< Galatas 2 >

1 Deinde post annos quattuordecim, iterum ascendi Ierosolymam cum Barnaba, assumpto et Tito.
Baada ya miaka kumi na nne nilienda tena Yerusalemu pamoja na Barnaba. Pia nilimchukua Tito pamoja nami.
2 Ascendi autem secundum revelationem: et contuli cum illis Evangelium, quod prædico in Gentibus, seorsum autem iis, qui videbantur aliquid esse: ne forte in vacuum currerem, aut cucurrissem.
Nilienda kwa sababu Mungu alijidhihirisha kwangu kwamba nilipaswa kwenda. Niliweka mbele yao Injili ambayo niliitangaza kwa watu wa mataifa. (Lakini niliongea kwa siri kwa waliosemekana kuwa viongozi muhimu). Nilifanya hivi ili kuhakikisha kwamba nilikuwa sikimbii, au nilikimbia bure.
3 Sed neque Titus, qui mecum erat, cum esset Gentilis, compulsus est circumcidi:
Lakini hata Tito, aliyekuwa pamoja nami, aliyekuwa Myunani, alilazimishwa kutahiriwa.
4 sed propter subintroductos falsos fratres, qui subintroierunt explorare libertatem nostram, quam habemus in Christo Iesu, ut nos in servitutem redigerent.
Jambo hili lilitokea kwa sababu ya ndugu wa uongo waliokuja kwa siri kupeleleza uhuru tuliokuwa nao katika Kristo Yesu. Walitamani kutufanya sisi kuwa watumwa wa sheria.
5 Quibus neque ad horam cessimus subiectione, ut veritas Evangelii permaneat apud vos:
Hatukujitoa kuwatii hata kwa saa moja, ili kwamba injili ya kweli ibaki bila kubadilika kwenu.
6 ab iis autem, qui videbantur esse aliquid, (quales aliquando fuerint, nihil mea interest. Deus personam hominis non accipit) mihi enim qui videbantur esse aliquid, nihil contulerunt.
Lakini wale waliosemwa kuwa walikuwa viongozi hawakuchangia chochote kwangu. Chochote walichokuwa wakikifanya hakikuwa na maana kwangu. Mungu hakubali upendeleo wa wanadamu.
7 Sed econtra cum vidissent quod creditum est mihi Evangelium præputii, sicut et Petro circumcisionis:
Badala yake, waliniona kwamba nimeaminiwa kuitangaza injili kwa wale ambao hawakutahiriwa. Ilikuwa kama Petro atangaze injili kwa waliotahiriwa.
8 (qui enim operatus est Petro in Apostolatum circumcisionis, operatus est et mihi inter Gentes)
Kwa maana Mungu, aliyefanya kazi ndani ya Petro kwa ajili ya utume kwa wale waliotahiriwa, pia alifanya kazi ndani yangu kwa watu wa mataifa.
9 et cum cognovissent gratiam, quæ data est mihi, Iacobus, et Cephas, et Ioannes, qui videbantur columnæ esse, dextras dederunt mihi, et Barnabæ societatis: ut nos in Gentes, ipsi autem in circumcisionem:
Wakati Yakobo, Kefa, na Yohana, waliotambulika kuwa waliojenga Kanisa, walifahamu neema niliyopewa mimi, walitupokea katika ushirika mimi na Barnaba. Walifanya hivi ili kwamba twende kwa watu wa mataifa, na ili kwamba waweze kwenda kwa wale waliotahiriwa.
10 tantum ut pauperum memores essemus, quod etiam solicitus fui hoc ipsum facere.
Pia walitutaka sisi kuwakumbuka masikini. Mimi pia nilikuwa natamani kufanya jambo hili.
11 Cum autem venisset Cephas Antiochiam: in faciem ei restiti, quia reprehensibilis erat.
Wakati Kefa alipokuja Antiokia, nilimpinga waziwazi kwa sababu alikuwa amekosea.
12 Prius enim quam venirent quidam a Iacobo, cum Gentibus edebat: cum autem venissent, subtrahebat, et segregabat se timens eos, qui ex circumcisione erant.
Kabla ya watu kadhaa kuja kutoka kwa Yakobo, Kefa alikuwa akila pamoja na watu wa mataifa. Lakini hawa watu walipokuja, aliacha na kuondoka kutoka kwa watu wa mataifa. Alikuwa anaogopa watu ambao walihitaji tohara.
13 Et simulationi eius consenserunt ceteri Iudæi, ita ut et Barnabas duceretur ab eis in illam simulationem.
Vilevile Wayahudi wengine waliungana na unafiki huu pamoja na Kefa. Matokeo yake yalikuwa kwamba hata Barnaba alichukuliwa na unafiki wao.
14 Sed cum vidissem quod non recte ambularent ad veritatem Evangelii, dixi Cephæ coram omnibus: Si tu, cum Iudæus sis, Gentiliter vivis, et non Iudaice: quomodo Gentes cogis Iudaizare?
Lakini nilipoona kwamba walikuwa hawafuati injili ya kweli, nilimwambia Kefa mbele yao wote, “Kama ninyi ni Wayahudi lakini mnaishi tabia za watu wa mataifa badala ya tabia za Kiyahudi, kwa nini mnawalazimisha watu wa mataifa kuishi kama Wayahudi?”
15 Nos natura Iudæi, et non ex Gentibus peccatores.
Sisi ambao ni Wayahudi kwa kuzaliwa na siyo “Watu wa mataifa wenye dhambi “
16 Scientes autem quod non iustificatur homo ex operibus legis, nisi per fidem Iesu Christi: et nos in Christo Iesu credimus, ut iustificemur ex fide Christi, et non ex operibus legis: propter quod ex operibus legis non iustificabitur omnis caro.
fahamu kwamba hakuna anayehesabiwa haki kwa matendo ya sheria. Badala yake, wanahesabiwa haki kwa imani ndani ya Yesu Kristo. Tulikuja kwa imani ndani ya Kristo Yesu ili kwamba tunahesabiwa haki kwa imani ndani ya Kristo na siyo kwa matendo ya sheria. Kwa matendo ya sheria hakuna mwili utakao hesabiwa haki.
17 Quod si quærentes iustificari in Christo, inventi sumus et ipsi peccatores, numquid Christus peccati minister est? Absit.
Lakini kama tunapomtafuta Mungu kwa kutuhesabia haki ndani ya Kristo, tunajikuta wenyewe pia kuwa wenye dhambi, je Kristo alifanywa mtumwa wa dhambi? Siyo hivyo!
18 Si enim quæ destruxi, iterum hæc ædifico: prævaricatorem me constituo.
Maana kama nikijenga tegemeo langu juu ya kutunza sheria, tegemeo ambalo nilikwisha liondoa, najionesha mwenyewe kuwa mvunja sheria.
19 Ego enim per legem, legi mortuus sum, ut Deo vivam: Christo confixus sum cruci.
Kupitia sheria nilikufa kwa sheria, kwa hiyo napaswa kuishi kwa ajili ya Mungu.
20 Vivo autem, iam non ego: vivit vero in me Christus. Quod autem nunc vivo in carne: in fide vivo Filii Dei, qui dilexit me, et tradidit semetipsum pro me.
Nimesulubiwa pamoja na Kristo. Si mimi tena ninayeishi, bali Kristo anaishi ndani yangu. Maisha ninayoishi katika mwili ninaishi kwa imani ndani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda na akajitoa kwa ajili yangu.
21 Non abiicio gratiam Dei. Si enim per legem iustitia, ergo gratis Christus mortuus est.
Siikani neema ya Mungu, maana kama haki ilikuwepo kupitia sheria, basi Kristo angekuwa amekufa bure.

< Galatas 2 >