< Danihelis Prophetæ 9 >

1 In anno primo Darii filii Assueri de semine Medorum, qui imperavit super regnum Chaldæorum:
Dario mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi. Alikuwa na Ahasuero ambaye alifanywa mfalme juu ya ufalme wa watu wa Babeli.
2 Anno uno regni eius, ego Daniel intellexi in libris numerum annorum, de quo factus est sermo Domini ad Ieremiam prophetam, ut complerentur desolationis Ierusalem septuaginta anni.
Sasa katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Dario, mimi Danieli, nilikuwa najisomea vitabu vilivyo na neno la Yahweh, neno ambalo lilikuwa limemjia Yeremia nabii. Niligundua kwamba kungekuwa na miaka sabini hadi mwisho wa kuachwa kwa Yerusalemu ungefika.
3 Et posui faciem meam ad Dominum Deum meum rogare et deprecari in ieiuniis, sacco, et cinere.
Niliugeuza uso wangu kumwelekea Bwana Mungu, ili kumtafuta yeye kwa sala na maombi, kwa kufunga, na kuvaa nguo za magunia na kukaa katika majivu.
4 Et oravi Dominum Deum meum, et confessus sum, et dixi: Obsecro Domine Deus magne et terribilis, custodiens pactum, et misericordiam diligentibus te, et custodientibus mandata tua.
Nilimwomba Yahweh Mungu wangu, na niliungama dhambi zetu. Nilisema, “Tafadhali, Bwana, wewe ni Mungu mkuu na mwenye kuheshimiwa, wewe hutunza maagano na uliye mwaminifu katika kuwapenda wale wanaokupenda wewe na kuzishika amri zako.
5 Peccavimus, iniquitatem fecimus, impie egimus, et recessimus: et declinavimus a mandatis tuis, ac iudiciis.
Tumetenda dhambi na tumefanya yaliyo mabaya. Tumeenenda kwa uovu na tumeasi, tumegeuka upande kinyume na amri na maagizo yako.
6 Non obedivimus servis tuis prophetis, qui locuti sunt in nomine tuo regibus nostris, principibus nostris, patribus nostris, omnique populo terræ.
Hatujawasikiliza watumishi wako manabii walizungumza na wafalme wetu, viongozi wetu, baba zetu, na kwa watu wote wa nchi kwa jina lako.
7 Tibi Domine iustitia: nobis autem confusio faciei, sicut est hodie viro Iuda, et habitatoribus Ierusalem, et omni Israel, his qui prope sunt, et his qui procul, in universis terris, ad quas eiecisti eos propter iniquitates eorum, in quibus peccaverunt in te.
Kwako Bwana, kuna uadilifu. Hata hivyo, kwetu kuna aibu katika nyuso zetu, kwa watu wa Yuda na wale wanaoishi Yerusalem, na kwa Israeli yote. Hii ni pamoja na wale walio karibu na wale walio mbali katika nchi zote ambazo kwazo uliwatawanya. Hii ni kwasababu ya udanganyifu mkubwa tulioufanya kinyume chako.
8 Domine nobis confusio faciei, regibus nostris, principibus nostris, et patribus nostris, qui peccaverunt.
Kwetu sisi, Yahweh, kuna fedheha katika nyuso, na kwa wafalme wetu, na kwa viongozi wetu, na kwa baba zetu, kwasababu tumekutenda dhambi wewe.
9 Tibi autem Domino Deo nostro misericordia, et propitiatio, quia recessimus a te:
Kwa Bwana Mungu wetu kuna huruma na msamaha, kwa kuwa tumemwasi yeye.
10 et non audivimus vocem Domini Dei nostri ut ambularemus in lege eius, quam posuit nobis per servos suos prophetas.
Hatujaitii sauti ya Yahweh Mungu wetu kwa kutembea katika sheria zake alizotupatia kupitia watumishi wake manabii.
11 Et omnis Israel prævaricati sunt legem tuam, et declinaverunt ne audirent vocem tuam, et stillavit super nos maledictio, et detestatio, quæ scripta est in libro Moysi servi Dei, quia peccavimus ei.
Israeli wote wameiasi sheria yako na kugeukia upande, kwa kukataa kuitii sauti yako. Laana na viapo vilivyoandikwa katika sheria ya Musa, mtumishi wa Mungu, zimemwagwa juu yetu kwa kuwa tummetenda dhambi.
12 Et statuit sermones suos, quos locutus est super nos, et super principes nostros, qui iudicaverunt nos, ut superinduceret in nos magnum malum, quale numquam fuit sub omni cælo, secundum quod factum est in Ierusalem.
Yahweh ameyathibitisha maneno ambayo aliyasema kinyume na sisi na kinyume na viongozi wetu juu yetu, kwa kuleta juu yetu janga kubwa. Kwa kuwa chini ya mbingu yote haijawahi kufanyika kitu chochote ambacho kinaweza kulinganishwa na kile kilichofanyika huko Yerusalemu.
13 Sicut scriptum est in lege Moysi, omne malum hoc venit super nos: et non rogavimus faciem tuam Domine Deus noster, ut reverteremur ab iniquitatibus nostris, et cogitaremus veritatem tuam.
Kama ilivyoandikwa kwenye sheria ya Musa, baa hili lote limetupata, ingawa bado hatujaomba rehema kutoka kwa Yahweh Mungu wetu kwa kugeuka na kuacha maovu yetu na kuufuata ukweli wako.
14 Et vigilavit Dominus super malitiam, et adduxit eam super nos: iustus Dominus Deus noster in omnibus operibus suis, quæ fecit: non enim audivimus vocem eius.
Hivyo basi, Yahweh ameyaweka tayari maafa na ameyaleta juu yetu, kwa kuwa Yahweh Mungu wetu ni mwenye haki katika matendo yote anayoyafanya, ingawa bado hatujaitii sauti yake.
15 Et nunc Domine Deus noster, qui eduxisti populum tuum de terra Ægypti in manu forti, et fecisti tibi nomen secundum diem hanc: peccavimus, iniquitatem fecimus.
Basi sasa, Bwana Mungu wetu, uliwatoa watu wako katika nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu, na umejifanyia jina maarufu kwa ajli yako mwenyewe, hata siku hii ya leo. Lakini bado tumekutenda dhambi; tumefanya mambo ya hila. Kwasababu ya matendo yako yote ya haki,
16 Domine in omnem iustitiam tuam: avertatur, obsecro, ira tua, et furor tuus a civitate tua Ierusalem, et monte sancto tuo. Propter peccata enim nostra, et iniquitates patrum nostrorum, Ierusalem, et populus tuus in opprobrium sunt omnibus per circuitum nostrum.
Bwana, iache hasira na ghadhabu yako iwe mbali na mji wako Yerusalemu, mlima wako mtakatifu. Hii ni kwasababu ya dhambi zetu, na kwasababu ya uovu wa baba zetu, Yerusalemu na watu wako wamekuwa kitu cha kudharauliwa na wote wanaotuzunguka.
17 Nunc ergo exaudi Deus noster orationem servi tui, et preces eius: et ostende faciem tuam super sanctuarium tuum, quod desertum est propter temetipsum.
Basi sasa, Mungu wetu, sikiliza sala za mtumishi wako na maombi yake kwa ajili ya rehema; kwa ajili yako, Bwana ufanye uso wako ung'ae katika sehemu yako takatifu iliyoachwa ukiwa.
18 Inclina Deus meus aurem tuam, et audi: aperi oculos tuos, et vide desolationem nostram, et civitatem, super quam invocatum est nomen tuum: neque enim in iustificationibus nostris prosternimus preces ante faciem tuam, sed in miserationibus tuis multis:
Mungu wangu, fungua masikio yako na usikie; fumbua macho yako na uone. Tumeharibiwa; utazame mji unaoitwa kwa jina lako. Hatukuombi msaada wako kwasababu ya haki yetu, ila kwasababu ya rehema zako kuu.
19 Exaudi Domine, placare Domine: attende et fac: ne moreris propter temetipsum Deus meus: quia nomen tuum invocatum est super civitatem, et super populum tuum.
Bwana, sikiliza! Bwana, samehe! Bwana, tuangalie na ufanye jambo! Kwa ajili yako mwenyewe, usichelewe, Mungu wangu, kwa kuwa mji wako na watu wako wanaitwa kwa jina lako.”
20 Cumque adhuc loquerer, et orarem, et confiterer peccata mea, et peccata populi mei Israel, et prosternerem preces meas in conspectu Dei mei, pro monte sancto Dei mei:
Nilipokuwa ninaongea kwa kuomba na kuungama dhambi yangu na dhambi ya watu wangu Israeli, na kuwasilisha maombi yangu mbele ya Yahweh Mungu wangu kwa niaba ya mlima mtakatifu wa Mungu.
21 adhuc me loquente in oratione, ecce vir Gabriel, quem videram in visione a principio, cito volans tetigit me in tempore sacrificii vespertini.
Nilipokuwa ninaomba, mtu Gabrieli, ambaye nilikuwa nimemwona katika ndoto hapo awali, alipaa kwa kasi kushuka kuja nilipo, ilikuwa ni wakati wa sadaka ya jioni.
22 Et docuit me, et locutus est mihi, dixitque: Daniel nunc egressus sum ut docerem te, et intelligeres.
Alinipa ufahamu na aliniambia, “Danieli, nimekuja sasa ili nikupe utambuzi na ufahamu.
23 Ab exordio precum tuarum egressus est sermo: ego autem veni ut indicarem tibi, quia vir desideriorum es: tu ergo animadverte sermonem, et intellige visionem.
Ulipoanza kuomba rehema, amri ilitolewa na nimekuja kukueleza jibu, kwa kuwa unapendwa sana. Hivyo basi, tafakari neno hili na uufahamu ufunuo.
24 Septuaginta hebdomades abbreviatæ sunt super populum tuum, et super urbem sanctam tuam ut consummetur prævaricatio, et finem accipiat peccatum, et deleatur iniquitas, et adducatur iustitia sempiterna, et impleatur visio, et prophetia, et ungatur Sanctus sanctorum.
Miaka sabini na saba zimeamriwa kwa ajili ya watu wako na mji wako mtakatifu kukomesha hatia na kumaliza dhambi, na kuleta haki ya milele, na kutimiza maono na unabii, na kupaweka wakfu mahali patakatifu sana.
25 Scito ergo, et animadverte: Ab exitu sermonis, ut iterum ædificetur Ierusalem, usque ad Christum ducem, hebdomades septem, et hebdomades sexaginta duæ erunt: et rursum ædificabitur platea, et muri in angustia temporum.
Ujue na kufahamu kuwa tangu kupitishwa kwa amri ya kurudi na kuijenga upya Yerusalemu mpaka ujio wa mpakwa mafuta (atakayekuwa kiongozi), kutakuwa na majuma saba na majuma sitini na mbili. Yerusalemu itajengwa pamoja na mitaa yake na handaki, licha ya kuwepo kwa nyakati za shida
26 Et post hebdomades sexaginta duas occidetur Christus: et non erit eius populus, qui eum negaturus est. Et civitatem, et sanctuarium dissipabit populus cum duce venturo: et finis eius vastitas, et post finem belli statuta desolatio.
Baada ya miaka ya majuma sitini na mbili, mtiwa mafuta ataharibiwa na atakuwa hana kitu chochote. Jeshi la kiongozi ajaye litauangamiza mji na mahali patakatifu. Mwisho wake utatatokea kwa gharika, na kutakuwa na vita hata mwisho. Uharibifu umekwisha amriwa.
27 Confirmabit autem pactum multis hebdomada una: et in dimidio hebdomadis deficiet hostia et sacrificium: set erit in templo abominatio desolationis: et usque ad consummationem et finem perseverabit desolatio.
Atalithibitisha agano pamoja na watu wengi kwa miaka saba. Katikati ya miaka saba atakomesha dhabihu na sadaka. Baada ya chukizo la uharibifu atatokea mtu atakayeleta ukiwa. Mwisho kamili na uharibifu umeamriwa kutokea kwa yeye aliyesababisha ukiwa.”

< Danihelis Prophetæ 9 >