< Iohannem 7 >

1 Post hæc autem ambulabat Iesus in Galilæam, non enim volebat in Iudæam ambulare: quia quærebant eum Iudæi interficere.
Na baada ya mambo haya Yesu alisafiri hivi katika Galilaya, kwa sababu hakupenda kwenda Uyahudi kwa sababu wayahudi walikuwa wakifanya mipango ya kumwua.
2 Erat autem in proximo dies festus Iudæorum, Scenopegia.
Sasa sikukuu ya Wayahudi, sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu.
3 Dixerunt autem ad eum fratres eius: Transi hinc, et vade in Iudæam, ut et discipuli tui videant opera tua, quæ facis.
Ndipo ndugu zake walipomwambia, “Ondoka mahali hapa uende Uyahudi, ili kwamba wanafunzi wako vile vile wayaone matendo ufanyayo.
4 Nemo quippe in occulto quid facit, et quærit ipse in palam esse: si hæc facis, manifesta teipsum mundo.
Hakuna afanyaye lolote kwa siri iwapo yeye mwenyewe anataka kujulikana wazi. Iwapo unafanya mambo haya, jionyeshe mwenyewe kwa ulimwengu.”
5 Neque enim fratres eius credebant in eum.
Hata ndugu zake pia hawakumwamini.
6 Dicit ergo eis Iesus: Tempus meum nondum advenit: tempus autem vestrum semper est paratum.
Ndipo Yesu alipowaambia, “Wakati wangu haujafika bado, lakini wakati wenu kila mara uko tayari.
7 Non potest mundus odisse vos: me autem odit: quia ego testimonium perhibeo de illo quod opera eius mala sunt.
Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, bali unanichukia mimi kwa sababu ninaushuhudia kuwa matendo yake ni maovu.
8 Vos ascendite ad diem festum hunc, ego autem non ascendo ad diem festum istum: quia meum tempus nondum impletum est.
Pandeni kwenda katika sikukuu; mimi siendi katika sikukuu hii kwa sababu muda wangu haujakamilika bado.”
9 Hæc cum dixisset, ipse mansit in Galilæa.
Baada ya kusema mambo hayo kwao, alibaki Galilaya.
10 Ut autem ascenderunt fratres eius, tunc et ipse ascendit ad diem festum non manifeste, sed quasi in occulto.
Hata hivyo, ndugu zake walipokuwa wamekwenda katika sikukuu, ndipo naye alienda, siyo kwa wazi bali kwa siri.
11 Iudæi ergo quærebant eum in die festo, et dicebant: Ubi est ille?
Wayahudi walikuwa wakimtafuta katika sikukuu na kusema, “Yuko wapi?”
12 Et murmur multum erat in turba de eo. Quidam enim dicebant: Quia bonus est. Alii autem dicebant: Non, sed seducit turbas.
Kulikuwa na majadiliano mengi miongoni mwa makutano juu yake. Wengine walisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walisema, “Hapana, huwapotosha makutano.”
13 Nemo tamen palam loquebatur de illo propter metum Iudæorum.
Hata hivyo hakuna aliyezungumza wazi juu yake kwa kuwaogopa Wayahudi.
14 Iam autem die festo mediante, ascendit Iesus in templum, et docebat.
Wakati sikukuu ilipofika katikati, Yesu alipanda kwenda Hekaluni na kuanza kufundisha.
15 Et mirabantur Iudæi, dicentes: Quomodo hic litteras scit, cum non didicerit?
Wayahudi walikuwa wakishangaa na kusema, “Kwa jinsi gani mtu huyu anajua mambo mengi? Hajasoma kamwe.”
16 Respondit eis Iesus, et dixit: Mea doctrina non est mea, sed eius, qui misit me.
Yesu akawajibu na kuwaambia, “Mafundisho yangu siyo yangu, bali ni yake yeye aliyenituma.
17 Si quis voluerit voluntatem eius facere: cognoscet de doctrina, utrum ex Deo sit, an ego a me ipso loquar.
Iwapo yeyote atapenda kufanya mapenzi yake yeye, atajua kuhusu mafundisho haya, kama yanatoka kwa Mungu, au kama ninazungumza kutoka kwangu mwenyewe.
18 Qui a semetipso loquitur, gloriam propriam quærit. Qui autem quærit gloriam eius, qui misit eum, hic verax est, et iniustitia in illo non est.
Kila anayezungumza yatokayo kwake mwenywe hutafuta utukufu wake, bali kila atafutaye utukufu wake yeye aliyemtuma, mtu huyo ni wa kweli, na ndani yake hakuna kutotenda haki.
19 Nonne Moyses dedit vobis legem: et nemo ex vobis facit legem?
Musa hakuwapa nyinyi sheria? Lakini hakuna hata mmoja kati yenu atendaye sheria. Kwa nini mnataka kuniua?
20 Quid me quæritis interficere? Respondit turba, et dixit: Dæmonium habes: quis te quæret interficere?
Makutano wakajibu, “Una pepo. Nani anataka kukuua?”
21 Respondit Iesus, et dixit eis: Unum opus feci, et omnes miramini:
Yesu akajibu na akawaambia, “Nimetenda kazi moja, nanyi nyote mmeshangazwa kwa sababu yake.
22 Propterea Moyses dedit vobis circumcisionem: (non quia ex Moyse est, sed ex patribus) et in Sabbato circumciditis hominem.
Musa aliwapa tohara (siyo kwamba inatoka kwa Musa, bali ile inatoka kwa mababa), na katika Sabato mnamtahili mtu.
23 Si circumcisionem accipit homo in Sabbato, ut non solvatur lex Moysi: mihi indignamini quia totum hominem sanum feci in Sabbato?
Iwapo mtu atapokea tohara katika siku ya Sabato ili kwamba sheria ya Musa isivunjwe, kwa nini mnanikasirikia mimi kwa sababu nimemfanya mtu kuwa mzima kabisa katika Sabato?
24 Nolite iudicare secundum faciem, sed iustum iudicium iudicate.
Msihukumu kulingana na mwonekano, bali hukumuni kwa haki.
25 Dicebant ergo quidam ex Ierosolymis: Nonne hic est, quem quærunt interficere?
Baadhi yao kutoka Yerusalemu wakasema, “Siye huyu wanayemtafuta kumwua?
26 Et ecce palam loquitur, et nihil ei dicunt. Numquid vere cognoverunt principes quia hic est Christus?
Na tazama, anaongea wazi wazi, na hawasemi chochote juu yake. Haiwezi ikawa kwamba viongozi wanajua kweli kuwa huyu ni Kristo, inaweza kuwa?
27 Sed hunc scimus unde sit: Christus autem cum venerit, nemo scit unde sit.
Tunajua huyu mtu anatokea wapi. Kristo atakapokuja, hata hivyo, hakuna atakayejua wapi anakotoka.”
28 Clamabat ergo Iesus in templo docens, et dicens: Et me scitis, et unde sim scitis: et a me ipso non veni, sed est verus, qui misit me, quem vos nescitis.
Yesu alikuwa akipaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema, “Ninyi nyote mnanijua mimi na mnajua nitokako. Sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye aliyenituma ni wa kweli, na hamumjui yeye.
29 Ego scio eum: quia ab ipso sum, et ipse me misit.
Ninamjua yeye kwa sababu nimetoka kwake na alinituma.”
30 Quærebant ergo eum apprehendere: et nemo misit in illum manus, quia nondum venerat hora eius.
Walikuwa wanajaribu kumkamata, lakini hakuna hata mmoja aliyeinua mkono wake juu yake kwa sababu saa yake ilikuwa bado haijafika.
31 De turba autem multi crediderunt in eum, et dicebant: Christus cum venerit, numquid plura signa faciet quam quæ hic facit?
Hata hivyo, wengi katika makutano walimwamini. Walisema, “Kristo atakapokuja, atafanya ishara nyingi kuliko alizofanya mtu huyu?”
32 Audierunt Pharisæi turbam murmurantem de illo hæc: et miserunt principes, et Pharisæi ministros ut apprehenderent eum.
Mafarisayo waliwasikia makutano wakinong'onezana mambo haya kuhusu Yesu, na wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakatuma maafisa ili kumkamata.
33 Dixit ergo eis Iesus: Adhuc modicum tempus vobiscum sum: et vado ad eum, qui me misit.
Ndipo Yesu aliposema, “Bado kuna muda kitambo niko pamoja nanyi, na baadaye nitakwenda kwake yeye aliyenituma.
34 Quæretis me, et non invenietis: et ubi ego sum, vos non potestis venire.
Mtanitafuta wala hamtaniona; kule niendako, hamtaweza kuja.”
35 Dixerunt ergo Iudæi ad semetipsos: Quo hic iturus est, quia non inveniemus eum? Numquid in dispersionem Gentium iturus est, et docturus Gentes?
Kwa hiyo Wayahudi wakasemezana wao kwa wao, “Mtu huyu atakwenda wapi kwamba tusiweze kumuona? Ataenda kwa Waliotawanyika kati ya Wayunani na kuwafundisha Wayunani?
36 Quis est hic sermo, quem dixit: Quæretis me, et non invenietis: et ubi sum ego, vos non potestis venire?
Ni neno gani hili alilolisema, 'Mtanitafuta wala hamtaniona; kule niendako hamtamweza kuja'?”
37 In novissimo autem die magno festivitatis stabat Iesus, et clamabat, dicens: Si quis sitit, veniat ad me, et bibat.
Sasa katika siku ya mwisho, siku kubwa ya sikukuu, Yesu alisimama akapaza sauti, akisema, “Ikiwa yeyote ana kiu, na aje kwangu anywe.
38 Qui credit in me, sicut dicit Scriptura, flumina de ventre eius fluent aquæ vivæ.
Yeye aniaminiye mimi, kama maandiko yalivyosema, kutoka ndani yake itatiririka mito ya maji ya uzima.”
39 Hoc autem dixit de Spiritu, quem accepturi erant credentes in eum: nondum enim erat Spiritus datus, quia Iesus nondum erat glorificatus.
Lakini aliyasema haya kuhusu Roho, ambaye wao wamwaminio watampokea; Roho alikuwa bado hajatolewa kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa bado.
40 Ex illa ergo turba cum audissent hos sermones eius, dicebant: Hic est vere Propheta.
Baadhi ya makutano, waliposikia maneno haya, walisema, “Kweli huyu ni nabii.”
41 Alii dicebant: Hic est Christus. Quidam autem dicebant: Numquid a Galilæa venit Christus?
Wengine walisema, “Huyu ni Kristo.” Lakini wengine walisema, “nini, Kristo aweza kutoka Galilaya?
42 Nonne Scriptura dicit: Quia ex semine David, et de Bethlehem castello, ubi erat David, venit Christus?
Maandiko hayajasema kuwa Kristo atatokea katika ukoo wa Daudi na kutoka Bethlehemu, kijiji ambacho Daudi alikuwa?
43 Dissensio itaque facta est in turba propter eum.
Hivyo, pale ukainuka mgawanyiko katikati ya makutano kwa ajili yake.
44 Quidam autem ex ipsis volebant apprehendere eum: sed nemo misit super eum manus.
Wengine kati yao wangelimkamata, lakini hakuna aliyenyoosha mikono yake juu yake.
45 Venerunt ergo ministri ad Pontifices, et Pharisæos. Et dixerunt eis illi: Quare non adduxistis illum?
Ndipo wale maofisa wakarudi kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, nao wakawaambia, “Kwa nini hamjamleta?”
46 Responderunt ministri: Numquam sic locutus est homo, sicut hic homo.
Maofisa wakajibu, “Hakuna mtu aliyewahi kuzungumza kama huyu kabla.”
47 Responderunt ergo eis Pharisæi: Numquid et vos seducti estis?
Ndipo Mafarisayo walipowajibu, “Na nyinyi pia mmepotoshwa?
48 Numquid ex principibus aliquis credidit in eum, aut ex Pharisæis?
Kuna yeyote kati ya watawala anayemwamini, au yeyote wa Mafarisayo?
49 Sed turba hæc, quæ non novit legem, maledicti sunt.
Bali hawa makutano wasiojua sheria - wamelaaniwa.”
50 Dixit Nicodemus ad eos, ille, qui venit ad eum nocte, qui unus erat ex ipsis:
Nikodemo akawaambia (yeye aliyemwendea Yesu zamani, akiwa mmoja wa Mafarisayo),
51 Numquid lex nostra iudicat hominem, nisi prius audierit ab ipso, et cognoverit quid faciat?
“Je sheria yetu inamhukumu mtu isipokuwa amesikilizwa kwanza na kujua anachokifanya?”
52 Responderunt, et dixerunt ei: Numquid et tu Galilæus es? Scrutare Scripturas, et vide quia a Galilæa propheta non surgit.
Walijibu na kumwambia, “Na wewe pia unatokea Galilaya? Tafuta na uone kwamba hakuna nabii aliyetokea Galilaya.”
53 Et reversi sunt unusquisque in domum suam.
(Zingatia: Baadhi ya maneno ya Yohana 7: 53 - 8: 11 hayamo katika nakala bora za kale). Kisha kila mtu alienda nyumbani kwake.

< Iohannem 7 >