< 2 Athesalonike 3 >

1 Nambiambi mwalongo mutulubii, linga likowe lya Nngwana hendelitukuzwa Kati mwaibile kwinu.
Na sasa, ndugu, tuombeeni, kwamba neno la Bwana liweze kuenea na kutukuzwa, kama ilivyo pia kwenu.
2 Mulube tuweze pona buka kwa bandu alau kwa kuwa botilii bene imani.
Ombeni kwamba tuweze kuokolewa kutoka katika uovu na watu waasi, kwa kuwa si wote wana imani.
3 Lakini Nngwana mwaminifu, ywembe ampanga mwinga nyimee na kunendila kwa yulo nnau.
Lakini Bwana ni mwaminifu, ambaye atawaimarisha ninyi na kuwalinda kutoka kwa yule mwovu.
4 Tui na ujasili kwa Nngwana kwa sababu yinu, mpanga maendeleo na mpayendelya panga ghalu gatunagile.
Tunaujasiri katika Bwana kwa ajili yenu, kwamba mnatenda na mtaendelea kutenda mambo ambayo tunawaagiza.
5 Nngwana awese kunongaya mioyo yinu katika upendo na katika komeo kwa Kirisitu.
Bwana aweze kuongoza mioyo yenu katika upendo na katika uvumilivu wa Kristo.
6 Tunda kunagya mwalongo, katika lina lya Nngwana Yesu Kirisitu, mwepuke kila nongo ywaishi kwa ukata na galuli mwamughapokile ga desturi ya buka kwitu.
Sasa tunawaagiza, ndugu, katika jina la Bwana Yesu Kristo, kwamba mwepuke kila ndugu ambaye anaishi maisha ya uvivu na siyo kwa kutokana na desturi ambazo mlipokea kutoka kwetu.
7 Kwa kuwa mwabene mutangike sawa kwinu kutujiga twee. Tutamili kwinu Kati balu bangali heshima.
Kwa kuwa ninyi wenyewe mnajua ni sawa kwenu kutuiga sisi. Hatukuishi miongoni mwenu kama wale ambao hawakuwa na nidhamu.
8 Tulileli chakulya cha mundu yeyote bila kunnepa. Badala yake, twapangite kachi kiloo na mutwe Kati kwa kachi ngumu na kwa mataticho linga kana tupange michigo Kwan yeyote katika mwenga.
Na hatukula chakula cha mtu yeyote bila kukilipia. Badala yake, tulifanya kazi usiku na mchana kwa kazi ngumu na kwa shida, ili tusiweze kuwa mzigo kwa yeyote katika ninyi.
9 Tupangite ga kwa sababulii twaina mamlakalii, Badala yake, twapangi linga tube mfano kwinu linga mutuyige twee.
Tulifanya hivi si kwa sababu hatuna mamlaka. Badala yake, tulifanya hivi ili tuwe mfano kwenu, ili kwamba mweze kutuiga sisi.
10 Palu patubile pamo na mwenga twati kunnogya, “Kati yinu Mana mundu haakani panga kachi kana alye”.
Wakati tulipokuwa pamoja nanyi tuliwaagiza, “Ikiwa mmoja wenu hataki kufanya kazi, na asile.”
11 Kwa kuwa tuyuwine baadhi yinu bayendelya kwa ukata miongoni mwitu. Bapangalii kachi lakini badala yake bandu bangali utaratibu.
Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi wanaenenda kwa uvivu miongoni mwenu. Hawafanyi kazi lakini badala yake ni watu wasio na utaratibu.
12 Tumbwe kwa aboo tunda kualagya na kuabakia katika Nngwana Yesu Kirisitu bapange kachi lazima kwa utulivu na lya chakulya chabe bene.
Sasa hao nao tunaagiza na kuwaasa katika Bwana Yesu Kristo, kwamba lazima wafanye kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe.
13 Lakini mwenga mwalongo kana muuimike mioyo katika panga gagapalikwa.
Lakini ninyi, ndugu, msizimie roho katika kufanya yaliyo sahihi.
14 Mana mundu yeyote hakani panga ga makowe gitu ga ujumbe wumo, mube nakwe makini na ywembe na kana mube shirika nakwe pamo linga apate oni.
Ikiwa mtu yeyote hataki kutii neno letu katika waraka huu, mwe makini naye na msiwe na ushirika pamoja naye, ili kwamba aweze kuaibika.
15 Kana muputulii kati alui, lakini mukwileke kati nongo.
Msimchukulie kama adui, lakini mwonyeni kama ndugu.
16 Nngwana wa Amani ampei Amani wakati woti katika ndila yote. Nngwana abe na mwenga mwaboti.
Bwana wa amani mwenyewe awape amani wakati wowote katika njia zote. Bwana awe nanyi nyote.
17 Yinu nga salamu yangu Paulo kwa luboko lwangu namwene ambago alamaa kila barua. Nya ngani andika.
Hii ni salam yangu, Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe, ambayo ni alama katika kila waraka. Hivi ndivyo niandikavyo.
18 Neema ya Nngwana Yesu Kirisitu ibe na mwenga mwaboti.
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iweze kuwa nanyi nyote.

< 2 Athesalonike 3 >