< Psalmorum 20 >

1 In finem, Psalmus David. Exaudiat te Dominus in die tribulationis: protegat te nomen Dei Iacob.
Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. Mungu akusaidie wakati wa shida; na jina la Mungu wa Yakobo likulinde
2 Mittat tibi auxilium de sancto: et de Sion tueatur te.
na kutuma msaada kutoka mahali patakatifu kwa ajili ya kukutegemeza wewe kutoka Sayuni.
3 Memor sit omnis sacrificii tui: et holocaustum tuum pingue fiat.
Naye akumbuke sadaka yako yote na kuipokea sadaka ya kuteketezwa.
4 Tribuat tibi secundum cor tuum: et omne consilium tuum confirmet.
Naye akujalie haja za moyo wako na kutimiza mipango yako yote.
5 Lætabimur in salutari tuo: et in nomine Dei nostri magnificabimur.
Ndipo tutakapo shangilia katika ushindi wako, na, katika jina la Mungu wetu, tutapeperusha bendera. Yahwe naakupe maombi yako yote ya haki.
6 Impleat Dominus omnes petitiones tuas: nunc cognovi quoniam salvum fecit Dominus CHRISTUM suum. Exaudiet illum de cælo sancto suo: in potentatibus salus dexteræ eius.
Sasa ninajua ya kuwa Yahwe atawaokoa wapakwa mafuta wake; yeye atamjibu yeye kutoka katika mbingu takatifu kwa uweza wa mkono wake wa kuume ambao waweza kumuokoa yeye.
7 Hi in curribus, et hi in equis: nos autem in nomine Domini Dei nostri invocabimus.
Baadhi hamini katika magari na wengine katika farasi, lakini sisi tumuita Yahwe Mungu wetu.
8 Ipsi obligati sunt, et ceciderunt: nos autem surreximus et erecti sumus.
Wao watashushwa chini na kuanguka, bali sisi tutainuka na kusimama wima!
9 Domine salvum fac regem: et exaudi nos in die, qua invocaverimus te.
Yahwe, umuokoe mfalme; utusaidie sisi tukuitapo.

< Psalmorum 20 >