< Ephesios 2 >

1 Et vos, cum essetis mortui delictis, et peccatis vestris,
Kama vile mlivyo kuwa mmekufa katika makosa na dhambi zenu.
2 in quibus aliquando ambulastis secundum sæculum mundi huius, secundum principem potestatis aeris huius, spiritus, qui nunc operatur in filios diffidentiæ, (aiōn g165)
Ilikuwa katika haya kwamba kwanza mlienenda kulingana na nyakati za ulimwengu huu. Mlikuwa mkienenda kwa kufuata mtawala wa mamlaka ya anga. Hii ndiyo roho yake yule afanyaye kazi katika wana wa kuasi. (aiōn g165)
3 in quibus et nos omnes aliquando conversati sumus in desideriis carnis nostræ, facientes voluntatem carnis, et cogitationum, et eramus natura filii iræ, sicut et ceteri:
Sisi wote hapo mwanzo tulikuwa miongoni mwa hawa wasioamini. Tulikuwa tukitenda kwa namna ya tamaa mbaya za miili yetu. Tulikuwa tukifanya mapenzi ya mwili na ufahamu wetu. Tulikuwa kwa asili wana wa ghadhabu kama wengine.
4 Deus autem, qui dives est in misericordia, propter nimiam charitatem suam, qua dilexit nos,
Lakini Mungu ni mwingi wa rehema kwa sababu ya pendo lake kubwa alilotupenda sisi.
5 et cum essemus mortui peccatis, convivificavit nos in Christo, (cuius gratia estis salvati)
Wakati tulipokuwa wafu katika makosa yetu, alituleta pamoja katika maisha mapya ndani ya Kristo. Ni kwa neema kwamba mmeokolewa.
6 et conresuscitavit, et consedere fecit in cælestibus in Christo Iesu:
Mungu alitufufua pamoja na kutufanya kukaa pamoja katika mahali pa mbingu ndani ya Kristo Yesu.
7 ut ostenderet in sæculis supervenientibus abundantes divitias gratiæ suæ in bonitate super nos in Christo Iesu. (aiōn g165)
Alifanya hivi ili katika nyakati zijazo aweze kutuonesha utajiri mkuu wa neema yake. Hutuonesha sisi hili kwa njia ya wema wake ndani ya Kristo Yesu. (aiōn g165)
8 Gratia enim estis salvati per fidem, et hoc non ex vobis: Dei enim donum est,
Kwa neema mmeokolewa kwa njia ya imani. Na hii haikutoka kwetu. Ni zawadi ya Mungu.
9 non ex operibus, ut nequis glorietur.
Haitokani na matendo. Matokeo yake, asiwepo mmoja wapo wa kujisifu.
10 Ipsius enim sumus factura, creati in Christo Iesu in operibus bonis, quæ præparavit Deus ut in illis ambulemus.
Kwa sababu sisi tu kazi ya Mungu, tumeumbwa katika Kristo Yesu kutenda matendo mema. Ni matendo haya ambayo Mungu aliyapanga tangu zamani za kale kwa ajili yetu, ili tutembee katika hayo.
11 Propter quod memores estote, quod aliquando vos Gentes in carne, qui dicimini præputium ab ea, quæ dicitur circumcisio in carne, manu facta:
Kwa hiyo kumbukeni kwamba hapo zamani mlikuwa watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili. Mnaitwa “msio na tohara” kwa kile kinachoitwa tohara ya mwili inayofanywa kwa mikono ya binadamu.
12 quia eratis illo in tempore sine Christo, alienati a conversatione Israel, et hospites testamentorum, promissionis spem non habentes, et sine Deo in hoc mundo.
Kwa wakati huo mlikuwa mmetengwa na Kristo. Mlikuwa wageni kwa watu wa Israel. Mlikuwa wageni kwa agano la ahadi. Hamkuwa na uhakika wa wakati ujao. Mlikuwa bila Mungu katika ulimwengiu.
13 Nunc autem in Christo Iesu vos, qui aliquando eratis longe, facti estis prope in sanguine Christi.
Lakini sasa katika Kristo Yesu ninyi ambao hapo mwanzo mlikuwa mbali na Mungu mmeletwa karibu na Mungu kwa damu ya Kristo.
14 Ipse enim est pax nostra, qui fecit utraque unum, et medium parietem maceriæ solvens, inimicitias in carne sua:
Kwa maana yeye ndiye amani yetu. Alifanya wawili kuwa mmoja. Kwa mwili wake aliuharibu ukuta wa utengano ambao ulikuwa umetutenganisha, huo uadui.
15 legem mandatorum decretis evacuans, ut duos condat in semetipso in unum novum hominem, faciens pacem,
Kwamba alikomesha sheria ya amri na kanuni ili kwamba aumbe mtu mmoja mpya ndani yake. Akafanya amani.
16 et reconciliet ambos in uno corpore, Deo per crucem, interficiens inimicitias in semetipso.
Alifanya hivi ili kuwapatanisha makundi mawili ya watu kuwa mwili mmoja kwa Mungu kupitia msalaba. Kwa njia ya msalaba aliufisha uadui.
17 Et veniens evangelizavit pacem vobis, qui longe fuistis, et pacem iis, qui prope.
Yesu alikuja na kutangaza amani kwenu ninyi mliokuwa mbali na amani kwao wale waliokuwa karibu.
18 Quoniam per ipsum habemus accessum ambo in uno Spiritu ad Patrem.
Kwa maana kwa njia ya Yesu sisi wote wawili tuna nafasi kwa yule Roho mmoja kuingia kwa Baba.
19 Ergo iam non estis hospites, et advenæ: sed estis cives sanctorum, et domestici Dei:
Hivyo basi, ninyi watu wa mataifa si wasafiri na wageni tena. Bali ni wenyeji pamoja na wale waliotengwa kwa ajili ya Mungu na wajumbe katika nyumba ya Mungu.
20 superædificati super fundamentum Apostolorum, et Prophetarum, ipso summo angulari lapide Christo Iesu:
Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii. Kristo Yesu mwenyewe alikuwa jiwe kuu la pembeni.
21 in quo omnis ædificatio constructa crescit in templum sanctum in Domino,
Katika yeye jengo lote limeungamanishwa pamoja na kukua kama hekalu ndani ya Bwana.
22 in quo et vos coædificamini in habitaculum Dei in Spiritu.
Ni ndani yake ninyi nanyi mnajengwa pamoja kama mahali pa kuishi pa Mungu katika Roho.

< Ephesios 2 >