu'Kristo.
Huyu ndiye tunayemtangaza. Tunamwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu kwa hekima yote, ili kwamba tumlete kila mtu mkamilifu katika Kristo.
29 Kwa ajili ya lee, nenga najibadilisha na kujitahidi lingana na likakala lyake lya lipanga kazi nkati yango mu'uweza.
Kwa jili hii, mimi najibidisha na kujitahidi kulingana na nguvu yake ifanyayo kazi ndani yangu katika uweza.

< Akolosai 1 >