< Actuum Apostolorum 24 >

1 Post quinque autem dies descendit princeps sacerdotum, Ananias, cum senioribus quibusdam, et Tertullo quodam oratore, qui adierunt præsidem adversus Paulum.
Baada ya siku tano, Anania kuhani mkuu, baadhi ya wazee na msemaji mmoja aitwaye Tertulo, wakaenda pale. Watu hawa wameleta mashtaka dhidi ya Paulo kwa gavana.
2 Et citato Paulo cœpit accusare Tertullus, dicens: Cum in multa pace agamus per te, et multa corrigantur per tuam providentiam;
Paulo alipo simama mbele ya gavana, Tertulo akaanza kumshitaki na kusema kwa gavana, “kwa sababu yako tuna amani kuu; na kwa maono yako yanaleta mageuzi mazuri katika taifa letu;
3 semper et ubique suscipimus, optime Felix, cum omni gratiarum actione.
basi kwa shukurani yote tunapokea kila kitu ukifanyacho, Wasalam mheshimiwa Feliki.
4 Ne diutius autem te protraham, oro, breviter audias nos pro tua clementia.
Lakini nisikuchoshe zaidi, nakusihi unisikilize maneno machache kwa fadhili zako.
5 Invenimus hunc hominem pestiferum, et concitantem seditiones omnibus Iudæis in universo orbe, et auctorem seditionis sectæ Nazarenorum:
Kwa maana tumempata mtu huyu mkorofi, na anasababisha Wayahudi wote kuasi duniani. Tena ni kiongozi wa madhehebu ya Wanazorayo. (Zingatia: Sehemu ya maneno ya mstari huu 24: 6
6 qui etiam templum violare conatus est, quem et apprehensum voluimus secundum legem nostram iudicare.
Na tena alijaribu kulitia hekalu unajisi hivyo tukamkamata., haumo kwenye nakala bora za kale). (Zingatia: Mstari huu
7 Superveniens autem Tribunus Lysias, cum vi magna eripuit eum de manibus nostris,
Lisiasi, afisa, alikuja na akamchukua kwa nguvu mikononi mwetu., haumo kwenye nakala bora za maandiko ya kale).
8 iubens accusatores eius ad te venire: a quo poteris ipse iudicans, de omnibus istis cognoscere, de quibus nos accusamus eum.
Ukimwuliza Paulo kuhusu mambo haya, hata utaweza kujifunza ni kitu gani tumemshtakia.”
9 Adiecerunt autem et Iudæi, dicentes hæc ita se habere.
Wayahudi nao wakamshtaki Paulo, wakisema kwamba haya mambo yalikuwa kweli.
10 Respondit autem Paulus, (annuente sibi præside dicere): Ex multis annis te esse iudicem genti huic sciens, bono animo pro me satisfaciam.
Liwali alipompungia mkono ili Paulo aongee, Paulo alijibu, “Ninajua ya kwamba kwa miaka mingi umekua mwamuzi wa taifa hili, na nina furaha kujieleza mwenyewe kwako.
11 Potes enim cognoscere quia non plus sunt mihi dies quam duodecim, ex quo ascendi adorare in Ierusalem:
Waweza kuhakikisha kuwa hazijapita siku zaidi ya kumi na mbili tangu nilipopanda kwenda kuabudu Yerusalemu.
12 et neque in templo invenerunt me cum aliquo disputantem, aut concursum facientem turbæ, neque in synagogis, neque in civitate:
Na waliponikuta katika hekalu, sikubishana na mtu yeyote, na sikufanya fujo katika mkutano, wala katika masinagogi wala ndani ya mji;
13 neque probare possunt tibi de quibus nunc me accusant.
na wala hawawezi kuhakikisha kwako mashitaka wanayoyashitaki dhidi yangu.
14 Confiteor autem hoc tibi, quod secundum sectam, quam dicunt hæresim, sic deservio Patri, et Deo meo, credens omnibus, quæ in Lege, et Prophetis scripta sunt:
Ila nakiri hili kwako, ya kwamba kwa njia ile ambayo wanaiita dhehebu, kwa njia iyo hiyo ninamtumikia Mungu wa baba zetu. Mimi ni mwaminifu kwa yote yaliyoko kwenye sheria na maandiko ya manabii.
15 spem habens in Deum, quam et hi ipsi expectant, resurrectionem futuram iustorum, et iniquorum.
Nina ujasiri ule ule kwa Mungu ambao hata hao nao wanaungojea, kuja kwa ufufuo wa wafu, kwa wote wenye haki na wasio na haki pia;
16 In hoc et ipse studeo sine offendiculo conscientiam habere ad Deum, et ad homines semper.
na kwa hili, ninafanya kazi ili niwe na dhamira isiyo na hatia mbele za Mungu na mbele ya watu kupitia mambo yote.
17 Post annos autem plures eleemosynas facturus in gentem meam, veni, et oblationes, et vota,
Sasa Baada ya miaka mingi nimekuja kuleta msaada kwa taifa langu na zawadi ya fedha.
18 in quibus invenerunt me purificatum in templo: non cum turba, neque cum tumultu.
Nilipofanya hivi, Wayahudi fulani wa Asia wakanikuta ndani ya sherehe ya utakaso ndani ya hekalu, bila kundi la watu wala ghasia.
19 Quidam autem ex Asia Iudæi, quos oportebat apud te præsto esse, et accusare, si quid haberent adversum me:
Watu hawa ambao imewapasa kuwapo mbele yako sasa hivi na waseme kile walichonacho juu yangu kama wana neno lo lote.
20 aut hi ipsi dicant si quid invenerunt in me iniquitatis cum stem in concilio,
Au watu hawa wenyewe na waseme ni kosa gani waliloliona kwangu niliposimama mbele za baraza la kiyahudi;
21 nisi de una hac solummodo voce, qua clamavi inter eos stans: Quoniam de resurrectione mortuorum ego iudicor hodie a vobis.
isipokuwa kwa ajili ya kitu kimoja nilichokisema kwa sauti niliposimama katikati yao, ' ni kwa sababu ya ufufuo wa wafu ninyi mnanihukumu.”'
22 Distulit autem illos Felix, certissime sciens de via hac, dicens: Cum Tribunus Lysias descenderit, audiam vos.
Feliki alikuwa ametaarifiwa vizuri kuhusu njia, na akauahirisha mkutano. Akasema, “Lisia jemedari atakapokuja chini kutoka Yerusalemu nitatoa maamuzi dhidi ya mashitaka yenu.”
23 Iussitque Centurioni custodire eum, et habere requiem, nec quemquam de suis prohibere ministrare ei.
Ndipo akamwamuru akida amlinde Paulo, ila awe na nafasi na hata asiwepo mtu wakuwakataza marafiki zake wasimsaidie wala wasimtembelee.
24 Post aliquot autem dies veniens Felix cum Drusilla uxore sua, quæ erat Iudæa, vocavit Paulum, et audivit ab eo fidem, quæ est in Christum Iesum.
Baada ya siku kadhaa, Feliki akarudi na Drusila mkewe aliyekuwa Myahudi, akatuma kumwita Paulo na akasikiliza toka kwake habari za imani ndani ya Kristo Yesu.
25 Disputante autem illo de iustitia, et castitate, et de iudicio futuro, tremefactus Felix respondit: Quod nunc attinet, vade: tempore autem opportuno accersam te:
Ila Paulo alipokuwa akijadiliana naye kuhusu haki, kuwa na kiasi na hukumu itakayokuja, Feliki akapata hofu akajibu, “nenda mbali kwa sasa, ila nikipata muda tena, nitakuita.”
26 simul et sperans, quod pecunia ei daretur a Paulo, propter quod et frequenter accersens eum, loquebatur cum eo.
Muda uo huo, alitegemea kwamba Paulo atampa fedha kwa hiyo alimwita mara nyingi akaongea naye.
27 Biennio autem expleto, accepit successorem Felix Portium Festum. Volens autem gratiam præstare Iudæis Felix, reliquit Paulum vinctum.
Ila miaka miwili ilipopita, Porkio Festo akawa Liwali baada ya Feliki, ila Feliki alitaka kujipendekeza kwa Wayahudi, hivyo akamwacha Paulo chini ya uangalizi.

< Actuum Apostolorum 24 >