< Exodus 35 >

1 Igitur congregata omni turba filiorum Israel, dixit ad eos: Hæc sunt quæ iussit Dominus fieri.
Musa akawakusanya jamii yote ya Waisraeli na kuwaambia, “Haya ndio mambo Yahweh aliyo waamuru mfanye.
2 Sex diebus facietis opus: septimus dies erit vobis sanctus, Sabbatum, et requies Domini: qui fecerit opus in eo, occidetur.
Kwa siku sita kazi ya weza fanywa, lakini kwako, siku ya saba lazima iwe siku takatifu, siku ya Sabato ya mapumziko, takatifu kwa Yahweh. Yeyote atakaye fanya kazi hiyo siku lazima auawe.
3 Non succendetis ignem in omnibus habitaculis vestris per diem Sabbati.
Haupaswi kuwasha moto kwenye nyumba zenu siku ya Sabato.”
4 Et ait Moyses ad omnem catervam filiorum Israel: Iste est sermo quem præcepit Dominus, dicens:
Musa akasema na jamii yote ya Waisraeli, kwa kusema, “Hichi ndicho kitu Yahweh alicho amuru.
5 Separate apud vos primitias Domino. Omnis voluntarius et prono animo offerat eas Domino: aurum et argentum, et æs,
Chukuwa sadaka kwa ajili ya Yahweh, wote wenye moyo mkunjufu. Leta sadaka kwa Yahweh - dhahabu, fedha, shaba,
6 hyacinthum et purpuram, coccumque bis tinctum, et byssum, pilos caprarum,
buluu, zambarau, sufu nyekundu na kitambaa kizuri; nywele za mbuzi;
7 pellesque arietum rubricatas, et ianthinas, ligna setim,
ngozi za kondoo zilizotiwa rangi nyekundu na ngozi za pomboo; na mbao za mshita;
8 et oleum ad luminaria concinnanda, et ut conficiatur unguentum, et thymiama suavissimum,
mafuta ya taa kwa pahali patakatifu, viungo vya manukato kwa hayo mafuta ya kutiwa,
9 lapides onychinos, et gemmas ad ornatum superhumeralis et rationalis.
kwa uvumba mzuri na vito vya shohamu na vito vya kutiwa kwa hiyo naivera, na kwa hicho kifuko cha kifuani.
10 Quisque vestrum sapiens est, veniat, et faciat quod Dominus imperavit:
Kila mwanaume mwenye ustadi kati yenu aje na afanye kila kitu ambacho Yahweh aliyaamuru —
11 Tabernaculum scilicet, et tectum eius, atque operimentum, annulos, et tabulata cum vectibus, paxillos et bases:
hema la kuabudia, na kifuniko chake, na vifungo vyake, na mbao zake, nguzo, na sakafu;
12 Arcam et vectes, propitiatorium, et velum, quod ante illud oppanditur:
pia sanduku na nguzo zake, kiti cha rehema, na pazia la kusitiri.
13 Mensam cum vectibus et vasis, et propositionis panibus:
Walileta meza na miguu yake, vyombo vyake vyote, na mkate wa wonyesho;
14 Candelabrum ad luminaria sustentanda, vasa illius et lucernas, et oleum ad nutrimenta ignium:
kinara cha taa, vyombo vyake, taa, na mafuta ya zile taa;
15 Altare thymiamatis, et vectes, et oleum unctionis et thymiama ex aromatibus: Tentorium ad ostium tabernaculi:
ile madhabahu ya uvumba na nguzo zake, mafuta ya upako na uvumba ulitiwa maukato; kishikizo cha mwingilio wa hema ya kuabudia;
16 Altare holocausti, et craticulam eius æneam cum vectibus et vasis suis: labrum et basim eius:
madhabahu ya sadaka ya kuteketeza na kitunzi cha shaba na nguzo na vyombo; na ile beseni kubwa na sakafu yake.
17 Cortinas atrii cum columnis et basibus, tentorium in foribus vestibuli,
Walileta vishikizo kwa ajili ya nyuani na nguzo zake na sakafu yake, na pazia kwa ajili mwingilio wa nyauni;
18 paxillos tabernaculi et atrii cum funiculis suis:
na ile misumari ya hema la kuabudia na nyuani, pamoja na kamba zake.
19 Vestimenta, quorum usus est in ministerio Sanctuarii, vestes Aaron pontificis ac filiorum eius, ut sacerdotio fungantur mihi.
Walileta mavazi yaliyofumwa kutumikia sehemu takatifu, mavazi takatifu ya Aruni kuhani na wanae, kwa wao kutumika kama makuhani.”
20 Egressaque omnis multitudo filiorum Israel de conspectu Moysi,
Kisha makabila yote ya Israeli yakaondoka na kwenda kutoka uweponi mwa Musa.
21 obtulerunt mente promptissima atque devota primitias Domino, ad faciendum opus tabernaculi testimonii. Quidquid ad cultum et ad vestes sanctas necessarium erat,
Kila mtu moyo wake ulimchochea na aliye andaliwa na roho yake alikuja na kuleta sadaka kwa Yahweh kwa matengenezo ya hema ya kuabudia, kwa vitu vyote kwajili ya huduma ndani yake, na kwa vazi takatifu.
22 viri cum mulieribus præbuerunt, armillas et inaures, annulos et dextralia: omne vas aureum in donaria Domini separatum est.
Walikuja, wote wanaume kwa wanawake, wote waliokuwa na moyo wa utayari. Walileta madini, hereni, pete, na vitu vya thamani, vitu vyote tofauti vyenye madini ya dhahabu. Waliwasilisha sadaka za dhahabu kama sadaka ya kupunga kwa Yahweh.
23 Si quis habebat hyacinthum, et purpuram, coccumque bis tinctum, byssum et pilos caprarum, pelles arietum rubricatas, et ianthinas,
Kila mmoja alikuwa na sufu ya buluu, dhambarau, au nyekundu, nguo nzuri, singa za mbuzi, ngozi za kondoo zilizobadili kuwa nyekundu, na ngozi ya pomboo walivileta.
24 argenti, ærisque metalla obtulerunt Domino, lignaque setim in varios usus.
kila mmoja alitengeneza sadaka ya fedha au shaba walizileta kama sadaka kwa Yahweh, na kila mmoja aliyekuwa na mti wa mshita kwa matumizi ya kazi aliuleta.
25 Sed et mulieres doctæ, quæ neverant, dederunt hyacinthum, purpuram, et vermiculum, ac byssum,
kila mwanamke mwenye ustadi walisokota sufu kwa mikono yao na walileta sufu walizosokota za buluu, dhambarau, au sufu nyekundu, au nguo nzuri.
26 et pilos caprarum, sponte propria cuncta tribuentes.
Wanawake wote wenye mioyo iliyochochewa na walio na ustadi walisokota singa za mbuzi.
27 Principes vero obtulerunt lapides onychinos, et gemmas ad superhumerale et rationale,
Viongozi walileta mawe ya shohamu na mawe mengine kwaajili ya kuwekwa kwenye hiyo naivera na hicho kifuko cha kifuani;
28 aromataque et oleum ad luminaria concinnanda, et ad præparandum unguentum, ac thymiama odoris suavissimi componendum.
walileta viungo na mafuta kwaajili ya taa, kwa mafuta ya upako, na kwa uvumba wa manukato.
29 Omnes viri et mulieres mente devota obtulerunt donaria, ut fierent opera quæ iusserat Dominus per manum Moysi. Cuncti filii Israel voluntaria Domino dedicaverunt.
Waisraeli walileta sadaka ya hiyari kwa Yahweh; kila mwanaume na mwanamke ambao mioyo yao ilikuwa tayari walileta vifaa kwaajili kazi zote ambazo Yahweh aliamuru kupitia Musa zifanyike.
30 Dixitque Moyses ad filios Israel: Ecce, vocavit Dominus ex nomine Beseleel filium Uri filii Hur de tribu Iuda.
Musa alisema kwa waisraeli, “Tazama, Yahweh ameita kwa jina juu ya Bezaleli mwana wa Uri mwana wa Huri, kutoka kabila la Yuda.
31 Implevitque eum Spiritu Dei, sapientia et intelligentia, et scientia et omni doctrina
Aliijaza Bezaleli kwa Roho yake, kumpa hekima, uwelewa, na maarifa, kwa aina zote za ujenzi,
32 ad excogitandum, et faciendum opus in auro et argento, et ære,
kufanya sanaa ya ubunifu na kufanya kazi za dhahabu, shaba, na shaba;
33 sculpendisque lapidibus, et opere carpentario. Quidquid fabre adinveniri potest,
pia kukata na kupanga mawe na mbao iliochongwa- kufanya kazi za aina zote kwa ubunifu na ujenzi.
34 dedit in corde eius: Ooliab quoque filium Achisamech de tribu Dan:
Aliiweka kufundisha ndani ya moyo wake, yeye pamoja na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, kutoka kabila la Dani.
35 ambos erudivit sapientia, ut faciant opera abietarii, polymitarii, ac plumarii de hyacintho ac purpura, coccoque bis tincto, et bysso, et texant omnia, ac nova quæque reperiant.
Aliwajaza kwa ustadi wa kufanya kazi za aina zote, kufanya kazi ya kama kuchora mawe, kama mwerevu, kama mtia taraza katika nyuzi za rangu ya buluu, dhambarau, na nyekundu na nguo nzuri, na kama washonaji. Walikuwa wachonga mawe wa kazi zote, na walikuwa wabunifu wa sanaa.

< Exodus 35 >