< Galatas 6 >

1 Fratres, et si præoccupatus fuerit homo in aliquo delicto, vos, qui spirituales estis, huiusmodi instruite in spiritu lenitatis, considerans te ipsum, ne et tu tenteris.
Ndugu, ikiwa mtu amekamatwa katika uovu, ninyi mlio wa kiroho, mnawiwa kumrejesha huyo ndugu katika roho ya upole. Huku mkijiangalia wenyewe ili msijaribiwe.
2 Alter alterius onera portate, et sic adimplebitis legem Christi.
Mchukuliane mizigo, na kwa hiyo mtaikamilisha sheria ya Kristo.
3 Nam si quis existimat se aliquid esse, cum nihil sit, ipse se seducit.
Ikiwa mtu yeyote anajiona ni bora wakati si kitu, anajidanganya mwenyewe.
4 Opus autem suum probet unusquisque, et sic in semetipso tantum gloriam habebit, et non in altero.
Kila mmoja na aipime kazi yake. Kisha atakuwa na kitu mwenyewe peke yake cha kujisifu, bila kujilinganisha mwenyewe na mtu yeyote.
5 Unusquisque enim onus suum portabit.
Maana kila mtu atachukua mzigo wake mwenyewe.
6 Communicet autem is, qui catechizatur Verbo, ei, qui se catechizat, in omnibus bonis.
Mtu aliyefundishwa neno lazima amshirikishe mazuri yote mwalimu wake.
7 Nolite errare: Deus non irridetur. Quæ enim seminaverit homo, hæc et metet.
Msidanganyike. Mungu hadhihakiwi. Kila apandacho mtu, ndicho atakachovuna pia.
8 Quoniam qui seminat in carne sua, de carne et metet corruptionem: qui autem seminat in spiritu, de spiritu metet vitam æternam. (aiōnios g166)
Kila apandaye mbegu katika asili yake ya dhambi atavuna uharibifu, lakini yeye apandaye mbegu katika Roho, atavuna uzima wa milele kutoka kwa Roho. (aiōnios g166)
9 Bonum autem facientes, non deficiamus: tempore enim suo metemus non deficientes.
Tusichoke katika kutenda mema, maana kwa wakati wake tutavuna ikiwa hatutakata tamaa.
10 Ergo dum tempus habemus, operemur bonum ad omnes, maxime autem ad domesticos fidei.
Hivyo basi, wakati tutakapokuwa na nafasi, tutende mema kwa kila mmoja. Tutende mema zaidi hasa kwa walio ndani ya imani.
11 Videte qualibus litteris scripsi vobis mea manu.
Angalieni ukubwa wa barua nilizowaandikia kwa mkono wangu mwenyewe.
12 Quicumque enim volunt placere in carne, hi cogunt vos circumcidi, tantum ut crucis Christi persecutionem non patiantur.
Wale wanaotaka kufanya mema kwa mtazamo wa mwili ndiyo wenye kuwalazimisha mtahiriwe. Wanafanya hivyo kwa sababu wasiingie kwenye mateso ya msalaba wa Kristo.
13 Neque enim qui circumciduntur, legem custodiunt: sed volunt vos circumcidi, ut in carne vestra glorientur.
Maana hata hao waliotahiriwa wenyewe hawaishiki sheria. Badala yake wanataka ninyi mtahiriwe ili waweze kujivunia miili yenu.
14 Mihi autem absit gloriari, nisi in cruce Domini nostri Iesu Christi: per quem mihi mundus crucifixus est, et ego mundo.
Isitokee nikajivuna isipokuwa kwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Ni katika yeye ulimwengu umesulubiwa kwangu na mimi katika ulimwengu.
15 In Christo enim Iesu neque circumcisio aliquid valet, neque præputium, sed nova creatura.
Kwa kuwa haijalishi kutahiriwa au kutokutahiriwa kuwa ni kitu. Badala yake uzao mpya ni muhimu.
16 Et quicumque hanc regulam secuti fuerint, pax super illos, et misericordia, et super Israel Dei.
Kwa wote wenye kuishi kwa kanuni hii, wawe na amani na rehema iwe juu yao wote, na juu ya Israel ya Mungu.
17 De cetero nemo mihi molestus sit: ego enim stigmata Domini Iesu in corpore meo porto.
Tangu sasa mtu yeyote asinitaabishe, maana nimebeba chapa za Yesu mwilini mwangu.
18 Gratia Domini nostri Iesu Christi, cum spiritu vestro, fratres. Amen.
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe na roho zenu, ndugu. Amina.

< Galatas 6 >