< Amos Propheta 4 >

1 Audite verbum hoc vaccæ pingues, quæ estis in monte Samariæ: quæ calumniam facitis egenis, et confringitis pauperes: quæ dicitis dominis vestris: Afferte, et bibemus.
Lisikilizeni neno hili, ninyi ng'ombe wa Bashani, ninyi mliomo katika mlima wa Samaria, ninyi mnaowakandamiza maskini, ninyi mnaowaponda wahitaji, ninyi muwaambiao waume zenu, “Tuleteeni vinywaji.”
2 Iuravit Dominus Deus in sancto suo: quia ecce dies venient super vos, et levabunt vos in contis, et reliquias vestras in ollis ferventibus.
Bwana Yahwe ameapa kwa utukufu wake, “Tazama, siku zitakuja kwenu wakati watakapowaondoa kwa ndoana, wa mwisho wenu na ndoana za kuvulia samaki.
3 Et per aperturas exibitis altera contra alteram, et proiiciemini in Armon, dicit Dominus.
Mtatoka kupitia mahali palipo bomolewa kwenye kuta za mji, kila mmoja wenu kwenda moja kwa moja kupitia hapo, na mtajitupa mbele ya Harmoni -hivi ndivyo asemavyo Yahwe.”
4 Venite ad Bethel, et impie agite: ad Galgalam, et multiplicate prævaricationem: et afferte mane victimas vestras, tribus diebus decimas vestras.
“Nendeni Betheli na uovu, hata Gilgali mkaongeza dhambi, leteni dhabihu zenu kila asubuhi, zaka zenu kila baada ya siku tatu.
5 Et sacrificate de fermentato laudem: et vocate voluntarias oblationes, et annunciate: sic enim voluistis, filii Israel, dicit Dominus Deus.
Toeni dhabihu za shukurani pamoja na mkate; tangazeni sadaka za hiari; watangazieni, kwa kuwa hii ndiyo iwapendezayo, ninyi watu wa Israeli -hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe.
6 Unde et ego dedi vobis stuporem dentium in cunctis urbibus vestris, et indigentiam panum in omnibus locis vestris: et non estis reversi ad me, dicit Dominus.
Nawapatia usafi wa meno katika miji yenu na na kupungukiwa na mkate katika sehemu zenu zote. Bado hamkurudi kwangu -hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
7 Ego quoque prohibui a vobis imbrem, cum adhuc tres menses superessent usque ad messem: et plui super unam civitatem, et super alteram civitatem non plui: pars una compluta est; et pars super quam non plui, aruit.
Pia nimeizuia mvua kutoka kwenu wakati bado kulikuwa na miezi mitatu kwa mavuno. Nikaifanya inyeshe juu ya mji, na kuifanya isinyeshe katika mji mwingine. Kipande kimoja cha nchi ilinyesha, lakini kipande kingine cha nchi ambapo haikunyesha palikuwa pakavu.
8 Et venerunt duæ et tres civitates ad unam civitatem ut biberent aquam, et non sunt satiatæ: et non redistis ad me, dicit Dominus.
Walizunguka miji miwili au mitatu kwenda mji mwingine kunywa maji, lakini hawakutosheka. Bado hawakunirudia mimi -asema Yahwe.
9 Percussi vos in vento urente, et in aurugine, multitudinem hortorum vestrorum, et vinearum vestrarum: oliveta vestra, et ficeta vestra comedit eruca: et non redistis ad me, dicit Dominus.
Nimewapiga kwa maradhi yanayosababisha kuvu. Wingi wa bustani, mashamba yenu ya zabibu, mitini yenu, na mizaituni-kuteketeza yote. Bado hamkunirudia hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
10 Misi in vos mortem in via Ægypti, percussi in gladio iuvenes vestros usque ad captivitatem equorum vestrorum: et ascendere feci putredinem castrorum vestrorum in nares vestras: et non redistis ad me, dicit Dominus.
Nimetuma tauni kwenu kama ya Misri. Nimewaua watoto wenu kwa upanga, kubeba farasi zenu, na kuufanya uvundo wa kambi zenu na kuingiza kwenye pua zenu. Bado hamkunirudia mimi -hivi ndivyo asemavyo Yahwe.
11 Subverti vos, sicut subvertit Deus Sodomam, et Gomorrham, et facti estis quasi torris raptus ab incendio: et non redistis ad me, dicit Dominus.
Nimeiangamiza miji miongoni mwenu, kama wakati Mungu alipoiangamiza Sodoma na Gomora. Mlikuwa kama kijinga kilichonyakuliwa kutoka kwenye moto. Bado hamkunirudia - asema Yahwe.
12 Quapropter hæc faciam tibi Israel: postquam autem hæc fecero tibi præparare in occursum Dei tui Israel.
Kwa hiyo nitafanya jambo baya kwako, Israeli; na kwa sababu nitafanya jambo baya kwako, jiandae kukutana na Mungu, Israeli!
13 Quia ecce formans montes, et creans ventum, et annuncians homini eloquium suum, faciens matutinam nebulam, et gradiens super excelsa terræ: Dominus Deus exercituum nomen eius.
Kwa kuwa, tazama, yeye atangenezaye milima pia ndiye aumbaye upepo, humfunulia mawazo yake mwanadamu, hufanya asubuhi kuwa giza, na kupakanyaga mahala pa juu ya dunia. Yahwe, Mungu wa majeshi, ndilo jina lake.”

< Amos Propheta 4 >