< Matendo ga Mitume 2 >

1 Paikite lisoba lya Pentekoste, bote babile pamope sehemu imo.
Ilipofika siku ya Pentekoste, wote walikuwa pamoja sehemu moja.
2 Ghafla lyapitike limbonga boka kunani kati mbepo kale, ngautweliya nyumba yote mwababile batami.
Ghafla ikatokea muungurumo kutoka mbinguni kama upepo mkali. ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi.
3 Hapo kabapitya lulimi, kati lulimi lwa mwoto zatigawanyika, ibile nnani yabe kila yumo wabe.
Hapo zikawatokea ndimi, kama ndimi za moto zimegawanyika, zikawa juu yao kila mmoja wao.
4 Bembe bote batwelilwe na Roho Mtakatifu na batumbwile baya kwa lugha yenge, kati yelo Roho atibajalia longela.
Wao wote wakajazwa na Roho Mtakatifu na wakaanza kusema kwa lugha zingine, kama vile Roho alivyowajalia kusema.
5 Babile Ayahudi babatamage Yerusalemu bandu ba Nnongo, boka kila litaifa pae ya kumaunde.
Sasa walikuwapo wayahudi waliokuwa wanaishi Yerusalemu, wacha Mungu, kutoka kila taifa chini ya mbingu.
6 Nundumo paziwowanike, likundi lya bandu liisile pamope na babile ni wasiwasi kwa sababu kila mundu bayowine bakilongela kwa lugha yake mwene.
Ngurumo hizi ziliposikiwa, kundi la watu likaja pamoja na wakiwa na wasiwasi kwa sababu kila mtu aliwasikia wakiongea kwa lugha yake mwenyewe.
7 Batisangala muno, bembe kababaya, “Kweli aba bote balongela Baagalilaya kwaa?
waliduwaa na kushangazwa, wao walisema, “Kweli, hawa wote wanaoongea siyo Wagalilaya?
8 Kwa mwanja namani twayowine, kila yumo katika lugha tubelekilwe nayo?
Kwa nini sisi tunawasikia, kila mmoja katika lugha tulizozaliwa nazo?
9 Waparthia na Bamedi na Baelamu, na bembe batama Mesopotamia, Uyahudi, na Kapadokia, na katika Ponto na Asia,
Waparthia na Wamedi na Waelamu, na hao waishio Mesopotamia, Uyahudi, na Kapadokia, na katika Ponto na Asia,
10 katika Frigia, Pamfilia, katika Misri, na sehemu ya Libya hata Kirene, na ageni boka Rumi,
katika Frigia, Pamfilia, katika Misri, na sehemu ya Libya hata Kirene, na wageni kutoka Rumi,
11 Ayahudi na baongofu, Bakrete na Baarabu, twayowa bakilongela katika lugha yitu kuhusu kazi ya uweza wa Nnongo.”
Wayahudi na waongofu, Wakrete na Waarabu, tunawasikia wakizungumza katika lugha zetu kuhusu kazi za uweza wa Mungu.”
12 Bote babile batishangala na tatanishwa; balongela bembe, “Ayee ibile na maana gani?”
Wote walikuwa wameduwaa na kutatanishwa; walisemezana wao kwa wao, “Hii ina maana gani?”
13 Lakini benge batidhihaki kababaya, “Aba banywile mvinyo wa ayambe.”
Lakini wengine walidhihaki wakisema, “Hawa wamejazwa kwa mvinyo mpya.”
14 Lakini Petro ayemi pamope na balo komi na jimo, ngabendya kaabakiya, “Bandu ba Yudea na bote mwatama pano Yerusalemu, lee liyowanike kwinu, muliyowe kwa makini maneno gango.
Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti, akawaambia, “Watu wa Yudea na wote mnaoishi hapa Yerusalemu, hili lijulikane kwenu, sikilizeni kwa makini maneno yangu.
15 Bandu aga batangite kwaa kati yamugawaza, kwa sababu ayee nga bwamba wa saa tatu.
Watu hawa hawajalewa kama mnavyodhani, sababu saa hizi ni asubuhi saa tatu.
16 Lakini lee libile latilongelwa pitya kwa nabii Yoeli.
Lakini hili lilikuwa limesemwa kupitia kwa nabii Yoeli:
17 Yalowa katika masoba ga mwisho, Nnongo abaya, napengana Roho bango kwa bandu bote. Bana binu na alombo binu balowa piya unabii, anchembe binu balola maono, na apindo binu walowa lota ndoto.
Itakuwa katika siku za mwisho; Mungu asema, nitamwaga Roho wangu kwa watu wote. Wana wenu na binti zenu watatoa unabii, vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.
18 Nyonyonyo nnani ya batumishi bango ba kale katika masoba ago, naapekaniya Roho wango, bembe balowa tabiri.
Vilevile juu ya watumishi wangu na watumishi wangu wa kike katika siku hizo, nitamwaga Roho wangu, nao watatabiri.
19 Nalowa kuwabonekeya maajabu nnani ya'anga na ishara pae ya dunia, myai, mwoto na mapundisho ga lyoi.
Nitaonesha maajabu juu angani na ishara chini duniani, damu, moto, na mafusho ya moshi.
20 Liumu lalowa badilishwa na kuwa libendo na mwei kuwa myai, kabla kuisa kwa lisoba likolo na ya ajabu ya Ngwana.
Na jua litabadilishwa kuwa giza na mwezi kuwa damu, kabla haijaja siku kuu na ya ajabu ya Bwana.
21 Yalowa pangika ya kwanza kila yumo ywabile alikema lina lya Ngwana alowa lopolelwa.'
itakuwa ya kwamba kila mmoja ambaye huliitia jina la Bwana ataokoka.'
22 Bandu ba Israeli, mugayowe maneno aga: Yesu wa Nazareti, mundu ywathibitishwa na Nnongo kwinu kwa matendo ga uweza na maajabu, na ishara ambazo Nnongo pitya ywembe katikati yinu, mana mwenga mwabene mutangite.
Watu wa Israeli, sikieni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mwanadamu aliyethibitishwa na Mungu kwenu kwa matendo ya uweza na maajabu, na ishara ambazo Mungu kupitia Yeye katikati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua-
23 Kwa sababu ya mpango waukusidiwa tangu mwanzo, na maarif ga Nnongo apiyilwe na mwenga, kwa maboko ga bandu baarifu, mwatikunsulubisha na kumulaga.
Kwa sababu ya mpango uliokusudiwa tangu mwanzo, na maarifa ya Mungu, alitolewa, na ninyi, kwa mikono ya watu wahalifu, mlimsulibisha na kumuua,
24 Ywabile Nnongo atikundondobeya, aboyele uchungu wa kiwo chake, kwa sababu iwezekana kwaa kwake kumilikiwa nabo.
ambaye Mungu alimwinua, akauondoa uchungu wa mauti kwake, kwasababu haikuwezekana kwake kumilikiwa na huo.
25 Nga nyo Daudi abaya kuhusu ywembe, “Nimweni Ngwana daima nnongi ya minyo bango, ywembe abile luboko lwangi lwa mmaliyo nga nyoo bai nasogezwa kwaa.
Hivyo Daudi anasema kuhusu yeye, 'Nilimwona Bwana daima mbele ya uso wangu, yeye yuko mkono wangu wa kulia hivyo basi sitasogezwa.
26 Kwa eyo mwoyo wango ubile na puraha na lulimi lwango watipuraishwa. Yega yango kae walowa tama katika ujasiri.
Kwa hiyo moyo wangu ulikuwa na furaha na ulimi wangu ulifurahishwa. Pia mwili wangu utaishi katika ujasiri.
27 Uileka kwaa nafsi yango iyende kuzimu, wala uruhusu kwaa Mtakatifu wako kubona uozo. (Hadēs g86)
Hutaiacha nafsi yangu iende kuzimu, wala hutaruhusu Mtakatifu wako kuona uozo. (Hadēs g86)
28 Wenga utijidhihirisha kwango ndela ya ukoto, walowa nipanga nijae puraha nnongi ya minyo gako.'
Wewe umedhihirisha kwangu njia za uzima; utanifanya nijae furaha mbele ya uso wako.'
29 Mwalongo, naweza longela kwinu kwa ujasiri kuhusu tate bitu Daudi, ywembe awile na sikwa, na kaburi lyake libile pamope ni twenga hata nambeambe.
Ndugu, ninaweza kuzungumza kwenu kwa ujasiri kuhusu baba yetu Daudi: yeye alikufa na akazikwa, na kaburi lake liko pamoja nasi hata hivi leo.
30 Nga nyo abile nabii na atangite kuwa Nnongo atilapa kwa kilapo sake, panga alowa beka yumo katika ubeleki wake katika iteo sa enzi.
Hivyo, alikuwa nabii na alijua kuwa Mungu alishaapa kwa kiapo kwake, kwamba ataweka mmoja katika uzao wake kwenye kiti cha enzi.
31 Alibweni lee mapema, na abayite kuhusu ufufuo wa Kristo,'wala abile alekwa kwaa kuzimu (Hadēs g86)
Aliliona hili mapema, na akasema kuhusu ufufuo wa Kristo, 'wala alikuwa hakuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuoza.' (Hadēs g86)
32 Ayoo Yesu-Nnongo atimfufua, ambaye twenga twabote ni mashahida.
Huyu Yesu - Mungu alimfufua, ambaye sisi wote ni mashahidi.
33 Kwa eyo, abile atiinulilwa katika luboko lwa kummalyo ba Nnongo, na abile atimpokya ahadi ya Roho Mtakatifu boka kwa Tate, Ywembe atimimina ahadi yee, ambaye mwenga mwabona na kuyowa.
Kwa hiyo, akiwa ameinuliwa katika mkono wa kuume wa Mungu, na akiwa amepokea ahadi ya Roho Mtakatifu kutoka kwa Baba, yeye amemimina hii ahadi, ambaye ninyi mnaona na kusikia.
34 Mana Daudi angolwike kwaa yendya kumaunde, lakini abaya,'NGWANA abaya kwa Ngwana wango.
Kwani Daudi hakupaa kwenda mbinguni, lakini anasema, 'BWANA alisema kwa Bwana wangu,
35 “Tama luboko lwango lwa kummalyo, mpaka panibapanga maadui bako kigoda kwa ajili ya magolo gako.
“keti mkono wangu wa kulia, mpaka nitakapowafanya adui zako kigoda kwa ajili ya miguu yako.
36 Kwa eyo nymba yote ya Israeli na itange kwa hakika panga Nnongo abapangite ywembe kuwa Ngwana na Kristo, yolo Yesu ambaye mwatimsulubisha.”
Kwa hiyo nyumba yote ya Israeli na ijue kwa hakika kwamba Mungu amemfanya Yeye kuwa Bwana na Kristo, huyu Yesu ambaye mlimsulibisha.”
37 Pabayowine nyoo, basonywi katika mioyo yabe, kabammakiya Petro na mitume yenge, “Mwalongo, tupange namani?”
Sasa waliposikia hivyo, wakachomwa katika mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, “Ndugu, tufanyeje?”
38 Na Petro kaabakiya, “Muipange toba na Mbatizwe, kila yumo winu, katika lina lya Yesu Kristo kwa ajili ya msamaha wa sambi yinu, na mwalowa pokya zawadi ya Roho Mtakatifu.
Na Petro akawaambia, “Tubuni na Mbatizwe, kila mmoja wenu, katika jina la Yesu Kristo kwa ajili ya msamaha wa dhambi zenu, na mtapokea zawadi ya Roho Mtakatifu.
39 Mana kwinu ni ahadi na kwa bana binu na kwa balo bote babile kutalu, bandu banyansima kwa kadri Ngwana Nnongo witu paakema.”
Kwani kwenu ni ahadi na kwa watoto wenu na kwa wale wote walioko mbali, watu wengi kwa kadri Bwana Mungu wetu atakavyowaita.”
40 Kwa maneno ganyansima ashuhudia na kubasihi, “Muilopwe boka katika ibeleko yee kiovu.”
Kwa maneno mengi alishuhudia na kuwasihi; alisema, “Jiokoeni mtoke katika kizazi hiki kiovu.”
41 Nga kabapokii maneno gake na kaabatiza, hapo kabaongezeka katika lisoba lee kati nafsi elfu tatu.
Ndipo wakayapokea maneno yake na wakabatizwa, hapo wakaongezeka katika siku hiyo kama nafsi elfu tatu.
42 Kabayendelya katika mapundisho ya mitume na ushirikiano, katika kuumega mkate na katika maombi.
Wakaendelea katika mafundisho ya mitume na ushirikiano, katika kuumega mkate na katika maombi.
43 Hofu yaisa nnani ya kila nafsi, na maajabu ganyansima na ishara zapangika pitya mitume.
Hofu ikaja juu ya kila nafsi, na maajabu mengi na ishara zikafanyika kupitia mitume.
44 Bote baaminiya babile pamope na kuwa na ilebe yabembe pamope,
Wote walioamini walikuwa pamoja na kuwa na vitu vyao kwa pamoja,
45 na bapemeya ilebe na milki yabe na kugawanya kwa bote lingana na hitaji lya kila yumo.
na waliuza vitu na milki zao na kugawanya kwa wote kulingana na hitaji la kila mmoja.
46 Nga nyoo lisoba baada ya lisoba kabayendelea babile na lengo limo katika hekalu, na batiumega mkate mu'nyumba, na batishiriki chakulya kwa puraha na unyenyekevu wa mwoyo;
Hivyo siku baada ya siku waliendelea wakiwa na lengo moja katika hekalu, na walimega mkate kwenye kaya, na walishiriki chakula kwa furaha na unyenyekevu wa moyo;
47 Batimsifu Nnongo na babile na kibali na bandu bote. Ngwana atibaongeza lisoba kwa lisoba ambao babile batilopolwa.
walimsifu Mungu na wakiwa na kibali na watu wote. Bwana aliwaongeza siku kwa siku ambao walikuwa wakiokolewa.

< Matendo ga Mitume 2 >