< Colossenes 2 >

1 Volo enim vos scire qualem solicitudinem habeam pro vobis, et pro iis, qui sunt Laodiciae, et quicumque non viderunt faciem meam in carne:
Kwa kuwa nataka mfahamu jinsi ambavyo nimekuwa na taabu nyingi kwa ajili yenu, kwa wote walioko Laodikia na kwa wote ambao hawajaona uso wangu katika mwili.
2 ut consolentur corda ipsorum, instructi in charitate, et in omnes divitias plenitudinis intellectus, in agnitionem mysterii Dei Patris et Christi Iesu:
Nafanya kazi ili kwamba mioyo yao iweze kufarijiwa kwa kuletwa pamoja katika upendo na katika utajiri wote wa wingi wa uhakika kamili wa maarifa, katika kuijua siri ya kweli ya Mungu, ambaye ni Kristo.
3 in quo sunt omnes thesauri sapientiae, et scientiae absconditi.
Katika Yeye hazina zote za hekima na maarifa zimefichwa.
4 Hoc autem dico, ut nemo vos decipiat in sublimitate sermonum.
Nasema hivi ili kwamba mtu yeyote asije akawafanyia hila kwa hotuba yenye ushawishi.
5 Nam etsi corpore absens sum, sed spiritu vobiscum sum: gaudens, et videns ordinem vestrum, et firmamentum eius, quae in Christo est, fidei vestrae.
Na ingawa sipo pamoja nanyi katika mwili, lakini nipo nanyi katika roho. Ninafurahi kuona utaratibu wenu mzuri na nguvu ya imani yenu katika Kristo.
6 Sicut ergo accepistis Iesum Christum Dominum, in ipso ambulate,
Kama mlivyompokea Kristo Bwana, tembeeni katika yeye.
7 radicati, et superaedificati in ipso, et confirmati in fide, sicut et didicistis, abundantes in illo in gratiarum actione:
Mwimarishwe katika yeye, mjengwe katika yeye, mwimarishwe katika imani kama tu mlivyofundishwa, na kufungwa katika shukrani nyingi.
8 Videte ne quis vos decipiat per philosophiam, et inanem fallaciam secundum traditionem hominum, secundum elementa mundi, et non secundum Christum:
Angalieni ya kwamba mtu yeyote asiwanase kwa falsafa na maneno matupu ya udanganyifu kulingana na mapokeo ya wanadamu, kulingana na kanuni za kidunia, na sio kulingana na Kristo.
9 quia in ipso inhabitat omnis plenitudo divinitatis corporaliter:
Kwa kuwa katika yeye ukamilifu wote wa Mungu unaishi katika mwili.
10 et estis in illo repleti, qui est caput omnis principatus, et potestatis:
Nanyi mmejazwa katika yeye. Yeye ni kichwa cha kila uweza na mamlaka.
11 in quo et circumcisi estis circumcisione non manu facta in expoliatione corporis carnis, sed in circumcisione Christi:
Katika yeye pia mlitahiriwa kwa tohara isiyofanywa na wanadamu katika kuondolewa mwili wa nyama, lakini ni katika tohara ya Kristo.
12 consepulti ei in baptismo, in quo et resurrexistis per fidem operationis Dei, qui suscitavit illum a mortuis.
Mlizikwa pamoja naye katika ubatizo. Na kwa njia ya imani katika yeye mlifufuliwa kwa uweza wa Mungu, aliyemfufua kutoka kwa wafu.
13 Et vos cum mortui essetis in delictis, et praeputio carnis vestrae, convivificavit cum illo, donans vobis omnia delicta:
Na mlipokuwa mmekufa katika makosa yenu na kutokutahiriwa kwa miili yenu, aliwafanya hai pamoja naye na kutusamehe makosa yetu yote.
14 delens quod adversus nos erat chirographum decreti, quod erat contrarium nobis, et ipsum tulit de medio, affigens illud cruci:
Alifuta kumbukumbu ya madeni iliyoandikwa, na taratibu zilizokuwa kinyume nasi. Aliiondoa yote na kuigongomea msalabani.
15 et expolians principatus, et potestates traduxit confidenter, palam triumphans illos in semetipso.
Aliziondoa nguvu na mamlaka. Aliyaweka wazi na kuyafanya kuwa sherehe ya ushidi kwa njia ya msalaba wake.
16 Nemo ergo vos iudicet in cibo, aut in potu, aut in parte diei festi, aut neomeniae, aut sabbatorum:
Kwa hiyo, mtu yeyote asiwahukumu ninyi katika kula au katika kunywa, au kuhusu siku ya sikukuu au mwezi mpya, au siku za Sabato.
17 quae sunt umbra futurorum: corpus autem Christi.
Hivi ni vivuli vya mambo yajayo, lakini kiini ni Kristo.
18 Nemo vos seducat, volens in humilitate, et religione angelorum, quae non vidit ambulans, frustra inflatus sensu carnis suae,
Mtu awaye yote asinyang'anywe tuzo yake kwa kutamani unyenyekevu na kwa kuabudu malaika. Mtu wa jinsi hiyo huingia katika mambo aliyoyaona na kushawishiwa na mawazo yake ya kimwili.
19 et non tenens caput, ex quo totum corpus per nexus, et coniunctiones subministratum, et constructum crescit in augmentum Dei.
Yeye hakishikilii kichwa. Ni kutoka katika kichwa kwamba mwili wote kupitia viungo vyake na mifupa huungwa na kushikamanishwa kwa pamoja; na hukua kwa ukuaji utolewao na Mungu.
20 Si ergo mortui estis cum Christo ab elementis huius mundi: quid adhuc tamquam viventes in mundo decernitis?
Ikiwa mlikufa pamoja na Kristo kwa tabia za dunia, mbona mnaishi kama mnawajibika kwa dunia:
21 Ne tetigeritis, neque gustaveritis, neque contrectaveritis:
“Msishike, wala kuonja, wala kugusa”?
22 quae sunt omnia in interitum ipso usu, secundum praecepta, et doctrinas hominum:
Haya yote yameamuriwa kwa ajili ya uharibifu ujao na matumizi, kutokana na maelekezo na mafundisho ya wanadamu.
23 quae sunt rationem quidem habentia sapientiae in superstitione, et humilitate, et non ad parcendum corpori, non in honore aliquo ad saturitatem carnis.
Sheria hizi zina hekima ya dini zilizotengenezwa kwa ubinafsi na unyenyekevu na mateso ya mwili. Lakini hazina thamani dhidi ya tamaa za mwili.

< Colossenes 2 >