< Iohannem 14 >

1 Non turbetur cor vestrum. Creditis in Deum, et in me credite.
“Usiruhusu moyo wako kuwa katika mahangaiko. Unamwamini Mungu niamini pia na mimi.
2 In domo Patris mei mansiones multæ sunt. Si quo minus dixissem vobis: Quia vado parare vobis locum.
Katika nyumba ya Baba yangu kuna makazi mengi ya kukaa; kama isingekuwa hivyo, ningekuwa nimekuambia, kwa vile ninakwenda kukuandalia mahali kwa ajili yako.
3 Et si abiero, et præparavero vobis locum: iterum venio, et accipiam vos ad meipsum, ut ubi sum ego, et vos sitis.
Kama nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena kuwakaribisha kwangu, ili mahali nilipo pia nanyi muwepo.
4 Et quo ego vado scitis, et viam scitis.
Mnajua njia mahali ninakoenda.”
5 Dicit ei Thomas: Domine, nescimus quo vadis: et quo modo possumus viam scire?
Tomaso alimwambia Yesu, “Bwana, hatujui mahali unakoenda; Je! Tunawezaje kuijua njia?
6 Dicit ei Iesus: Ego sum via, et veritas, et vita. Nemo venit ad Patrem, nisi per me.
Yesu alimwambia, “Mimi ndiye njia, kweli, na uzima; hakuna awezaye kuja kwa Baba isipokuwa kupitia kwangu.
7 Si cognovissetis me, et Patrem meum utique cognovissetis: et amodo cognoscetis eum, et vidistis eum.
Kama mngeli nijua mimi, mngalikuwa mnamjua na Baba yangu pia; kuanzia sasa na kuendelea mnamjua na mmeshamuona yeye.”
8 Dicit ei Philippus: Domine, ostende nobis Patrem, et sufficit nobis.
Philipo alimwambia Yesu, “Bwana, tuonyeshe Baba, na hivyo itakuwa imetutosha.”
9 Dicit ei Iesus: Tanto tempore vobiscum sum: et non cognovistis me? Philippe, qui videt me, videt et Patrem. Quomodo tu dicis: Ostende nobis Patrem?
Yesu akamwambia, “Sijakuwa pamoja nanyi kwa muda mrefu, na bado hunijui mimi, Philipo? Yeyote aliyeniona mimi amemwona Baba; Jinsi gani unasema, 'Tuonyeshe Baba'?
10 Non creditis quia ego in Patre, et Pater in me est? Verba, quæ ego loquor vobis, a me ipso non loquor. Pater autem in me manens, ipse fecit opera.
Hamuamini kuwa mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Maneno ninayoyasema kwenu sisemi kwa kusudi langu mwenyewe; badala yake, ni Baba anayeishi ndani yangu anayetenda kazi yake.
11 Non creditis quia ego in Patre, et Pater in me est?
Niamini mimi, kwamba niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani yangu; kadhalika niamini mimi kwa sababu ya kazi zangu hasa.
12 Alioquin propter opera ipsa credite. Amen, amen dico vobis, qui credit in me, opera, quæ ego facio, et ipse faciet, et maiora horum faciet: quia ego ad Patrem vado.
Amini, amini, nawaambia, yeye aniaminiye, mimi kazi zile nizifanyazo, atazifanya kazi hizi pia; na atafanya hata kazi kubwa kwasababu ninakwenda kwa Baba.
13 Et quodcumque petieritis Patrem in nomine meo, hoc faciam: ut glorificetur Pater in Filio.
Chochote mkiomba katika jina langu, nitafanya ili kwamba Baba aweze kutukuzwa katika Mwana.
14 Si quid petieritis me in nomine meo, hoc faciam.
Kama mkiomba kitu chochote katika jina langu, hilo nitafanya.
15 Si diligitis me: mandata mea servate.
Kama mkinipenda, mtazishika amri zangu.
16 Et ego rogabo Patrem, et alium Paraclitum dabit vobis, ut maneat vobiscum in æternum, (aiōn g165)
Na nitamwomba Baba, Naye atawapa Msaidizi mwingine ili kwamba aweze kuwa pamoja nanyi milele, (aiōn g165)
17 Spiritum veritatis, quem mundus non potest accipere, quia non videt eum, nec scit eum. Vos autem cognoscetis eum: quia apud vos manebit, et in vobis erit.
Roho wa kweli. Ulimwengu hauwezi kumpokea yeye kwa sababu haumuoni, au kumjwa yeye. hata hivyo ninyi, mnamjua yeye, kwani anakaa pamoja nayi na atakuwa ndani yenu.
18 Non relinquam vos orphanos: veniam ad vos.
Sitawaacha peke yenu; Nitarudi kwenu.
19 Adhuc modicum: et mundus me iam non videt. Vos autem videtis me: quia ego vivo, et vos vivetis.
Kwa muda kitambo, ulimwengu hautaniona tena, lakini ninyi mwaniona. Kwa sababu ninaishi, nanyi mtaishi pia.
20 In illo die vos cognoscetis quia ego sum in Patre meo, et vos in me, et ego in vobis.
Katika siku hiyo mtajua kwamba mimi niko ndani ya Baba, na kwamba ninyi mko ndani yangu, na kwamba mimi niko ndani yenu.
21 Qui habet mandata mea, et servat ea: ille est, qui diligit me. Qui autem diligit me, diligetur a Patre meo: et ego diligam eum, et manifestabo ei meipsum.
Yeyote azishikaye amri zangu na kuzitenda, ndiye mmoja ambaye anipenda mimi; na ambaye anipenda mimi atapendwa na Baba yangu, na Nitampenda na nitajionyesha mimi mwenyewe kwake.”
22 Dicit ei Iudas, non ille Iscariotes: Domine, quid factum est, quia manifestaturus es nobis tepisum, et non mundo?
Yuda (siyo Iskariote) akamwambia Yesu, “Bwana, Je! Ni nini kinatokea kwamba utajionyesha mwenyewe kwetu na siyo kwa ulimwengu?
23 Respondit Iesus, et dixit ei: Si quis diligit me, sermonem meum servabit, et Pater meus diliget eum, et ad eum veniemus, et mansionem apud eum faciemus:
Yesu alijibu akamwambia, “Kama yeyote danipendaye, atalishika neno langu. Baba yangu atampenda, na tutakuja kwake na tutafanya makao yetu pamoja naye.
24 qui non diligit me, sermones meos non servat. Et sermonem, quem audistis, non est meus: sed eius, qui misit me, Patris.
Yeyote ambaye hanipendi mimi, hashiki maneno yangu. Neno ambalo mnasikia siyo langu bali la Baba ambaye alinituma.
25 Hæc locutus sum vobis apud vos manens.
Nimeyasema mambo haya kwenu, wakati bado ninaishi miongoni mwenu.
26 Paraclitus autem Spiritus Sanctus, quem mittet Pater in nomine meo, ille vos docebit omnia, et suggeret vobis omnia, quæcumque dixero vobis.
Hata hivyo, Mfariji, Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisha mambo yote na atawafanya mkumbuke yote ambayo niliyasema kwenu.
27 Pacem relinquo vobis, pacem meam do vobis: non quomodo mundus dat, ego do vobis. Non turbetur cor vestrum, neque formidet.
Amani nawapa amani yangu ninyi. Siwapi hii kama ulimwengu utoavyo. Msiifanye mioyo yenu kuwa na mahangaiko, na woga.
28 Audistis quia ego dixi vobis: Vado, et venio ad vos. Si diligeretis me, gauderetis utique, quia vado ad Patrem: quia Pater maior me est.
Mlisikia vile nilivyowaambia, 'Ninaenda zangu, na nitarudi kwenu.' Kama mngelinipenda mimi, mngekuwa na furaha kwa sababu ninakwenda kwa Baba, kwa kuwa Baba ni mkuu kuliko mimi.
29 Et nunc dixi vobis priusquam fiat: ut cum factum fuerit, credatis.
Sasa nimekwisha kuwaambia kabla haijatokea ili kwamba, wakati ikitokea, mweze kuamini.
30 Iam non multa loquar vobiscum. Venit enim princeps mundi huius, et in me non habet quidquam.
Sitaongea nanyi maneno mengi, kwa kuwa mkuu wa dunia hii anakuja. Yeye hana nguvu juu yangu,
31 Sed ut cognoscat mundus quia diligo Patrem, et sicut mandatum dedit mihi Pater, sic facio. Surgite, eamus hinc.
lakini ili kwamba ulimwengu upate kujua kwamba nampenda Baba, nafanya ambacho Baba ananiagiza mimi, kama vile alivyonipa amri. Inukeni, na tutoke mahali hapa.

< Iohannem 14 >